Wednesday, September 11, 2013

KATIKA ulimwengu wa mastaa wa Kibongo, kuna vijimambo kibao mojawapo ni wale wa kike kujiingiza kwenye mapenzi na kudanganywa kilaini kisha kushiriki mchezo wa kikubwa bila usalama (kinga).
Matokeo yake ni kuzalishwa na kuachwa solemba na sasa wanalea
watoto wao wenyewe bila baba zao. Unajua sababu? Ni ileile, yaani kupenda maisha ya ghali wakati hawana uwezo hivyo kujikuta wakijinasua kwa kujirahisisha kimapenzi kwa wanaume.
Leo Ijumaa Wikienda linakuletea mastaa 10 wa Kibongo waliozalishwa na kuachwa solemba wakilea watoto bila baba zao.
 
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
Alianzia kwenye filamu kisha akajiingiza kwenye muziki. Kwa mujibu wake mwenyewe, aliwahi kukiri kuwa  aliingia kwenye fani hizo kwa ajili ya kujitafutia kipato ili kulea wanaye. Aliolewa ndoa ya kwanza huko kwao Tabora na kuzalishwa mtoto mmoja kisha ndoa ikaota mbawa. Hakukaa muda mrefu akapata mwanaume mwingine ambaye alimpa ujauzito na kuzaa mtoto wa pili. Aliwahi kusema kati ya wanaume hao, hakuna anayemsaidia kulea.

ISABELLA MPANDA

Alianzia kwenye urembo, akatwaa Taji la Miss Ruvuma 2006 na sasa anafanya filamu na muziki. Ana watoto wawili wa kiume ambao amezaa na  wanaume tofauti. Anakiri kuwa anamshukuru Mungu kwa kuwa anaweza kuwapatia malezi bora wanaye kwa msaada kiduchu kutoka kwa wanaume hao.
 
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Alianzia kwenye uigizaji kisha urembo na sasa ameongezea muziki. Amezaa na Mkurugenzi wa Tuesday Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ ambapo walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kike na baada ya hapo mapenzi yakaisha. Kwa kuwa mapenzi yalikwisha, Jini Kabula alibaki na mwanaye akimlea mwenyewe japo Mr Chuz huwa anampiga ‘tafu’.

JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’
Alianzia kwenye urembo kisha akaingia kwenye filamu na muziki. Ana mtoto mmoja. Anakiri kuwa mtoto huyo alizaa na mwanaume mmoja ambaye hakumtaja kwa jina lakini baada ya hapo waliachana na anaendea kumlea mwanaye peke yake.

NURU NASSORO ‘NORA’

Mwigizaji huyo aliolewa na mwanaume wake wa kwanza ambaye alimzalisha mtoto mmoja wa kiume. Baadaye waliachana na kuanzia hapo hakumsaidia chochote kuhusu matumizi ya mtoto hadi mwanaume huyo alipofariki dunia na sasa anamlea mwanaye mwenyewe.

JACQUELINE DUNSTAN ‘JACK WA MAISHA PLUS’
Alipata umaarufu kupitia Shindano la Maisha Plus II kabla ya kujiingiza kwenye filamu. Aliachwa solemba baada ya kuzalishwa na mwanaume ambaye hadi sasa hana mawasiliano naye na hajui alipo hivyo analea mwanaye mwenyewe akiwa kwa bibi yake mkoani Morogoro.
 
SNURA MUSHI
Alianzia kwenye uigizaji kabla ya hivi karibuni kujikita pia katika tasnia ya filamu. Ana mtoto mmoja wa kike. Anakiri kuwa tangu akiwa mjamzito baba mtoto wake aliingia mitini. Mpaka sasa anamlea mwanaye mwenyewe kupitia sanaa ya filamu na muziki.

FAIDHA OMARI ‘SISTER FAY’

Japo hasikiki sana, mwanzoni alijikita kwenye muziki na hivi karibuni ameongezea nyingine ya uigizaji. Ana mtoto mmoja aliyejifungua mwaka jana. Anakiri kuachwa njia panda na mwanaume aliyemzalisha kwani hadi sasa anamlea mwanaye mwenyewe.
 
MAUNDA ZORRO
Alipata umaarufu kupitia muziki na baadaye akaongezea uigizaji. Ana mtoto mmoja na huwa hapendi kumwanika mwanaume aliyemzalisha ambapo mpaka sasa anaishi nyumbani kwa baba yake, mzee Zahir Zorro na hakuna dalili zozote za ndoa.

YVONNE-CHERRY NGATIKWA ‘MONALISA’
Mwigizaji huyu legendary pia ni Mtangazaji wa Radio Times FM. Alijaliwa kupata mtoto na prodyuza wa filamu za Kibongo, George Otieno ‘Tyson’ ambaye alikuwa ni mume wake wa ndoa. Baadaye waliachana akaolewa tena kwa ndoa ya Kiislam na kupata mtoto mwingine. Mpaka sasa anaishi na watoto wake na anawalea kupitia kazi zake za filamu na utangazaji.
 
Baada ya miaka miwili ya mipango na 
ujenzi, hatimaye jumba la kifahari la mcheza
 kikapu mwenye mafanikio na jina 
kubwa kutoka marekani, Michael Jordan 
 limekamilika. Mansion 
 hiyo iliyojengwa South Florida 
 imekamilika ikiwa na thamani 
ya dola za kimarekani 12.4 milioni.
Ona picha zaidi za Mansion hiyo:
 
Michael Jordan ni mcheza kikapu wa siku nyingi katika ligi ya NBA nchini Marekani, baadhi ya timu alizowahi kuchezea ni Chicago Bulls na Cleveland Cavaliers. Kwa sasa MJ ni mjasiriamali akimiliki hisa nyingi na pia ni mwenyekiti wa timu ya mpira huo ya Charlotte Bobcats.
Michael anatajwa na website ya NBA kuwa ni mcheza kikapu mkubwa ambae hajawahi kutokea, yaani "Greatest basketball player of all time"
True Fans Kwenye Kili Music Tour Kahama 
Wakipata Show Ya Ukweli, Ilifanyika Uwanja wa 
Taifa Wa Kahama, Next Ni Dar Es Salaam.

          Recho na madansa wake
 katika steji ya Kili Music Tour Kahama
  Ben Pol na Alice wakiimba wimbo wao mpya wa Waubani
                                 Ben Pol akiwaimbisha mashabiki kwa hisia
                                         Barnaba Boy jukwaani
                         Linex katika backstage ya Kili Music Tour

                   Izzo Bizness na Barnaba wakishambulia jukwaa kwa pamoja
                  Baada ya kushuka jukwaani 
mashabiki hawakutaka kupoteza 
nafasi ya kupiga nae picha.
     Kala Jeremiah
 akiwauliza mashabiki kama wameilewa Kikwetu kwetu
                                 Lady Jaydee na Profesa Jay wakiimba Joto Hasira
                             Profesa Jay akiifunga Kili Music Tour Kahama
       Mashabiki wakinyoosha mikono juu 
kuwashukuru wakali wa muziki waliopanda jukwaani
fid-q
Farid Kubanda alias Fid Q aka Ngosha The Don, he’s a real Hip Hop super star hapa Bongo baada ya mangoma yake kibao ku-bang kwa hewa.
Fid Q decided kuanzisha darasa la Hip Hop kwa lengo la kuwapa skillz wasanii katika utungaji pamoja na kufokafoka.
Lakini wakati Kubanda akiwa kwenye mission yake mwenye nyumba aliamua kumpiga bonge la boot na kumwonyesha mlango wa kutokea fastafasta.
Kweli baada ya Ngosha kustopishwa class pia ilisimama, lakini Fid Q sio mtu wa ku-give up coz currently ameongea.
“Narudisha darasa langu la hip hop baada ya sehemu niliyokodi mwazo kuwa na magumashi ya kupandishiwa kodi na nikaona ni-stop ku-provide ma-skillz, but now nimepata place maeneo ya TMJ Mikocheni na pako very suitable kwa wanafunzi.” Ngosha ze swagger Don added , “Class itaanza soon na wanafunzi 35 wapo permanently so ninawakaribisha na wengine wote who likes Hip Hop”


ll
Mwanadada anayefanya vizuri sana kwenye muziki na filamu,baby Madaha amelamba bingo ya uhakika na kampuni ya Candy n’ Candy Records Label ya jijini Nairobi iliyomsainisha mkataba msanii mwingine wa Tanzania Mr.Nice hivi karibuni.
Akizungumza kwa simu na bongomovies leo meneja wa msanii huyo  Joe Kariuki amesema kuwa  pamoja na msanii huyo kupewa mkataba huo wa million hamsini (50) pia wamempa mwanadada huyo gari ya kutembelea ya kisasa aina ya AUDI TT na nyumba  kali mitaa kijitonyama jijini  Dar es salaam.
Pamoja na hayo pedeshee huyo wa Mr.Nice ambaye ndio mmiliki wa studio hiyo amesema wanataka kumuhamishia msanii huyo jijini Nairobi nchini Kenya kwa kipindi cha mwaka mmoja ili afanye nao kazi huko kwani wamegundua kuwa anakubalika sana nchini humo na wapenzi wa muziki.
Baby madaha ambaye  anatarajia kutua nchini leo akitoka Nairobi pamoja na meneja wake kwa ajili ya kuachia video ya  wimbo wake wa kwanza aliofanya na Label hiyo uitwao (Summer Holiday) ambao umefanywa huko huko jijini Naironi
 Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', ambaye pia ni Mjumbe wa Nec CCM, Asha Baraka, akiwaka wakati akizungumza  na mtandao huu jana jioni alipokuwa akisimamia zoezi la kuwazuia wabomoaji kutobomoa nyumba na vibanda vya wananchi katika eneo hilo la Hanansifu bila kufikia muafaka kwa mazungumzo na wahusika.
Zoezi hilo la kubomoa eneo hilo ili kujengwa barabara ya mtaa lilianza tangu mwezi wa tano mwaka huu, ambapo wenye nyumba zizizopo eneo hilo baada ya mazungumzo na wasimamizi wa zoezi hilo na Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, walikubaliana na kuwekewa alama eneo linalotakiwa kubomolewa ili kupisha upanuzi huo.
Baada ya alama hizo ulifanyika ubomoaji na kuchimba barabara hiyo kana kwamba zoezi la ujenzi lilikuwa likianza muda mfupi tu baada ya ubomoaji, lakini cha kushangaza watu wao baada ya kubomoa waliondoka zao na kuacha eneo hilo likiwa na madimbwi makubwa yaliyojaa maji na kusababisha eneo hilo kutopitika kwa wenye magari na waenda kwa miguu.
Aidha baada ya kumalizika kwa ubomoaji huo, wahusika wenye nyumba zao na fremu za maduka eneo hilo, walikaa kwa muda wa miezi miwili na walipohakikishiwa kuwa zoezi hilo limemalizika na hakuna ubomoaji utakaoongezeka, walianza kukarabati nyumba na fremu zao upya ili kuendelea na biashara.
Cha kushangaza ghfla watu hao walirejea tena jana na kuchora alama mpya kwa kutumia mkaa, na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo jambo lililowaacha hoi wananchi wa eneo hilo na wenye frem zao, kutokana na kutotolewa kwa taarifa wala watu hao kutokuwa na kiongozi hata mmoja wa Eneo hilo yaani Diwani au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambao walitakiwa kuwepo ili kutoa ufafanuzi wa tukio hilo.
Lakini cha kushangaza wakati wa zoezi hilo, hakuwepo Mwenyekiti wala Diwani, jambo lililowafanya wananchi kuhoji juu ya uhalali wa zoezi hilo.
Wakati wa zoezi hilo Asha Baraka, alimpigia simu Diwani, Abasi Tarimba, lakini naye alimjibu kuwa hajui lolote kama Diwani na kumtumia namba ya simu ya mtu mwingine ili azungumze naye, wakati yeye ndiye hasa alitakiwa kuwapo eneo hilo na kuwatetea wapiga kura wake.
Hata hivyo watu waliokuwapo eneo hilo walishangazwa na kitendo cha jamaa hao kuendelea kumoboa upande mmoja wa eneo hilo huku wakikwepa ukuta wa ghorofa lililopo eneo hilo ambalo ni jipya lililojengwa hivi karibuni kwa kukwepa gharama, wakati alama za awali zinaonyesha kuwa hata ukuta wa ghorofa hilo ulitakiwa kubomolewa.
 Katapila likiendelea kubomoa....
 Asha Baraka akisimama mbele ya Frem zake eneo hilo kuwazuia jamaa hao kuendelea na zoezi hilo hadi upatikane muafaka na wahusika kwanza.
 Asha Baraka, akionyesha alama ya pili iliyowekwa jana na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo.....
 Wananchi wakimsikiliza Asha Baraka.....
 Sehemu ya madimbwi yaliyoachwa na wachimbaji hao mara ya kwanza ambayo kwa sasaa yameanza kukauka.
 Nyumba ya Asha Baraka (kushoto) inayotakiwa kubomolewa na (kulia) ndiyo Ghorofa lilalokwepwa ili kupindisha barabara hiyo jambo linalofanya kubomolewa kwa nyumba za upande mmoja.
 Asha Baraka, akionyesha alama za awali zilizowekwa kwa rangi nyekundu ambazo zinaonyesha kuwa hadi ukuta wa ghorofa unatakiwa kuondoka...
 Alama hiyo ipo kwenye kibanda hiki cha mkaa ambacho kipo sambamba na ghorofa hilo..
 Alama iliypchorwa kwa mkaa mara ya pili jana.......
Sehemu ya uhalibifu uliotokea jana wakati wa zoezi hilo.....katika moja ya fremu zilizopo eneo hilo..

waliotembelea blog