Saturday, March 14, 2015


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dr Alex Gehaz Malasusa, Mwenyekiti wa Harambee hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Mchechu na wachangiaji wakubwa katika harambee hiyo iliyofanyika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambapo jumla ya shilingi bilioni 1.6 kati ya shilingi bilioni 2 zinazohitajika zilipatikana. Michango hiyo ni ya kufanikisha upanuzi wa chuo hicho katika awamu ya pili.

 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wakuu wa majimbo ya KKKT, Wachungaji, Wainjilisti na wafanyakazi wa Parish na viongozi wengine
 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wakuu wa majimbo ya KKKT, Wachungaji, Wainjilisti na wafanyakazi wa Parish na viongozi wengine
 Rais Kikwete akipongezwa kwa kufanikisha harambee hiyo
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya harambee hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wake Mzee Arnold Kilewo ( wa kwanza kulia mbele) baada ya harambee hiyo iliyofanyika usiku huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam ambapo jumla ya shilingi bilioni 1.6 kati ya shilingi bilioni 2 zinazohitajika zilipatikana. Michango hiyo ni ya kufanikisha upanuzi wa chuo hicho katika awamu ya pili.


Dakika ya 42 Joel Wardalipachika tena bao la tatu na kuwaua zaidi QPR kwa kufanya 3-0 baada ya kupata mpira kutoka kwa Wilfried Zaha bao hilo lilihitimisha kipindi cha kwanza Crystal Palace wakienda mapumziko Vifua wazi kwa bao 3-0 kwenye Uwanja wao wa Nyumbani Selhurst Park, London wakiongozwa na Mwamuzi L. Mason.

James McArthur dakika ya 40 alipachika bao la pili na kufanya 2-0 baada ya kulishwa mpira na Yannick Bolasie.

W. Zaha kawapachikia bao mapema dakika ya 21 na kufanya 1-0 dhidi ya QPR

VIKOSI:
Crystal Palace starting XI: Speroni, Ward, Delaney, Dann, Kelly, McArthur, Ledley, Puncheon, Zaha, Bolasie, Murray
Subs: Hennessey, Hangeland, Maiappa, Souare, Ameobi, Sanogo, Gayle
QPR starting XI: Green, Furlong, Caulker, Onouha, Suk-Young, Wright-Phillips, Sandro, Henry, Phillips, Taarabt, Austin
Subs: McCarthy, Hill, Kranjcar, Hoilett, Vargas, Zamora, Grego-Cox

sylvestermarshAliyekuwa Kocha msaidizi wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Sylvester Marsh amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kocha huyo (Marsh) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya koo na hivi karibuni alisafirishwa kutoka Mwanza hadi jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, hali ya Marsh pia aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Kilimanjaro Stars pia alizinoa timu kadhaa za Ligi Kuu Bara iliendelea kuwa mbaya kadiri siku zinavyosonga mbele.
Pamoja na hivyo suala la afya yake liliendelea kuwa siri kubwa huku baadhi ya wadau wakisumbuka kutafuta wodi aliyolazwa.
Aliwahi kuugua taabani na kukawa na taarifa za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtelekeza. Lakini baadaye lilikanusha.
Mdau, Abdulfatah Saleh ambaye ni mmiliki wa Hoteli ya Sapphire Court ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ndiye alijitolea kumhudumia katika matibabu yake.
Ingawa alikuwa hapendi watu wajue, lakini mdau huyo ndiye alifanya kila, juhudi kuhakikisha Marsh anapata matibabu bora hadi alipopata nafuu na kurejea kwao Mwanza.
IMG_20150313_160039Na Amplifaya Amplifaya
Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania katika michuano ya ufukweni leo imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani mara baada ya kukubali kichapo kikali cha goli 6-2.
Walikuwa ni Tanzania ambao walianza mchezo katika morali nzuri ila mashambulizi yakiwa ya kushtukiza katika fukwe hizo za Escape One walifanikiwa kupata bao la kwanza kipindi cha kwanza na mfungaji akiwa ni Ally Rabbi.
Haikuchukua muda mrefu sana mchezaji Mwalimu Akida aliwainua mashabiki waliokuwepo katika fukwe hizo mara baada ya kujipatia timu hiyo goli la pili na kuwafanya Tanzania waongoze kwa goli hizo 2.IMG_20150313_162417
Waarabu wa Misri walirejea vizuri wakiwa kama wanacheza kwenye uwanja wao walimiliki mpira kwa asilimia kubwa zaidi huku wakifanya mashambulizi makali zaidi pia wakikosa magoli mengi.
Misri walifunga bao lao la kwanza kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji wao Islam Ahmed,  mapema baada ya kupata bao hilo waliendelea kujituma zaidi na hatimaye kupata bao lingine lililofungwa na Yehia Ally ambaye alifunga goli 4 peke yake leo, Goli jingine lilifungwa na Mohammed likiwa ni goli la 4 huku msumali wa mwisho ulimaliziwa na Yehia Ally na kukamilisha idadi ya mabao 6-2 kutoka kwa waarabu hao.
Tanzania sasa inabidi ijiandae kikamilifu kwenda kupambana na Mafarao hao wa Misri nchini kwao baada ya wiki moja.
 
Basi la Simiyu Express linalofanya safari zake Dar - Simiyu kila siku limepata ajali kwa kugonga mkokoteni unaosukumwa na ng'ombe na kuua mtu mmoja na ng'ombe wote leo saa sita mchana
mkoani Simiyu katika kijiji cha Salunda barabara kuu iendayo Shinyanga.
Hakuna abiria aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa ila kiongozi wa mkokoteni.dereva alifariki dunia na ng'ombe wake wawili walifariki pia.

Basi aina ya Scania lenye namba za asajili  T396 AMP Kampuni ya Simiyu Express mali ya Adinan Khan Mkazi wa Dar es salaam linalofanya safari zake Mkoani Simiyu-Dar es salaam, likiwa kwenye kichaka baada ya kupata ajali muda mfupi baada ya kutoka stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Inaelezwa kuwa baada ya kuacha njia likiwa katika mwendo kasi lilikutana na mkokota toroli la ngo'mbe akiwa katikati ya barabra maeneo ya Salunda kata ya Bariadi Mjini .

Kufuatia hali hiyo basi hilo lilimgonga mkokota toroli aitwaye Bahati Suti (25) Mkazi wa Musoma wilayani Itilima Mkoani Simiyu ambaye alifariki dunia  papo hapo , huku ngo'mbe 2 na wakipoteza uhai papo hapo.

 Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu  Charles Mkumbo amesema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na Ramadhan Hassan (30) mkazi wa Magomeni Kagera Jijini Dar es salaam, na kwamba kufuatia ajali hiyo gari hilo liliharibika kioo cha mbele pamoja na bampa na dereva wa basi  anashikiliwa na jeshi la polisi.
 Abiria wote 34 katika basi hilo ni wazima.

Baadhi ya wasamaria wema wakikokota mkokoteni uliosababisha ajali hiyo na kupoteza uhai wa dereva wake pamoja na Ngo'mbe 2.

Baadhi ya mashuhuda wakiangalia basi hilo

Mashuhuda.

Ngo'mbe akiwa amekufa


Baada ya basi kutolewa kichakani, muonekano wake lilivyopata ajali





Ajali mbaya ambayo imetokea Usiku wa kuamkia leo  maeneo ya CBE Dodoma..Basi la Osaka Raha ambalo lilikuwa linatoka mwanza kuelekea Dar,Chanzo cha ajali hiyo ni gari kubwa aina ya semitrela lilikuwa limekata tela lake katikati ya bara bara kuu inayoelekea Dodoma Inn, Na basi hilo inasemekana lilikuwa spidi sana na bila kujua kuwa katikati kulikuwa na t ela hilo na katika jitahada za kujaribu kulikwepa liliingia kwenye mtaro na kugonga mti ambao..Inasemekana hakuna aliyepoteza maisha ila majeuhi ni wengi na wamekimbizwa katika hospitali
 
 



MANCHESTER UNITED inafanya mkakati wa kumwezesha Radamel Falcao awe bora zaidi.
Hilo limetamkwa na Meneja wa Manchester United Louis van Gaal hii Leo.
Falcao, Straika wa Colombia mwenye Miaka 29, amefunga Bao 4 katika Mechi 20 tangu atue Man United mwanzoni mwa Msimu kwa Mkopo kutoka AS Monaco.
Akiongea hii Leo na Wanahabari kwa ajili ya Mechi yao ya Jumapili ya Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford na Tottenham Hotspur, Van Gaal ameeleza: "Tunatafuta suluhisho. Unaweza kuwa mzuri Nchi nyingine lakini ulipo ikawa tofauti! Hii si mara ya kwanza na ya mwisho!"
Baada ya kupigwa Benchi Jumatatu iliyopita kwenye Mechi ya FA CUP na Arsenal, Falcao alichezeshwa kwenye Kikosi cha Vijana U-21 dhidi ya Tottenham Siku ya Pili yake.
Meneja Van Gaal ameeleza hakumpeleka Falcao huko kumdhalilisha ila kumjenga zaidi baada ya Msimu uliopita kuumia vibaya Goti lake.
Falcao yuko kwa Mkopo Man United hadi mwishoni mwa Msimu kutoka AS Monaco ya France kwa makubaliano kuwa Uhamisho huo unaweza kuwa wa kudumu kwa Dau la Pauni Milioni 43.2.


Manuel Pellegrini ana hakika hatafukuzwa kazi mwishoni mwa Msimu.
Bosi huyo wa Manchester City yupo kwenye presha kubwa ya kuleta mafanikio na hasa Timu yake kutetea Taji lao la Ubingwa wa Ligi Kuu England.
Hadi sasa, Man City wameshatupwa nje ya Makombe mawili ya England, FA CUP na CAPITAL ONE CUP, na huko Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI wapo mguu nje baada ya kuchapwa 2-1 na FC Barcelona wakiwa kwao Etihad na watarudiana huko Nou Camp Wiki ijayo.
Huku kukiwa na tetesi Mtaliana Carlo Ancelotti, Bosi wa Mabingwa wa Ulaya Real Madrid, yuko mbioni kutua Etihad Msimu ujao, Pellegrini amesisitiza Mkataba wake ni hadi Juni 2016.
Jumamosi, City wako Ugenini kucheza Mechi ya Ligi Kuu England na Burnley huku wao wakiwa Nafasi ya Pili Pointi 5 nyuma ya Vinara Chelsea ambao wamecheza Mechi 1 pungufu.
Mwishoni mwa Desemba, Uwanjani Etihad, Burnley walitoka nyuma 2-0 na kutoka Sare 2-2 na tangu wakati huo City wameshinda Mechi 3 tu za Ligi.
Mbali ya presha yake binafsi, Pellegrini pia amelazimika kukanusha tuhuma za Magazeti ya Uingereza kuwa amempiga Benchi Nahodha Vincent Kompany baada ya kudaiwa kugombana na Mchezaji mwenzake Fernandinho.
Straika wa Chelsea Diego Costa akimsonga Ibrahimovic na kumshinikiza refa Bjorn Kuipers kutoa kadi nyekundu

Wachezaji wa Chelsea wakimzunguka Mwamuzi Kuipers wakati wa mchezo wa Uefa Champions Ligi dhidi ya PSG kitendoambacho kocha wa City amekiponda kwamba Wachezaji wake hawawezi kufanya Uwanjani.

Ibrahimovic mpaka alipewa kadi Nyekundu katika Mtanange huo ambao Chelsea waliondoshwa licha ya Chelsea kucheza 11 Uwanjani na wenzao pungufu 10 PSG.

waliotembelea blog