Thursday, August 7, 2014



MWANASHERIA wa Luis Suarez anajiamini kuwa adhabu ya kifungo cha miezi minne cha mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez itapunguzwa na mahakama ya juu ya rufani ya michezo ya CAS ambapo rufani hiyo itasikilizwa kesho ijumaa.
Suarezi alikata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa shughuli zote za soka na FIFA na rufani yake itasikilizwa Agosti 8 mwaka huu katika mahakama hiyo iliyopo Lausananne, Uswizi.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alifungiwa baada ya kumng’ata beki wa Italia,Giorgio Chiellini wakati akiichezea Uruguay katika mechi ya kombe la dunia nchini Brazil na baada ya tukio hilo alijiunga na Barcelona kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 75 kutokea Liverpool.
Rufani aliyowasilishwa FIFA na Suarez alitupiliwa mbali mwezi uliopita na akaamua kukata rufani mahakama ya juu ya rufani ya michezo.
Maamuzi ya CAS yanatarajia kutolewa wiki ijayo. Kama atashinda maana yake Suarez ataanza mazoezi na wachezaji wenzake wiki mbili zijazo na atakuwepo katika mechi ya ya kwanza ya msimu mpya wa La Liga dhidi ya Elche, jumapili ya Agosti 24 mwaka huu.
Shirikisho la soka la Uruguay (UAF) lilimteua wakili wa Brazil, Daniel Cravo ili asimamie rufani dhidi ya kifungo ambacho kimemfanya Suarez akose mechi 9 za kimataifa. Mchezo mmoja wa kifungo umepita ambao ulikuwa dhidi ya Colombia hatua ya 16 ya kombe la dunia.
Cravo aliiambia Radio Globo akiwa Brazil kuwa anaamini adhabu hiyo itapunguzwa.
“Nadhani FIFA walitaka kuonesha kuwa wanaweza kuchukua hatua,” alisema.” Maamuzi hayakuridhisha ukilinganisha na matukio makubwa yaliyowahi kutokea huko nyuma. Hata kifungo cha (Zinedine) Zidane mwaka 2006 au yale ya Leonardo na (Mauro) Tassotti mwaka 199, adhabu haikuwa kubwa zaidi”.
“Tukio la Suarez ndio baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya kombe la duniua?
“Naamni kifungo kitakachoathiri kazi yake kwa ngazi ya klabu kitaondolewa. Hakuna kesi iliyoamuriwa kama hiyo katika historia.

“Naenda kujaribu na kupunguza kifungo cha kuichezea Uruguay—mechi tisa ni nyingi sana na zinaweza kumzuia kucheza mpaka 2016


Staying put: Real Madrid forward Karim Benzema has committed himself to the club until 2019
Bado nipo nipo kwanza!: Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, ameamua kuongeza mkataba mpaka mwaka 2019. 


KARIM Benzema ameamua kuzeekea Real Madrid baada ya kuongeza mkataba wake mpaka mwaka 2019.
Nyota huyu alikuwa anahusishwa kujiunga na baadhi ya klabu za ligi kuu, lakini biashara imekatika ghafla na sasa Mfaransa huyo ataendelea kudunda dunda Santiago Bernabeu.
Arsenal, Liverpool na Tottenham Hotspur zilikuwa miongoni mwa klabu nyingi za ligi kuu England zilizokuwa zikihusishwa kumsajili mshambuliaji huyo mwenye miaka 26, lakini mchezaji huyo wa zamani wa Lyon hatafanya baishara ya kucheza England msimu ujao.
Wanted: Benzema had been linked with a move to Liverpool, Tottenham or Arsenal this summer
Aliwindwa: Benzema alihusishwa kujiunga na klabu za  Liverpool, Tottenham au Arsenal majira haya ya kiangazi.


New: The Premier League have confirmed that referees will use vanishing spray this season
Mpya: Msimu ujao Ligi kuu nchini England imethibitisha matumizi ya dawa hii ya kupulizia.
BAADA ya kuthibitisha matumizi ya dawa maalumu ya kupulizia, ile inayokauka haraka na alitumiwa kombe la dunia, bodi ya ligi kuu England imeripotiwa kuagiza chupa 2,000 kwa ajili ya marefa msimu ujao, kwa mujibu wa gazeti za  Daily Telegraph.
Waamuzi watamaliza msimu ujao wakiwa na dawa hiyo ambayo itawasaidia kuweka alama umbali wa mita 10 kutoka kwenye mpira pale inapotokea adhabu ndogo na mabeki wanatakiwa kuweka ukuta.
Mkurugenzi mkuu wa ligi kuu, Richard Scudamore alisema: 'Tunaenda sambamba na maendeleo yanayoongeza ushindani na tulitazama kombe la dunia na kuona dawa ya kupuliza iliyotumika na waamuzi, hakika iliwasiaida marefa, wachezaji na wale wote waliokuwa wanaangalia mechi".


SIKU iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa burudani mbalimbali imewadia ambapo kesho Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa patakuwa hapatoshi wakati Tamasha la Usiku wa Matumaini litakapokuwa likichukua nafasi.
Mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali wakitunishiana misuli.
Akizungumza na Centre Spread, mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto alisema kuwa maandalizi yote yameshafanyika na tayari mkali wa muziki kutoka Nigeria anayetamba na ngoma ya Johnny, Yemi Alade ameshatua nchini, kinachosubiriwa ni burudani mwanzo mwisho.

“Kila kona ya burudani imeshakamilika hivyo kama wewe ni mpenzi wa ndondi kuna ngumi kati ya mabondia Mada Maugo dhidi ya Thomas Mashali, JB dhidi ya Cloud 112, Said Memba dhidi ya Khalid Chokoraa na wengineo.
Navy Kenzo.
“Wapenzi wa Bongo Fleva, kutakuwa na mfalme wao, Ali Kiba akiwa sambamba na mastaa kama Shilole, Madee, R.O.M.A, Meninah, Navy Kenzo, Scorpion Girls, Juma Nature na wengine kibao,” alisema Maloto na kuongeza:“Kwa wale wapenzi wa soka basi watakutana na mechi kabambe kati ya Wabunge Mashabiki wa Simba dhidi ya wenzao wa Yanga, Azam Fc dhidi ya Mtibwa, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie na wengine wengi.”

Ally Kiba.
Maloto aliongeza kuwa jukwaa litashambuliwa pia na wanamuziki wa nyimbo za Injili kama Martha Mwaipaja, Upendo Nkone, Angel na wengine wengi. Tamasha la Usiku wa Matumaini linatarajiwa kuanza kesho saa 5 asubuhi hadi saa 6 usiku ambapo wapenzi wa burudani watainjoi mambo yote kwa kiingilio cha shilingi elfu 5 tu.

  

Pepe Reina
Klabu ya Bayern Munich wameukubali mpango wa kumsajili mlinda mlango wa Liverpool, Pepe Reina.
Klabu hiyo ya ujerumani kupitia mtandao wao wa Twitter wameandika, "Mlinda mlango Pepe Reina yuko tayari kuhama kutoka Liverpool kuja FC Bayern kisha vipimo vya afya vitafuata.

Mwispainia huyo amepoteza nafasi yake kama mlinda mlango nambo moja wa Liverpool kutoka kwa Meneja Brendan Rodgers baada ya kumsajili Simon Mignolet ambapo msimu uliopita alikuwa Napoli.



Brendan Rogers atoa sababu za kufungwa na United katika International Champions Cup.
Meneja wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers, ameelezea hisia zake baada ya kupoteza mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya International Champions Cup dhidi ya Man Utd uliochezwa usiku wa kuamkia jana  mjini Miami nchini Marekani.

Rodgers, amesema matokeo ya mchezo huo hayajamvunja moyo wa kuendelea kukiamini kikosi chake ambacho August 16 kitaanza mshike mshike wa kusaka ubingwa wa nchini Uingereza, baada ya kukosa nafasi ya kutawazwa kuwa mabingwa msimu uliopita.
Amesema kikosi chake hakikucheza vibaya katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wengi, lakini makosa madogo madogo yaliwafanya wachezaji wake kujikuta wakiadhibiwa na Man Utd kwa kufungwa mabao matatu kwa moja.
Katika mchezo huo Liverpool walikuwa wa kwanza kupata bao kwa njia ya mkwaju wa penati uliopigwa na kiungo na nahodha Steven Gerrard lakini Man Utd waligeuka na kupata mabao matatu yaliyopachikwa wavuni na Wayne Rooney, Juan Mata pamoja na Jesse Lingard.

Katika hatua nyingine meneja huyo kutoka Ireland ya Kaskazini ameahidi kufanya usajili wa mchezaji mmoja ama wawili katika kipindi hiki cha kuelekea mwanzoni mwa msimu wa ligi.

Wachezaji ambao wanadhaniwa huenda wakawa njiani kujiunga na klabu hiyo ya Anfield ni beki wa kuliwa kutoka nchini Hispania na klabu ya Atletico Madrid Javier Manquillo pamoja na Alberto Moreno Pérez anaecheza nafasi ya beki wa kushito kwenye klabu ya Sevilla.
Wakati huo huo, Rodgers amethibitisha kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil Philippe Coutinho, anakaribia kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Liverpool baada ya kuonyesha kiwango kizuri tangu aliposajiliwa akitokea Inter Milan.


Mwakilishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (kushoto) akisalimiana na baadhi ya Wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara walipowasilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Juliana Yassoda akiwaelekeza jambo baadhi ya Wanamichezo waliwakirisha Tanzania kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara walipowasilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akifurahia jambo na baadhi ya wanamichezo walikuwa wamewakilisha nchini katika mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko Akizungumza kwa niaba ya Serikali na wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jan.Kulia ni Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi.

Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akizungumza na wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika jana katika Ukumbi uliopo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda na Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Rish Urio
Mwakilishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko akikabidhiwa Bendera ya Taifa na Kapteni wa Timu ya Taifa iliyoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola Bw. Seleman Kidunda, mara baada ya kurejea nchini jana jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bibi. Juliana Yassoda, Meneja wa Timu hiyo Muharami Mchume na Katibu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi
Baadhi ya wanamichezo walioshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland, wakiwa nje ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere mara baada ya kuwasili nchini jana jijini Dar es Salaam.



NYOTA wawili wa Klabu ya Barcelona ya Hispania, Neymar na Lionel Messi, Jana walirejea rasmi kikosini humo na  kuanza kujifua baada ya kumaliza mapumziko ya Muda kufuatia kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunnia huko Brazil. Wemeungana na wenzao Javier Mascherani na Dani Alves. Messi na Mascherano walikuwemo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Argentina iliyofanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia na kufungwa bao 1-0 na Ujerumani. Wakati Alves na Messi walihakikisha timu yao ya Taifa ya Brazil inafikia angalau nafasi ya nne bora ya michuano hiyo.

Neymar

Lionel Messi kwenye mazoezi

Kocha Mpya Luis Enrique




waliotembelea blog