MWANASHERIA wa Luis Suarez anajiamini kuwa adhabu
ya kifungo cha miezi minne cha mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez
itapunguzwa na mahakama ya juu ya rufani ya michezo ya CAS ambapo rufani hiyo
itasikilizwa kesho ijumaa.
Suarezi alikata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa
shughuli zote za soka na FIFA na rufani yake itasikilizwa Agosti 8 mwaka huu
katika mahakama hiyo iliyopo Lausananne, Uswizi.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alifungiwa baada ya
kumng’ata beki wa Italia,Giorgio Chiellini wakati akiichezea Uruguay katika
mechi ya kombe la dunia nchini Brazil na baada ya tukio hilo alijiunga na
Barcelona kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 75 kutokea Liverpool.
Rufani aliyowasilishwa FIFA na Suarez alitupiliwa
mbali mwezi uliopita na akaamua kukata rufani mahakama ya juu ya rufani ya
michezo.
Maamuzi ya CAS yanatarajia kutolewa wiki ijayo.
Kama atashinda maana yake Suarez ataanza mazoezi na wachezaji wenzake wiki
mbili zijazo na atakuwepo katika mechi ya ya kwanza ya msimu mpya wa La Liga
dhidi ya Elche, jumapili ya Agosti 24 mwaka huu.
Shirikisho la soka la Uruguay (UAF) lilimteua
wakili wa Brazil, Daniel Cravo ili asimamie rufani dhidi ya kifungo ambacho
kimemfanya Suarez akose mechi 9 za kimataifa. Mchezo mmoja wa kifungo umepita
ambao ulikuwa dhidi ya Colombia hatua ya 16 ya kombe la dunia.
Cravo aliiambia Radio Globo akiwa Brazil kuwa anaamini adhabu hiyo itapunguzwa.
“Nadhani FIFA walitaka kuonesha kuwa wanaweza
kuchukua hatua,” alisema.” Maamuzi hayakuridhisha ukilinganisha na matukio
makubwa yaliyowahi kutokea huko nyuma. Hata kifungo cha (Zinedine) Zidane mwaka
2006 au yale ya Leonardo na (Mauro) Tassotti mwaka 199, adhabu haikuwa kubwa
zaidi”.
“Tukio la Suarez ndio baya zaidi kuwahi kutokea
katika historia ya kombe la duniua?
“Naamni kifungo kitakachoathiri kazi yake kwa
ngazi ya klabu kitaondolewa. Hakuna kesi iliyoamuriwa kama hiyo katika
historia.
“Naenda kujaribu na kupunguza kifungo cha kuichezea Uruguay—mechi tisa ni nyingi sana na zinaweza kumzuia kucheza mpaka 2016
0 maoni:
Post a Comment