Daktari wa klabu ya Chelsea Eva Carneiro amewashukuru masabiki wa
klabu hiyo ambao walichukua muda wao na kutuma ujumbe wa kumuunga mkono
baada ya kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho kumshutumu kufuatia tukio
lililojitokeza kwneye mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya England kwa
mabingwa hao dhidi ya Swansea.
Huku matokeo yakienda kinyume na matarajio ya kocha huyo kwenye
mchezo huo dhidi ya Swansea ambako Chelsea walibanwa na kutoka sare ya
2-2, Mourinho alimshutumu daktari wa timu baada ya kitendo cha kwenda
kumtibu Eden Hazard wakiwa akiwa ameumia .
Daktari wa Chelsea akiwashukuru mashabiki walioonyesha kumuunga mkono.
Mourinho alisema kuwa Daktari huyo alikosea kwa alichofanya kwani
kwenda kumtibu kiungo Eden Hazard kuliifanya timu yake ibaki na
wachezaji nane uwanjani hali ambayo iliwafanya wacheze kwa mazingira
magumu .
Wakati kitendo hicho kinatokea Chelsea ilikuwa imebaki na wachezaji 9
uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kipa Thibaut Courtois na
daktari huyo kwenda kumtibu Hazard ambaye sheria zinalazimu mchezaji
kutoka nje kabla ya kurudishwa uwanjani kwa ruhusa ya refa kuliifanya
Chelsea kubaki na watu 8 tu kwa takribani dakika mbili.
Mourinho akionyesha kukerwa wakati wa mchezo kati ya Chelsea na Swansea.
Mourinho alimshutumu daktari huyo kwa kusema kuwa baadhi ya watu
wanaokaa kwenye benchi la ufundi wanapaswa kuelewa jinsi ambavyo mchezo
wa soka unakwenda huku akiongeza kuwa Hazard hakuwa ameumia alikuwa
amechoka na alihitaji kuachwa na angenyanyuka mwenyewe.
Mourinho alikasirika baada ya daktari wa chelsea kwenda kumtibu Eden Hazard.
Watu wengi wametafsiri tukio hili kama dharau toka kwa Mourinho na
wamekuwa wakimtumia daktari huyo ujumbe wa kumuunga mkono ktiando
ambacho kimemgusa daktari huyo ambaye amejijengea umaarufu mkubwa akiwa
daktari pekee wa kike kwenye timu kubwa.