Basi
la Simiyu Express linalofanya safari zake Dar - Simiyu kila siku
limepata ajali kwa kugonga mkokoteni unaosukumwa na ng'ombe na kuua mtu
mmoja na ng'ombe wote leo saa sita mchana mkoani Simiyu katika kijiji cha Salunda barabara kuu iendayo Shinyanga. Hakuna
abiria aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa ila kiongozi wa
mkokoteni.dereva alifariki dunia na ng'ombe wake wawili walifariki pia.
|
Basi aina ya Scania lenye namba za
asajili T396 AMP Kampuni ya Simiyu Express mali ya Adinan Khan Mkazi wa
Dar es salaam linalofanya safari zake Mkoani Simiyu-Dar es salaam,
likiwa kwenye kichaka baada ya kupata ajali muda mfupi baada ya kutoka
stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
|
Inaelezwa kuwa baada ya kuacha njia
likiwa katika mwendo kasi lilikutana na mkokota toroli la ngo'mbe akiwa
katikati ya barabra maeneo ya Salunda kata ya Bariadi Mjini .
Kufuatia hali hiyo basi hilo lilimgonga
mkokota toroli aitwaye Bahati Suti (25) Mkazi wa Musoma wilayani
Itilima Mkoani Simiyu ambaye alifariki dunia papo hapo , huku ngo'mbe 2
na wakipoteza uhai papo hapo.
Kamanda
wa polisi Mkoani Simiyu Charles Mkumbo amesema basi hilo lilikuwa
likiendeshwa na Ramadhan Hassan (30) mkazi wa Magomeni Kagera Jijini Dar
es salaam, na kwamba kufuatia ajali hiyo gari hilo liliharibika kioo
cha mbele pamoja na bampa na dereva wa basi anashikiliwa na jeshi la
polisi.
Abiria wote 34 katika basi hilo ni wazima.
|
Baadhi ya wasamaria wema wakikokota mkokoteni uliosababisha ajali hiyo na kupoteza uhai wa dereva wake pamoja na Ngo'mbe 2.
|
|
Baadhi ya mashuhuda wakiangalia basi hilo
|
|
Mashuhuda.
|
|
Ngo'mbe akiwa amekufa
|
|
Baada ya basi kutolewa kichakani, muonekano wake lilivyopata ajali
|
0 maoni:
Post a Comment