Friday, September 20, 2013

Ray J aliwajia juu polisi akiwatuhumu kufanya utani kwenye mwili wa Whitney Houston baada ya muda mfupi kufariki walipoukuta mwili wake ndani ya Hoteli imeripoti TMZ.
Ra J ambae alikuwa anamahusiano ya kimapenzi na marehemu Whitney miezi michache kabla ya umauti kumkuta. Nje ya hoteli ambayo alifariki polisi na wanahuduma ya kwanza walifanya ujinga wao ndani ya hoteli hiyo, channzo kimoja ambacho kilikuwepo eneo la tukio kinasema Ray J alisikia polisi hao wakimkejeli marehemu Whitney Houston ikifuatiwa na vicheko vya nguvu ilimuuma sana Ray J ndipo alipojaribu kuingia kwa nguvu ndani ya chumba hicho lakini walimzuia

Chanzo cha stor hii kinasema Ray J alijaribu kuingia kwa nguvu kwenye chumba hicho baada ya kusikia vicheko zaidi akashindwa kuingia tena ndipo alipotolewa kabisa kutoka kwenye ile floor aliyekuwepo marehemu.

TMZ ndio walioripoti  kifo cha Whitney
usiku ule na mtu mmoja wa karibu na Whitney kwa hasira alikuwa akilalamika kwa familia na watu wengine kwamba watoa huduma ya kwanza walikuwa wakiongea maneno ya kejeli kwa  mwili wa marehemu Whitney

Taarifa zetu zinaonekana kuwa na uhakika kwa askari wa Beverly Hill ambae amefunguliwa kesi na CA Labor Dept kwamba askari wake alimfunua shuka iliyokuwa imefunika mwili wa marehemu Whitney na akasema “Damn. She’s still looking good. Huh?

. Vituo vya kisheria vinasema kwamba mashataka hayo hayana mantiki yoyote na kwamba polisi huyo hakusema neno lolote kuhusu mwili wa marehemu. TMZ wamejaribu kuwasiliana na Ray J lakini hwakufanikiwa..endelea kufuatilia hapa hapa utapata zaidi kuhusu story hii..


Nikiwa kama mtanzania halisi na mdau mkubwa wa michezo nchini hasa soka niliamua kujitosa katika kugombea uongozi ndani ya shirikisho la soka nchini katika uchaguzi wa shirikisho hilo ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao. 

Kwa sifa nilizonazo na mapenzi yangu niliamua kuomba kugombea katika nafasi ya kuingia kwenye kamati ya utendaji nikiuwakilisha mkoa wa Dar Es Salaam. Kwenye mchakato wa awali uliofutwa nilichukua fomu na kuzirudisha kama ilivyokuwa kwa wajumbe wengine lakini kwa bahati mbaya jina langu likakatwa kutokana na sababu za kukosa uadilifu kwa kile kilichoelezwa ya kwamba mara baada ya mchakato wa uchaguzi wa DRAF ambao pia nilishiriki kuwania nafasi ya kuuwakilisha mkoa wa Dar Es Salaam kwenye mkutano mkuu wa TFF na nikafanikiwa kupata kura 2,Nilizungumza hovyo juu ya namna uchaguzi ulivyofanyika kwenye vipindi vya michezo vya Clouds Media (Sports Xtra na Sports Bar ) . Nilikata rufaa na nikashinda lakini kutokana na matatizo mengine uchaguzi ukafutwa na FIFA na mchakato ukaamuriwa uanze upya. 

Mara ya pili nilichukua fomu na kuzirudisha tena, nikiwa nasubiria majibu ya fomu yangu nikawa nasikia taarifa kwamba jina langu lazima likatwe kutokana na sababu eti nili-publish barua ya FIFA kwenye mtandao wangu (www.shaffihdauda.com ). Sikuziamini taarifa hizo na nikazipuuzia lakini baada ya siku kadhaa TFF ikaitisha mkutano na waandishi wa habari wakatoa matokeo ya baada ya usaili uliofanywa na kamati ya uchaguzi,kwa upande wangu kupitia vyombo vya habari ikatangazwa ya kwamba jina langu kweli limepekwa kwenye kamati ya maadili kwa madai ya kukosa maadili kwa kuianika barua ya FIFA, nikajitetea na nikashinda na jina langu likarudishwa kwenye mchakato wa uchaguzi. 

Lakini hivi sasa kutokana na vyanzo vyangu vya taarifa ndani ya TFF kwamba nimeandaliwa zengwe lingine la kuondoa jina langu kwenye uchaguzi huo kwa madai ya kukosa uzoefu. Hii ni sababu isiyo na mashiko kwa kuwa mimi nina uzoefu mzuri unaonipa sifa za kugombea nafasi ninayoomba. 

Na hata kama sababu ingekuwa hiyo kwanini wasingesema tangu mwanzo walipokata jina langu mara mbili na nikawashinda. Hizi ni hila za baadhi ya watu wasiotaka kuona Shaffih Dauda anaingia TFF kwa sababu binafsi zisizo na faida kwa soka la Tanzania. 

Ninachotaka kuwaambia vikwazo vyao na mizengwe wanayoniwekea haitoweza kunikatisha tamaa katika harakati zangu za kutetea maslahi ya soka Tanzania. Kazi imejihidhirisha siku zote katika kupambana na maovu yote yanayorudisha maendeleo ya soka nyuma. Sasa ninachowaambia kwamba msijaribu kufanya mnachotaka la sivyo kwa mara nyingine tena mtanipa pointi 3 za mezani kwani nina uhakika UZOEFU NINAO NA NDIO MAANA KWENYE MICHAKATO YOTE YA AWALI KUANZIA DRFA MPAKA TFF SIKUWAHI KUONDOLEWA KWA KIGEZO HICHO ( USHAHIDI UPO IKILAZIMIKA KUUWEKA NITAUWEKA ILI WATANZANIA WOTE WAUFAHAMU ). SIKU NJEMA
Msanii wa muziki wa bongo fleva ambaye sasa ni mjasiriamali pia Anasteria Sanga Linah au muite Ndege Mnana amefunguka kuwa producer wa studio ya Bhitz Pancho Latino ndiye mwenye siri nzito ya penzi lake na msanii mwenzake Amini ambaye kwasasa penzi lao limekuwa stori ya kale baada ya kuachana. 

Linah amesema tokea wanaanza mapenzi yao Pancho ndiye alikuwa mtu pekee anayejua mambo mengi kuwahusu wao na jinsi walivyotumbukia katika penzi ambalo anasema yeye binafsi ndiye hasa alikuwa akimpenda Amini kupita kiasi japo baadaye akagundua kuwa hata mwenzake naye anamzimika na hivyo penzi likawa linasonga.

"Yaani we muulize Pancho yule ndio ana siri kubwa sana ya penzi langu na Amini,yaani jamani nilimpenda sana Amini mpaka nikakubali kuingia kwenye mapenzi na nilimpenda hasa kutoka moyoni,kuna vitu vingi nyuma yake ambavyo Pancho anajua",alisema Linah.

Msanii huyo mwenye sauti tamu kiasi cha kupachikwa jina la Ndege Mnana na msanii mkongwe Patricia Hillary ameendelea kufunguka kuwa wakati ameangukia katika penzi la Amini alikuwa anawachomolea wanaume wengi waliokuwa wanamtokea tena wenye pesa zao na wengine ni watu wazito lakini aliamua kutoka moyoni kwa dhati kuwa na Amini kwahiyo akawa anamtunzia heshima yake.

Anasema kama angekuwa macho juu kuna uwezekano mkubwa asingeendelea kuwa na Amini au angekuwa anamsaliti kwa kiasi kikubwa lakini moyo wake usio na tamaa ndio ulikuwa unamfanya aendelee kumpatia penzi la kweli.

Akavujisha siri kuwa Amini ndiye aliyemtibua na ndipo akapitisha uamuzi wa kujiweka pembeni kwasababu ambazo ni ngumu kuziweka hadharani lakini mpenzi wake huyo wa zamani anazijua na ni sababu ambazo haziwezi tena kulirudisha penzi lao japo anakiri kuwa aligundua kuwa mpenzi wake huyo wa zamani anampenda siku alipomtamkia kuwa mapenzi yameisha kila mmoja ashike lake.

Anasema katika kuonesha kuwa ameachana na Amini lakini hana bifu naye wakaamua kutoa wimbo wa pamoja wa Mtima wange.

Akizungumzia show anazofanya na Amini jukwaani wakiwa kama wapenzi anasema ni kuonesha kuwa hakuna bifu na hata mabusu anayopigwa na zilipendwa wake huyo anayapokea kwasababu anashindwa kuyapotezea jukwaani akiogopa kumtia aibu jamaa huyo mbele ya mashabiki na watu wengine.

Cheki video ya vitu vingine alivyofunguka katika interview niliofanya nae katika kipindi chaHatua Tatu cha Times fm.

waliotembelea blog