LIGI kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015 inatarajia kuanza kushika
kasi septemba 20 mwaka huu kwa timu 14 kuwania ubingwa unaoshikiliwa na Azam
fc.
Kanuni inasema kuwa ratiba ya ligi inatakiwa kuanikwa hadharani angalau
mwezi mmoja kabla ya ligi kuanza, ingawa inaweza kutangazwa hata miezi miwili
kabla kama inavyotokea ulaya.
Waendeshaji wa ligi kwa maana ya Bodi ya ligi kuu (TPL Board) na
Shirikisho la soka Tanzania, TFF wamekidhi matakwa ya kikanuni baada ya kufanikiwa
kuweka hadharani ratiba septemba 20 mwaka huu ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya
michuano kuanza.
Bodi ya ligi kuu Tanzania Bara (TPL Board) ndio wenye wajibu mkubwa wa
kuratibu ligi kuu na ligi daraja la kwanza.
Uchaguzi wa Bodi ya TPL ulifanyika Oktoba 25 mwaka jana. Oktoba
18 mwaka huo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa wakati huo, Hamidu Mbwezeleni
alitaja orodha ya mwisho ya wagombea waliokidhi vigezo katika uchaguzi huo.
Nafasi ya Mwenyekiti alikuwa ni Hamad Yahya Juma (Mtibwa Sugar),
Makamu Mwenyekiti ni Said Muhammad Said Abeid (Azam). Waliowania ujumbe wa Bodi
ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na Omary Khatibu Mwindadi
(Mwadui).
Baada ya uchaguzi kufanyika, Mbwezeleni aliwataja washindi ambapo Hamad
Yahya Juma wa Mtibwa Sugar alishinda na kuwa mwenyekiti wa Bodi ya ligi kuu na
Said Mohamed wa Azam fc alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti.
Wagombea hao wawili wa nafasi mbili za juu walitangazwa kupata ushindi
wa 100% ya kura zilizopigwa, lakini kwa mujibu wa Mbwezeleni baadhi ya wapiga
kura katika uchaguzi huo waliondolewa kwasababu hawakukidhi vikezo.
Mwenyekiti huyo wa kamati ya uchaguzi aliwatangaza Kazimoto Miraji Muzo
(Pamba) na Omary Khatibu Mwindadi (Mwadui fc).
Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamid Mbwezeleni
Kwa mujibu wa Tangazo la uchaguzi wa Bodi ya Ligi lililotolewa Oktoba 14
mwaka 2013 zilitangazwa nafasi tatu kama zinavyoonekana hapo chini pamoja na
masharti au sifa zinazotakiwa kuzingatiwa na waombaji:
1.
Nafasi
zilizotangazwa kugombewa ni hizi zifuatazo:
(i)
Mwenyekiti wa TPL
Board.
(ii)
Makamu
Mwenyekiti wa TPL Board.
(iii)
Wajumbe
wawakilishi wa Klabu za Ligi Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL
Board (TPL Board Management Committee), nafasi mbili (2).
2.
Mtu
yeyote anayeomba nafasi ya uongozi
katika TPL Board lazima atimize masharti yafuatayo:
(i)
Awe Raia wa
Tanzania
(ii)
Awe na
kiwango cha elimu kisichopungua Kidato cha Nne na cheti cha kuhitimu elimu ya
Sekondari.
(iii)
Awe na
uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano
(5).
(iv)
Asiwe na
hatia yoyote ya kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini.
(v)
Awe na umri
wa angalau miaka 21.
(vi)
Awe amewahi
kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji
wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Mkoa au Ligi daraja la kwanza.
(vii)
Kwa nafasi
ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa TPL Board awe Mwenyekiti wa kati ya Klabu
zilizoshika nafasi ya kwanza hadi ya sita kwenye Ligi Kuu kwa msimu uliopita
(2012/13).
(viii)
Kwa nafasi
za Mjumbe mwakilishi wa Klabu za Ligi
Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL Board awe Mwenyekiti wa Klabu
Daraja la Kwanza.
Mabingwa Azam fc walitoa kiongozi mmoja wa Bodi ya ligi kuu, Makamu mwenyekiti, Said Mohamed
Ukisoma masharti
yaliyotakiwa kuzingatiwa (namba vii) , inasema kwa nafasi ya mwenyekiti na
makamu mwenyekiti wa TPL Board, mgombea alitakiwa awe Mwenyekiti wa kati ya Klabu zilizoshika nafasi ya kwanza hadi ya
sita kwenye Ligi Kuu kwa msimu wa mwaka juzi (2012/13).
Kwa nafasi za Mjumbe mwakilishi wa Klabu za Ligi
Daraja la Kwanza kwenye Kamati ya Uongozi ya TPL Board awe Mwenyekiti wa Klabu
Daraja la Kwanza.
Hamad Yahya Juma (Mtibwa) na Said Mohamed (Azam) walikidhi sharti hilo kwasababu msimu
wa 2012/2013 timu zao zilikuwa katika nafasi sita za juu.
Kwa upande wa wajumbe, Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na Omary Khatibu
Mwindadi (Mwadui fc), pia walifuzu kigezo hicho kwasababu timu zao zilikuwa
ligi daraja la kwanza.
Lakini katika msimu wa 2013/2014 kulitokea mabadiliko kwa timu zilizotoa
viongozi hao.
Azam fc ilitwaa ubingwa kwa upande wa Ligi kuu wakati Mtibwa Sugar
ilishika nafasi ya 7 katika Msimamo.
MSIMAMO WA LIGI KUU MWAKA JANA
Standings
|
Rnk
|
|
Team
|
MP
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
+/-
|
Pts
|
|
|
1
|
|
|
26
|
18
|
8
|
0
|
51
|
15
|
36
|
62
|
|
|
2
|
|
|
26
|
16
|
8
|
2
|
61
|
19
|
42
|
56
|
|
|
3
|
|
|
26
|
13
|
10
|
3
|
33
|
20
|
13
|
49
|
|
|
4
|
|
|
26
|
9
|
11
|
6
|
41
|
27
|
14
|
38
|
|
|
5
|
|
|
26
|
9
|
11
|
6
|
23
|
20
|
3
|
38
|
|
|
6
|
|
|
26
|
10
|
8
|
8
|
28
|
32
|
-4
|
38
|
|
|
7
|
|
|
26
|
7
|
10
|
9
|
30
|
31
|
-1
|
31
|
|
|
8
|
|
|
26
|
10
|
1
|
15
|
23
|
40
|
-17
|
31
|
|
|
9
|
|
|
26
|
6
|
11
|
9
|
16
|
20
|
-4
|
29
|
|
|
10
|
|
|
26
|
6
|
10
|
10
|
26
|
33
|
-7
|
28
|
|
|
11
|
|
|
26
|
6
|
8
|
12
|
18
|
35
|
-17
|
26
|
|
|
12
|
|
|
26
|
6
|
7
|
13
|
20
|
39
|
-19
|
25
|
|
|
13
|
|
|
26
|
3
|
10
|
13
|
19
|
37
|
-18
|
19
|
|
|
14
|
|
|
26
|
3
|
7
|
16
|
18
|
39
|
-21
|
16
|
|
Kwa
kuzingatia msimamo huo, viongozi wa nafasi mbili za juu wa Bodi ya ligi kuu
kwasasa wanatakiwa kutoka klabu za Azam
fc, Yanga, Mbeya City, Simba, Kagera Sugar na Ruvu Shooting.
Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi
Kwa
kuzingatia sharti lilelile, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi kuu, Hamad Yahya Juma
(Mtibwa Sugar) amekosa sifa kwasababu timu yake msimu uliopita ilitoka nje ya
timu sita za juu. Kwa upande wa Said Mohamed ameendelea kuwa na sifa ya kuiongoza
bodi hiyo.
Kwa
upande wa wajumbe, Pamba fc imeshuka daraja kutoka ligi daraja la kwanza,
kwahiyo Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) kwa mujibu wa masharti
yaliyotangazwa amekosa sifa ya kuwa mjumbe.
Omary Khatibu Mwindadi (Mwadui fc), yeye anaendelea
kuwa kiongozi halali kwasababu timu yake ipo ligi daraja la kwanza.
Kwa hiyo Bodi ya ligi kuu ina viongozi wawili ambao
hawajakidhi masharti kwasababu ya timu zao kufanya vibaya msimu uliopita.
Tayari msimu mpya unatarajia kuanza septemba 20 na
tayari Bodi ya ligi kuu imetangaza ratiba, lakini Mwenyekiti wa Bodi hiyo
hatakiwi kuendelea kushika nafasi hiyo kwasababu timu yake haipo kwenye timu
sita za juu.
Kwa maana hiyo ilitakiwa kabla ya ligi kuanza, ufanyike
uchaguzi mwingine ili kuchagua viongozi wapya, au kama ni ngumu ungefanyika
uchaguzi mdogo ili kuziba nafasi ya mwenyekiti ambaye hana sifa na mjumbe mmoja
ambaye amekosa sifa kwa mujibu wa kanuni.
Kitendo cha kuruhusu ligi ianze bila uchaguzi ina
maana wanakiuka taratibu zilizowekwa.
Na kuzingatia masharti yaliyowekwa wakati wa
uchuguzi, Bodi ya ligi haina mwenyekiti na inatakiwa uchaguzi ufanyike pamoja
na kumpata mjumbe mmoja aliyepoteza sifa kutoka timu ya Pamba.
Hata wale wajumbe walioteuliwa na mwenyekiti wa
Bodi kwa ajili ya kuingia kamati ya utendaji ya TFF hawana sifa.
Mwenyekiti wa Bodi anaingia moja kwa moja kwenye
kamati ya utendaji kujadili mambo ya mpira, lakini inakuwaje aendelee kupata
fursa hiyo wakati hana sifa?
Tatizo linabaki pale pale kuwa viongozi wanaoongoza
mpira wa Bongo wana tabia ya kusahau mambo waliyojiwekea wenyewe.
Hamad Yahya alipoteza sifa, muda mfupi baada ya
msimu kumalizika ilitakiwa mchakato wa uchaguzi uanze mapema ili apatikane
mwenyekiti.
Lakini ratiba imetoka na ligi inaelelekea
kuanza na kiongozi muhimu wa Bodi hana
sifa.
Ifike wakati tukubali kukaa katika misingi ya
kanuni tuliyojiwekea, jambo lipo wazi na ukweli unafahamika, lakini kuna watu
wachache wanavunga kama hawaoni hivi.
Sidhani kama watu wote pale TFF wamesahau, lakini
kutokana na mfumo wa kubebana kwa urafiki na masilahi binafsi, watu wasiokuwa
na sifa wanaendelea kujadili na kuongoza mpira wa nchi hii.