Monday, August 10, 2015


Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger ambae anafahamika kwa kutofanya manunuzi ya wachezaji kwa gharama ya juu, hadi sasa hajafanya usajili wowote mkubwa wakuongeza nguvu kikosi chake. Wengi walidhani baada ya kipigo cha goli 2-0 kutoka West Ham United huenda atafanya usajili mapema.
Wenger-main
Kocha huyo wa Arsenal amemsajili Peter Cech pekee kama mchezaji aliyeongeza nguvu kikosini licha ya kuwa mitandao mingi ya Ulaya inajua klabu ya Arsenal itafanya usajili mkubwa msimu huu licha ya Wenger kutokubali kuwa ana mpango wa kusajili.
Hata baada ya kufungwa mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu Uingereza na klabu ya West Ham United ya Uingereza bado Wenger anakikri kuwa walikuwa dhaifu dhidi ya West Ham lakini haamini kama ufumbuzi wa ubovu wa kikosi chake utapatikana kwa kusajili.
arsene-wenger-arsenal
“Hatukuwa na kiwango kizuri na cha kuvutia, kimsingi West Ham walicheza vizuri na hongera kwao natumaini tutarejea katika kiwango chetu haraka. Naweza rudia tena kama nilivyosema awali kama ufumbuzi pekee wa tatizo utakuwa ni kusajili tutafanya hivyo lakini baada ya kufungwa kama hivi sio muhimu kuangalia ufumbuzi wa tatizo nje ya kikosi”>>>Wenger

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog