Monday, February 9, 2015


RATIBA:

Jumanne Februari 10

22:45 Hull vs Aston Villa
22:45 Sunderland vs QPR
22:45 Arsenal vs Leicester
23:00 Liverpool vs Tottenham

Jumatano Februari 11
22:45 Southampton vs West Ham
22:45 Stoke vs Manchester City 

22:45 Chelsea vs Everton
22:45 Manchester United vs Burnley
23:00 Crystal Palace vs Newcastle 

23:00 West Brom vs Swansea


Vijana wakifanya yao kwenye Uzinduzi jana jumapili tarehe 8 Feb, 2015. Ukiwa ni Uzinduzi maalum wa Shindano hilo la Nani Mkali Bukoba. Shindano linalokutanisha Makundi 10. Makundi matatu ya Kina Dada na makundi 7 ya Upande wa Vijana, Ikiwa ni Wasanii wa kucheza na Kuigiza.
Majaji.
Vijana wakiendelea kutoa burudani kwenye Uzinduzi wa Shindano la Nani Mkali Bukoba yaliyofnguliwa jana Jumapili kwenye Ufukwe wa Ziwa Victoria- Kiroyera Beach. Mashindano hayo yatachukua muda wa Wiki 9.
Watoto nao waliingia kwa wingi kuwaona wakubwa wao wakitoa burudani kwenye Uzinduzi huo
Moja ya Msanii kutoka kwenye Vikundi vinavyochuana hapa Bukoba kwenye Shindano la kumsaka mmoja mkali wao.


Majaji wakiendelea na Kazi yao na hapa wakiteta jambo mezani na Mwandaaji wa Shindano hilo Tesso Boy(kulia).



Ma Mc' wakiendelea na kazi kwenye Ufunguzi wa Mashindano hayo
Mashabiki waliingia kwa Wingi katika Eneo hilo Pendwa la Kiroyera Beach kwani Kiingilio kilikuwa Bure...
Mkurugenzi wa Kiroyera tours Bi Mary Kalikawe(kushoto) nae alikuwepo katika Maeneo yake kuona Vijana wanavyotoa Burudani katika Uzinduzi huo.
Burudani zikiendelea katika Fukwe hizo

Picha ya Pamoja ya Baadhi ya Wasanii waliojitokeza katika Uzinduzi huo

Msanii mkongwe Nchini, Inspector Haroun akisalimiana na Viongozi Meza kuu.
Msanii mkongwe Nchini, Inspector Haroun akisalimiana na Mgeni rasmi Mh. Diwani Anatory Amani

Msanii mkongwe nchini, Inspector Haroun
Taswira kamili.. Inspector Haroun Kutoka Jijini Dar es Salaam  akitoa Burudani mbele ya Mashabki wake katika uzinduzi huo wa Nani Mkali.


Mwandaaji wa Shindano hilo Teso Boy (kulia) akiteta na Msanii mkongwe Nchini, Inspector Haroun
Dj akiachia Muziki katika Burudani hizo za Ufunguzi wa Shindano la Nani Mkali Bukoba.

Taswira kamili ya Uzinduzi wa Mashindano hayo ya Nani mkali yaliyofanyika kwenye Ufukwe wa Ziwa Victoria Maarufu katika Eneo hilo Kiroyera Beach.


Kipa Nambari Wani wa Manchester United David De Gea, yupo kwenye mazungumzo na Klabu yake kuhusu kupewa Dili mpya na wala hajafikia makubaliano na Real Madrid kuhamia huko Spain. 
Habari hizi zimetobolewa na Wakala wa Kipa huyo kutoka Spain, Jorge Mendes, ambae ametupilia mbali dhana kuwa amekubaliana na Real Madrid kujiunga nao.
Hivi sasa De Gea, mwenye Miaka 24 na ambae pia ni Kipa wa Timu ya Taifa ya Spain, amebakiza kama Miezi 18 kwenye Mkataba wake na Man United na hilo lilianzisha uvumi mkubwa kuwa ataenda Real Madrid.
Akiongea na Kituo cha Redio Cadena Ser hapo Jana, Jorge Mendes, alisema: “Hivi sasa tupo kwenye mazungumzo na Man United kumpa Mkataba mpya lakini hatujasaini! Hamna ukweli kwamba yapo makubaliano kujiunga na Real!”
De Gea ni Mzaliwa wa Jiji la Madrid na alianza kuichezea Atlético Madrid tangu akiwa na Miaka 13 kisha kuichezea Timu ya Kwanza kwa mara ya kwanza Mwaka 2009 na Mwaka uliofuatia alikuwa langoni wakati Atletico inatwaa UEFA EUROPA LIGI na UEFA SUPER CUP.


www.bukobasports.com
TFF Leo imetoa Ratiba yenye marekebisho kidogo ili kuzipisha Klabu za Azam FC na Yanga kushiriki vizuri michuano ya Klabu ya CAF Barani Afrika. 

Azam inacheza Ligi ya Mabingwa, CAF CHAMPIONS LIGI, na itaanzia Nyumbani Februari 15 kwa kuikaribisha El Merreikh ya Sudan kwenye Uwanja wa Azam Complex Jijini Dar es Salaam wakati Yanga itacheza michuano ya CAF ya Kombe la Shirikisho na imepangiwa kucheza mechi ya kwanza Nyumbani dhidi ya BDF IX ya Botswana na Mechi hiyo itafanyika Februari 14 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga itarejea kwenye VPL hapo Februari 21 kwa kucheza huko Sokoine, Mbeya dhidi ya Mbeya City na Azam FC watacheza kwao Azam Complex Jijini Dar es Salaam Jumatano hii na Mtibwa Sugar na kisha kutocheza hadi Februari 22 dhidi ya Tanzania Prison pia hapo hapo Azam Complex.
Wikiendi hii ya Februari 14 na 15 zipo Mechi 5 za VPL.
Baada ya Mechi 13, Yanga ndio wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 25 wakifuatiwa na Azam FC wenye Pointi 22 kwa Mechi 12.

LIGI KUU VODACOM
RATIBA:
Jumatano Februari 11

Azam FC vs Mtibwa Sugar  

Jumamosi Februari 14
Ndanda FC vs Mtibwa Sugar
Coastal Union vs Mbeya City
Stand United vs Mgambo JKT

Jumapili Februari 15
Polisi Morogoro vs Simba
Kagera Sugar vs JKT Ruvu



MSIMAMO ULIVYO KWA SASA:
PosLogo &TeamPWDLGDPts
1ChelseaChelsea2417523356
2Manchester CityManchester City2414732349
3SouthamptonSouthampton2414372145
4Manchester UnitedManchester United2412841744
5Tottenham HotspurTottenham Hotspur241347643
6ArsenalArsenal2412661842
7LiverpoolLiverpool241167639
8West Ham UnitedWest Ham United241077837
9Swansea CitySwansea City24978-334
10Stoke CityStoke City24969-233
11Newcastle UnitedNewcastle United24879-631
12EvertonEverton24699-327
13Crystal PalaceCrystal Palace246810-826
14SunderlandSunderland244128-1224
15West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion245811-1223
16Aston VillaAston Villa245712-2022
17BurnleyBurnley244911-1721
18Hull CityHull City244812-1320
19Queens Park RangersQueens Park Rangers245415-1919
20Leicester CityLeicester City244515-1717

waliotembelea blog