Monday, August 10, 2015


.Huku Wachambuzi wakimnyooshea kidole Kipa mpya wa Arsenal Petr Cech kwa kufanya makossa yaliyoruhusa Bao zote walipopigwa 2-0 Leo kwao Emirates na West Ham katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Msimu mpya, Meneja Arsene Wenger amekataa kumshushia lawama Kipa huyo.
Cech, alienunuliwa kutoka Chelsea, aliutokea Mpira wa Frikiki ili aupanchi lakini akaukosa na kutoa mwanya kwa Cheikhou Kouyate kufunga kilaini kwa Kichwa Bao la kwanza na kisha shuti la mbali la Mauro Zarate kumhadaa Cech kwenye Posti yake ya karibu na kutinga.

Lakini Wenger, akiongea mara baada ya kipigo hicho, ameeleza: “Ni kutokuwa makini kwa pamoja. Kuna vitu vingi hapo. Nilijua kama ile frikiki itapigwa vizuri basi tutakuwa mashakani kutokana na tulivyojipanga, tulijiua wenyewe. Sijaongea na Cech lakini sikuona Mchezaji mwingine yeyote akicheza kwa kufurahisha hii Leo hivyo ni ngumu kumlaumu mmoja.” 
Aliongeza: “Pasi zetu hazikuwa nzuri. Leo lazima tujitazame wenyewe. Hatukuwa wazuri.”
Mara baada ya Wikiendi iliyopita kuwafunga Mabingwa Chelsea Bao 1-0 huko Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii, Wachambuzi wengi huko England waliipa nafasi kubwa Arsenal kuwemo rasmi kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa Msimu huu lakini kichapo hiki cha Leo kimeleta fikra nyingine.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog