Tuesday, July 21, 2015


Rais wa FIFA Sepp Blatter ambaye alitangaza dhamira ya kwamba atajiuzulu June 2 2015 baada ya shirikisho hilo litakapompata Rais mpya.
Leo hii amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya mchekeshaji wa Uingereza Simon Brodkin kumfuata akiwa katika Press Conference alafu akamwagia pesa huku akijifanya kuwa yeye ni mjumbe wa FIFA kutoka Korea Kaskazini.

Simon Brodkin ambaye anafahamika kwa kupenda kufanya utani katika maeneo mbalimbali, amewahi kufanya utani kama huo 2014 baada ya kujiunga na timu ya taifa ya Uingereza kama moja kati ya viongozi wa bodi na kutaka kusafiri na Kikosi cha Timu hiyo kilichokuwa kinasafiri kwenda Brazil kwenye Michuano ya Kombe la Dunia 2014.
Jamaa aliwahi pia kujiunga na kikosi cha Manchester City mwaka 2013 kama mchezaji wa timu hiyo na kufanya nao mazoezi kabla ya mechi yao na Everton kuanza



jose-mourinho-chelsea_e5smuyx0q03h1346wwab0ldj5
Iker Casillas amelelewa na Klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa miaka 25, ndani ya kipindi hicho ameichezea Klabu hiyo kwa miaka 16, lakini mambo yakabadilika baadae ambapo mwezi huu alitangaza kuhamia Klabu ya FC Porto ya Ureno kwa mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi.
Casillas amejiunga na FC Porto na atakuwa analipwa mshahara wa pound milioni 1.7 kwa mwaka.
mou-kicks-iker-514
Hata hivyo kufuatia uhamisho huo kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amelaumu uamuzi wa FC Porto kumsajili kipa wa Real Madrid Iker Casillas kwa mkataba wa muda mrefu na wenye maslahi mazuri… Mourinho ambaye aliwahi kuwa kocha wa Real Madrid kati 2010 hadi 2013 hana imani na uwezo wa Casillas kuna wakati aliwahi kumuweka benchi na nafasi yake kumpa Diego Lopez.
Iker19495000
Lakini pia Mourinho alishangazwa na maamuzi mengine ya FC Porto kumsajili kiungo kutokea klabu ya Marsseille ya Ufaransa Giannelli Imbula kwa dau la pound milioni 13.8.


2015 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu Tanzania, kila siku stori za Siasa zimekuwa kwenye headlines nyingi kuanzia Magazetini, kwenye TV, Radio na hata mitandaoni.
Mbunge James Lembeli alikuwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili.. kuna stori za baadhi ya Wabunge wametangazwa kuhama Vyama vyao, Lembeli kathibitisha kuhama CCM kwa maneno yake mwenyewe.

waliotembelea blog