Friday, October 11, 2013

SERIKALI imesema inaangalia uwezekano wa kubadili sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambayo inaruhusu mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 15 badala yake iruhusu umri wa kuolewa uanzie miaka 18.
Aidha imeeleza kuwa ndoa za utotoni kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikirudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike, kutokana na wengi wao kuachishwa shule na kuozeshwa.
Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe wakati akizungumza katika majadiliano ya ngazi ya juu kuhusiana na ndoa za utotoni, ambapo jana ilikuwa ni Siku ya Mtoto wa Kike Duniani.
Waziri Chikawe alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya sasa mtoto wa miaka 15 anaruhusiwa kuolewa kwa idhini ya wazazi wake, jambo ambalo amewataka wadau wote kushirikiana kuhakikisha sheria itambue umri wa ndoa uwe ni miaka 18 na si vinginevyo. Hata hivyo, Waziri Chikawe alisema suala la kubadili sheria hiyo linatarajiwa kuchukua zaidi ya miaka mitatu, ili kukomesha kabisa ndoa za utotoni.
"Serikali inatambua uwepo wa ndoa za utotoni na hili ni tatizo kubwa sana, hivyo mbali na kurekebisha sheria lakini pia tunahitaji kuwapa wananchi wetu elimu zaidi kuhusiana na ndoa za utotoni ili hata wao wajue madhara yake," alisema Waziri Chikawe.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valerie Msoka alisema suala la ndoa za utotoni bado ni changamoto kwa nchi zote za Afrika, ambapo Tanzania inaonekana kuwa ni ya 20, jambo ambalo alisema ni lazima serikali iungane na taasisi mbalimbali kulitetea jambo hilo.
"Kikubwa ni elimu iendelee kutolewa kwa wananchi wote, pia tunafarijika kuona kuwa sasa serikali itaenda kubadilisha sheria ya ndoa kutoka miaka 14 kwenda miaka 18, japo napo ni bado ingekuwa hata miaka 21 lakini kwa kuanza si mbaya" alisema Msoka.

MOJA YA KIBANDA CHA MAMA NTILIE KIKIWA KIMEBOMOLEWA
BATI ZINONESHA HATA HANA MUDA MREFU TOKA ZIEZEKWE
MMILIKI WA MGAHAWA AKIELEZEA KUWA WALIAMBIWA NA BIBI AFYA KUWA WAEZEKE MABATI NA SI MATURUBAI CHAKUSHANGAZA HATA BATI LAKE JIPYA LIMENG'OLEWA HATA WALIPOOMBA WATOE KISTAARABU HAKURUHUSIWA
MAWAZO TELE; CHAKULA HAKIJAISHA, FAMILIA NITAILEAJE NA MAISHA YATAENDESHWAJE SASA...!
HIFADHI YA MUDA YA CHAKULA NA VYOMBO
ALIYEKUWA NA NGUVU YA KUSHAWISHI KUBOMOA MWENYEWE  BASI ALIJITOLEA MALI ZAKE KISTAARABU KWA MATUMIZI MENGINE YA BAADAE, KWA MNYONGE WALIMSAIDIA
KAZI NI KAZI NA SIE NDO WAZEE WA KAZI TUMETUMWA KUFANYA KAZI MJI UPENDEZE
(MATUKIO YOTE HAPO JUU NI MAENEO YA SKONGE ROAD NA YAFUATAYO NI MAENEO YA CLUB ROYAL NA KARIBU NA GETI LA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA MJINI TABORA)
KAMA KAWAIDA WABISHI HAWAKURUHUSU KUHARIBIWA MALI ZAO WALIZITOA LAKINI CHA KUSHANGAZA KUNA WENGINE HAWAKUGUSWA KABISA JAPO WANAJIHUSISHA NA BIASHARA YA AINA MOJA
OFISI YA MLEMAVU WA KUSIKIA AKISUBIRI KUONDOA OFISI HIYO MAENEO YA UKUTA WA CLUB ROYAL
MOJA YA KIBANDA KILICHOSALIMIKA BILA HATA KUGUSWA MAENEO KARIBU NA GETI TA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA
MAJANGA YAMEMKUTA RAMADHANI AMBAYE WAMEMBOMOLEA BANDA LAKE HAELEWI AFANYAJE; AMEKIRI KUWA BIBI AFYA ALIMPA UTARATIBU WA NAMNA YA KUFANYA BIASHARA KWA KUFANYA MABORESHO ZAIDI ASIUZE CHAKULA WAZIWAZI BALI AJENGE BANDA LINALOELEWEKA, LAKINI WAZEE WA KUSAFISHA MJI WAMEPITISHA FAGIO BILA HATA MAELEZO
HAPA NI NYUMA YA STENDI YA MABASI TABORA, AKINA MAMA NTILIE WAKIUZA VYAKULA ENEO LA WAZI PEMBEZONI MWA UKUTA
GARI LA WAZEE WA KAZI
Mkali ambae mwaka jana alidondoka kwenye Fiesta mkali Rick Ross ametangaza tarehe ya kuachia album yyake mpya inakuja inayoitwa “Mastermind”. Albam hiyo yam kali kutoka kampuni ya M.M.G The Bawse Rozay amesema albam hiyo ya “Mastermind” itatoka December 17 mwaka huu wa 2013. Albam ya Rick Ross “Mastermind” inafuata baada ya ile albam yake iliyofanya vizuri ya “God Forgives I Don’t” ambayo ilitoka mwaka jana 2012 mwaka huo huo pia alitoa kanda mseto (Mix tape) iliyokwenda kwa jina la “The Black Bar Mitzvah”. Mkali huyo Hold Me Back hit maker alitangaza tarehe ya kutoka kwa album hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa twitter akipost picha na updates.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. JAKAYA KIKWETE amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhahakisha kuwa shule zote za sekondari za kata, zahanati na vituo vyote vya afya nchini vinawekewa umeme haraka iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imeeleza kuwa Rais KIKWETE amesema kwa maeneo yenye umeme wa Gridi ya Taifa, taasisi hizo za umma zipatiwe umeme kutoka kwenye Gridi hiyo na kwa maeneo yasiyokuwa na umeme wa Gridi basi shule na taasisi hizo nyingine ziwekewe umeme wa jua.
Kupitia account yake ya Instagram msanii mkali wa bongo fleva anayeteka mabinti wengi mjini hapa amewaonyesha mashabiki wake gari yake mpya aliyoinunua. Gari hii ya Nissan ingawa sikuweza kujua kwa haraka haraka ni Nissan gani ameonekana akifurahia manufaa ya kazi zake anazozifanya kupitia jukwaani na aina ya maandishi anayoyaandika ili tu kujipatia ridhiki. Mbali ya hili gari kununua mtu mzima Mavoko anafumua mjengo mmoja wa hatari ingawa nimeambiwa nisiseme kwanza sehemu uliopo hadi ukamilike na kuamia ndio atasema amehamia wapi








Kampuni ya Ndege ya Fastjet imedaiwa kukiuka agizo la Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ya kutakiwa kukutana na mfanyabiashara Majaliwa Mbasa kumaliza mgogoro uliopo kufuatia kampuni hiyo kushindwa kumsafirisha kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg, Afrika Kusini. Kwa mujibu wa barua ya TCCAA yenye

kumbukumbu namba TCAA/0.10/350/139 iliyoandikwa Oktoba 2 mwaka huu na kusainiwa na James Mabala kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Fastjet, mamlaka hiyo iliagiza kampuni hiyo kukutana na mfanyabiashara huyo ndani ya siku saba ili kuyapatia ufumbuzi malalamiko yake. Hata hivyo, Mbasa hadi kufikia juzi siku saba ilizotoa TCAA zikiwa zimeisha kampuni ya Fastjet ilikuwa haijamwita wala wakili wake kampuni ya Legal Clinics Advocate. Mmoja wa viongozi wandamizi wa kampinu ya Fastjet, Brown Francsi, alipoulizwa alisema halifahamu. Mbasa alisema alikata tiketi Septemba 23, mwaka huu kwa


Wengi walioipata hii taarifa wanashangaa imekuaje ni viungo tu vya binadamu vimepatikana kwenye kontena zima vikiwa vinaingizwa Kenya? vinakwenda wapi? kazi yake ni nini?

Taarifa iliyoripotiwa na Citizen TV Kenya inasema Shehena hii iliyokamatwa baada ya kupitishwa kwenye bandari ya Mombasa inasemekana imesafirishwa na Mwanasiasa maarufu ambae kabla ya kukamatwa alisema ilikua na bidhaa za nyumbani ambapo ilipofika kwenye kituo cha ukaguzi wa mashehena cha Changamwe ilipatikana na vikaragosi vya mafuvu na mifupa ya binadamu ndipo amri ikatoka kontena likamatwe.
Baadhi ya mifupa ya binadamu iliyopatikana ni pamoja na mafuvu, miguu na mikono pamoja bidhaa za nyumba ambapo vyote kwa pamoja vilikua vinasafirishwa ambapo Afisa wa maswala ya Uhusiano mwema wa KRA Fatuma Yusuf alithibitisha kwamba hii shehena iliingia kutoka China siku ya pili ya October 2013 kabla ya kugundulika ilikua na vikaragosi vya kutisha ikiwemo mifupa ya binadamu.

Mpaka sasa uchunguzi wa shehena hili unaendelea lakini baadhi ya wakazi wa Mombasa wameonyesha wasiwasi wao na kusema kuna haja ya Serikali kutoa ripoti ya ibada za kishetani ambayo inasemekana kubuniwa na Rais Mstaafu Daniel Arap Moi miaka kadhaa iliyopita.


 
*Asema uamuzi wake haukushirikisha wizara nyingine
*Adai wadau walipaswa kupewa muda zaidi, aonya rushwa


WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amemuonya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kwa mara nyingine tena kuacha tabia ya kufanya uamuzi wa jambo lolote bila kushirikisha pande zinazohusika.

Mbali ya karipio hilo, Waziri Mkuu amewataka viongozi wengine wa Serikali, kuepuka mfumo usio shirikishi katika uamuzi wao kwa kuwa unasababisha migogoro ndani ya jamii na usumbufu kwa Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya mgomo wa wasafirishaji wa mizigo na abiria ulioanza Oktoba 5, mwaka huu, Pinda alisema Serikali imeamua kurejesha kwa muda wa mwezi mmoja asilimia tano ya uzito wa mizigo uliozidi kwenye mizani.


Alisema hatua zilizochukuliwa na Dk. Magufuli kufuta vifungu vilivyokuwa vikiruhusu asilimia tano zilifuata sheria, lakini tatizo lililojitokeza ni kutoshirikisha pande zinazohusika ili kushauriana na kupata uamuzi wa pamoja.

Alisema mbali ya kutoshirikisha pande hizo, uamuzi wa Dk. Magufuli ulikuwa wa ghafla kwa wasafirishaji kitendo ambacho kimewapa wakati mgumu wa utekelezaji, kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wameingia mikataba na wateja wao.

Chimbuko la mgogoro huu, ni tangazo la Dk. Magufuli alilotoa Oktoba mosi, mwaka huu la kuondoa ofa ya asilimia ya uzito uliozidi, baada ya uamuzi huo wadau wa usafirishaji wa malori na mabasi waliingia kwenye mgomo na kulalamikia hatua hiyo.

“Kutokana na mgogoro huu, nililazimika kukutana na Dk. Magufuli, baadhi ya mawaziri wa wizara zenye uhusiano na masuala haya, wanasheria na wataalamu wa masuala ya usafiri na uchumi.

Kilichoongeza mgogoro ni tafsiri ya vifungu vya sheria na kwenye kanuni ya 7 (2) na 7(3) ambacho kinaeleza wasafirishaji wa magari yenye uzito uliozidi, lakini upo ndani ya asilimia tano ya uzito unaokubaliwa kisheria, wanatakiwa kupunguza mzigo, kupinga na iwapo watashindwa kutekeleza, watatakiwa kulipia mara nne ya tozo za kawaida.

Sasa suala la asilimia tano, lilitokana na ombi la wadau wa usafirishaji kwa aliyekuwa waziri wa Ujenzi miaka ya nyuma na halikuwa sheria kamili, ndio maana limeondolewa baada ya kuonekana linatumiwa vibaya.

Nakubaliana na Dk. Magufuli, wapo baadhi ya wasafirishaji ni wakorofi na hawataki kufuata sheria…ndio maana walifanya mazoea ingawa wapo wengine wazuri na hao nawapongeza sana kutii sheria.

Maagizo
Pinda aliagiza kuanzia jana, wasafirishaji wa malori na mabasi waanze kutumia utaratibu uliokuwa ukitumika awali, huku akitoa onyo kwa atakayebainika kuzidisha uzito zaidi ya asilimia tano ya ofa anapaswa kupigwa faini.

Pia aliagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), iliyo chini ya Wizara ya Ujenzi, ipange utaratibu wa kupima mabasi katika mizani tofauti kati ya Kibaha na Mikese, ili kuondoa msongamano utakaokuwapo kwa siku mbili au tatu.

Alisema ofa hiyo itadumu kwa mwezi mmoja, wakati kamati itakayoundwa kwa kushirikisha wadau wote, itatafuta suluhisho la namna ya kuweka sheria hiyo vizuri ili kupata uamuzi wa pamoja.

Aliagiza mizani yote kugaguliwa ili kujua kama inafanya udanganyifu na watumishi wa mizani hiyo kwa lengo la kujipatia rushwa.

Aliwataka wajumbe wa kamati hiyo kwenda na lori la mizigo kwenye mizani kupima, ili kujihakikisha kama kompyuta hizo hazijachezewa kwa lengo la kuleta usumbufu.

Alisema kamati hiyo, itahusisha watu watano kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, Wizara ya Mambo ya Ndani, Viwanda na Biashara, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), pamoja na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Ofisi ya Waziri Mkuu na wataalamu wengine.

Alisema kamati hiyo, inapaswa kuja na majibu ya mabasi ya abiria kama yanastahili kupimwa kwenye mizani au la, kuangalia tozo ya asilimia tano katika uzito unaozidi kuondolewa au kubakia na masuala mengine muhimu yanayohusu Jumuiya ya Afrika Mashariki juu ya usafirishaji wa abiria na mizigo.

Hata hivyo, alisema suala hilo linapaswa kufanyiwa kazi kwa makini, kwa sababu linatishia usalama wa uchumi wa nchi na kipato cha mwananchi mmoja mmoja.

Alisema licha ya baadhi ya watumishi wa mizani waliokuwa wakijihusisha na rushwa kuondolewa kwenye vituo hivyo kwa asilimia 85 sawa na wafanyakazi 400, bado rushwa inaendelea kuwapo.

Aliagiza wizara na taasisi zinazohusika kulifanyia kazi suala la rushwa katika mizani za kupimia uzito, ili kuondoa sababu zisizo na msingi.

Mgomo wa mabasi na malori ulianza Oktoba 5, mwaka huu nchi nzima ikiwa ni siku nne baada ya Dk. Magufuli kutangaza rasmi kuondoa ofa ya asilimia tano ya uzito uliozidi, jambo ambalo lilisababisha mgogoro mkubwa.

WAFANYABIASHARA
Juzi wamiliki wa malori walizungumza na waandishi wa habari na kusema hawakubaliani na uamuzi uliochukuliwa na Dk. Magufuli.

Mmoja wa wamiliki hao, ni Davis Mosha kutoka Kampuni ya Delina Group, alisema wao kama wafanyabiashara hawajagoma bali wamepaki malori yao wasiharibu barabara. Aliongeza kuwa wao ni wadau wakubwa wa kulinda miundombinu ya barabara na wanachotaka ni sheria kufuatwa.

Naye Ibrahimu Ismail kutoka Kampuni ya Usangu, alisema wamepata usumbufu mkubwa kutokana na mizani kutokuwa na viwango vilivyo sawa.

Kwa upande wake, Faisal Edha kutoka Kampuni ya Overland Logistic, alisema asilimia tano haipo Tanzania pekee, bali ipo katika nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).




Mr. President, the faculty, staff, students, invited guests and the public at large. Allow me to express my gratitude, for the cordial welcome at your lovely campus. It is one of a kind, and If I could, I would have stayed much longer to learn more on your success that I could take back to our young people. The environment and the surroundings are as beautiful as the people themselves. Along the way, I have met great people with great hearts, and I thank you for that.

Likewise, receive greetings from the people of Tanzania. I was quite impressed with your level of research, and the homework you have done trying to know Tanzania, I was also particularly touched by some of you in the audience that knew the geography of my country; and even trying to challenge me . Mrs. Macquire, “People of Mto wa Mbu” are definitely proud of you for being such a good Ambassador. We thank you, and Tanzania needs more of you that will help in exposing it to the people of America.

The Samford community, my journey has been long and tedious; I have travelled through hills and valleys of trials and tribulations. However, due to the need and challenges we face as a nation, physical fatigue of travel would not stop me from marching forward. I am determined to work with my countrymen to see our nation of Tanzania reach the Promised Land.

Tanzania is a great and rich country, with rich culture and rich people at heart. Her people have sent me on a study tour. They have sent me to learn the secrets of your success as a society

Tanzania is one of the most blessed countries on the face of the earth. It has abundance of natural wealth, and for those who understand the world history, know that the best game parks are in Tanzania. It is the place believed to be the cradle of mankind.

Tanzania is the home of Mt. Kilimanjaro, Serengeti national park, Ngorongoro crater, and Olduvai Gorge where the first man is believed to have lived. We have some of the world best beaches; our people are very hospitable and extremely welcoming. I welcome all of you to Tanzania

For a long time, Africa has been known as a dark continent infested with disease, poverty, starvation, illiteracy and never endings wars. This might have been created in your minds with the images in your televisions. I can’t blame you, because this is the truth you know

However, this is far from the reality. Africa and Tanzania in particular is the new frontier. Tanzania is a country rich in natural resources and only lacks human capital. It is a country with rich land and plenty of water bodies
Many African leaders are believed to come to Washington and other western capitals begging for handouts known as foreign aid. This has created a notion in the minds of many that Africans are poor and lazy.

This is not the case.

Africa is transitioning from mismanagement, dictatorship and corruption that have plagued the continent. Corruption is the main vice depriving Tanzanians and other Africans a chance to a better education, better healthcare and economic prosperity.

Well, I am not here to beg, because my country is rich. I know clearly well that, foreign aid does not come cheaply. It comes with a condition of signing up our sovereignty

I am not here for foreign aid, and CHADEMA party which I represent does not believe on foreign AID. This is my party’s philosophy, and any sane human being would not want to live off handouts, or going around begging because foreign aid is only needed as short term relief for countries coming out of calamities. Rwanda needed help to so it could emerge out of the ruins of genocide. Once it did, it became less interested on the foreign aid now a success economic story in Africa

Foreign aid is a form of slavery which creates a false sense of entitlement. It confines a beggar into a psychological and mental prison of his own creation, becoming incapable to make any meaningful decision of his own. He does not think on how to get out of his difficulties as long as he knows that, someone somewhere will help him.

CHADEMA party believes that all too often, foreign aid creates dependency by the receiving country onto the giving country and winds up in the pockets of corrupt rulers.

Foreign aid money are your taxes, your sweat which should work for your benefit not for people sitting on their wealth. More important than your dollars, are your brain trust, investments and technological advantage. This is what we need to utilize our resources and also in planning for years beyond our non-renewable resources

Our country rich in resources is being exploited by foreign entities, while our President is busy trotting the world begging for mosquito nets. With our resources, we can make our own mosquito nets without them being donated to us. Chadema party which I represent is poised to changed that, and the most important tool we need is the development of human capital

We need our resources to benefit our people. We need to create jobs for our people, we need to improve our health care, we need to improve our education, our infrastructures, communication and economy as a whole. And this is only possible if can with the wealth that we have all we need is better education for our people

We are currently having inequitable trade, where far eastern countries are exporting their poor populations to compete for jobs with our citizens. They are even exporting to us their prisoners to work on our roads yet millions of our young men have no jobs. This is not possible in any civilize society, unfortunately, because our rulers have signed contacts shrouded in secrecy whose contents are only known to them

Some of these individuals have turn to insult us as a nation. They are now interfering on our sovereignty, publicly aligning themselves with political parties. A whole ambassador standing on a political platform to address a political rally, and has ignored the public call for him to leave the country!

This is not the kind of trade we are looking for. We are looking for partners that will work with us to develop our resources in order to benefit our people; Partners that will bring to our country new skills, and also create jobs for our graduates. We need your expertise so we can turn our country into a bread basket of Africa. America is the world’s land of milk and honey where everyone wants to be, that’s the model we want to learn from

Well, we have come to realize, that if you feed us today with your milk and honey, our meals for tomorrow may not be guaranteed. We instead want to know how you made your country into a land of milk and honey so we can be able to feed ourselves for unforeseeable future and also feed the rest of the world. We have the potential but lack the expertise, and the know how is what we need

Tanzania is not an island; it is part of the global community where all humans have the liberty to visit whenever they want. Our boarders are open for all, as long as our laws and culture are respected. All we need is trade partnership that will guarantee fifty-fifty trade, in which the country benefits equally with the investor.

The younger American generation, I am inviting you to visit Tanzania; I am talking to you as the investors of tomorrow. Come and explore the endless possibilities my country has for you. We need investors that will bring into our country, a set of skills and creativity to turn our hardwood into high quality, made in Tanzania products, as opposed to bringing cheap furniture made of plywood while hauling away our valuable timber

Chadema party believes on the free market economic philosophy in which individual creativity is rewarded. We need your partnership in fostering individual innovation within our people. We don’t need your tax money; neither do we need your mosquito net donations, we need your skills.

We don’t need shoe boxes, we need to know how to make our own shoes. We need your technological know how
CHADEMA party’s priority number one is education! Priority number two is education and so is the priority number three.

We believe on education to be the only way for Tanzania to rise from the abject poverty it is in today. We have no alternative but train our young people who will in turn, employ their intellectual creativity into full practice to enable Tanzania become an economic giant in a continent long forgotten

Samford is one of the American’s finest educational institutions. It is producing some of the world finest, from school teachers to the finest lawyers. It is my hope that we see your institution open its doors to our support and in preparing Tanzania’s aspiring scientists, teachers, and accountants to become innovators.

In our effort to make our country a unique success story, I am challenging you the young people to go out to the world, and open new trails for others to follow. Tanzania has its doors open for you.

Thank you all for listening.

Dr Wilbrod Peter Slaa is the General Secretary of the Main Opposition Party in Tanzania (CHADEMA).He came second during the 2010 Presidential elections which President Kikwete won. Dr Slaa is expected to contest in the year 2015 General elections.He is the number one critique of President Kikwete's government.


imageKamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akisalimiana na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Gilberto Sebregondi ambaye aliongoza ujumbe wa Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya katika ziara yao leo Oktoba 10, 2013 Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam ili kujionea namna ambavyo Jeshi la Magereza linazingatia kikamilifu masuala ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika Uendeshaji wa Magereza hapa nchini.
.image (1)Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akisoma hotuba yake fupi mbele ya Balozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi(aliyeketi mbele) pamoja na Mabalozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya wanaoonekana katika picha kabla ya kutembelea sehemu mbalimbali za Gereza Kuu Ukonga leo Jijini Dar es Salaam.
image (3)Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya wakiwasilikiza kwa makini Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam waliohukumiwa Adhabu ya Kunyongwa(hawapo pichani) ambapo wameiomba Jumuiya ya Ulaya kuendelea kupaza sauti na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili Adhabu hiyo hapa Nchini Tanzania iweze kuondelewa(wa pili kulia) ni Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Mhe. Dianna Melrose.image (2)Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( wa tatu kushoto mstari wa pili) akiongozana na Mabalozi mbalimbali wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya kuelekea sehemu ya Zahanati ya ndani inayohudumia Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam waliopotembelea leo Oktoba 10, 2013.image (4)Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za Gereza Kuu Ukonga leo Jijini Dar es Salaam(wa tatu kushoto) ni Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi ambaye aliongoza Ujumbe wa Mabalozi hao(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

waliotembelea blog