Saturday, November 8, 2014


LIGI KUU ENGLAND Wikiendi hii inaanza kwa Mechi ya Jumamosi ya mapema kabisa huko Anfield kwa Bigi Mechi kati ya Liverpool na Vinara wa Ligi Chelsea. Mechi hii, itakayoanza Saa 9 Dakika 45 Mchana, inazikutanisha Liverpool, walio Nafasi ya 7 kwenye Ligi, na Vinara wa Ligi Chelsea walio Pointi 12 mbele yao. Timu zote hizi mbili zinatoka kwenye Mechi za kati Wiki za UEFA CHAMPIONS LIGI wakati Liverpool, ikipumzisha Mastaa wao kibao, ilifungwa 1-0 huko Spain na Mabingwa wa Ulaya Real Madrid na Chelsea kucheza ugenini huko Slovenia na kutoka 1-1 na NK Maribor.
Kwenye Ligi, Wikiendi iliyopita, Liverpool ilichapwa 1-0 na Newcastlle na Chelsea kuifunga QPR Bao 2-1.
simu uliopita, kwenye Mechi kama hii, Chelsea iliitwanga Liverpool Bao 2-0.

Mara baada ya Bigi Mechi hii, zitafuata Mechi 4 zitakazoanza Saa 12 Jioni na mojawapo ni kule Old Trafford ambapo Man United, ambao Wikiendi iliyopita walichapwa 1-0 na Man City, watacheza na Crystal Palace iliyofungwa 3-1 na Sunderland.
Mechi ya mwisho Jumamosi ni ile itakayoanza Saa 2 na Nusu Usiku huko Loftus Road ambako QPR itacheza na Mabingwa wa England Man City ambao Juzi kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI, wakicheza kwao Etihad, walinyukwa 2-1 na CSKA Moscow.
Jumapili Ligi itaendelea kwa Mechi nne.


LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:

Jumamosi Novemba 8
15:45 Liverpool v Chelsea
18:00 Burnley v Hull
18:00 Man United v Crystal Palace
18:00 Southampton v Leicester
18:00 West Ham v Aston Villa
20:30 QPR v Man City

Jumapili Novemba 9
16:30 Sunderland v Everton
16:30 Tottenham v Stoke
16:30 West Brom v Newcastle
19:00 Swansea v Arsenal

waliotembelea blog