Fainali
za Kombe la Dunia ni uwanja mpana. Ni mahali ambapo vipaji na vipaji
vya wanasoka duniani huonekana. Madalali wa kuvumbua na kununua
wachezaji [scouts] hufurika kwenye mashindano kama haya wakijua wazi
kabisa kwamba pale ndipo watakapoona “lulu” kwa ajili ya vilabu vyao.
Kwa maana hiyo kuna kila aina ya harakati za kimichezo na kuonyesha na
kuonyeshana vipaji. Hii sio kumaanisha kwamba wachezaji wote mahiri hapa
duniani walicheza katika fainali za Kombe la Dunia.La. Wapo wasakata
kabumbu kadhaa ambao hawakuwahi kugusa fainali hizi.Mfano ni George
Opong Weah na watu kama kina George West nk.
Lakini
wakati wengine wakionyesha vipaji ili wang’amuliwe na kubadilisha
maisha yao ya kisoka,wapo wale ambao wanashuka dimbani tayari wakiwa na
majina [superstars] na ambao dunia tayari inakuwa ikiwaangalia kwa
makini kutaka kujua na kuona kile watakachokifanya. Kila timu huwa na
mchezaji ambaye hutizamwa zaidi. Kwa umombo unaweza kumuita Key Player.
Kila timu,kwa kupenda au kutopenda,huwa ina star player. Hii haimanishi
kwamba katika timu hakuna wachezaji wengine wenye majina au wanaoweza
pia kuwa stars.La. Ni sheria ya mmoja mmoja inayozingatiwa hapa.
Kwa
mujibu wa wataalamu mbalimbali wa soka,wachezaji hawa 32 [mmoja kutoka
katika kila timu inayoshiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka huu] ndio
watarajiwa kuchomoza zaidi huko Brazil. Mpangilio huu hapa ni kutokana
na makundi ya FIFA World Cup 2014. NB: Orodha hii inaweza kubadilika
kwani imeandikwa kabla timu zote hazijathibitisha wachezaji wake 23
iliyowachagua mwisho. Wengine wanaweza kuumia katika siku hizi za mwisho
na hivyo kutokwenda Brazil.Zingatia.
Neymar-Brazil.
Hakuna ubishi kwamba Neymar anayechezea soka la
kulipwa Barcelona nchini Spain ndio gumzo kubwa kwa timu ya Brazil.
Anatarajiwa kuongoza mashambulizi ya The Kings Of Samba[Brazil]
Oribe Peralta-Mexico
Ingawa wachezaji wengine wa Mexico kama
Chicharito na Giovani dos Santos wanatajwa kama ma-star,Oribe Peralta
ambaye anacheza katika ligi ya nyumbani katika club ya Santos Laguna,
ndiye anaaminika hivi sasa kuwa star zaidi
Luka Modric-Croatia
Hakuna shaka kwamba Luka Modric ndiye mchezaji
star zaidi hivi sasa katika timu ya Croatia. Kiungo huyu ambaye hivi
sasa anachezea timu ya Real Madrid nchini Spain ameonekana wazi kuwa
tegemeo sio tu katika club bali nchi yake Croatia.
Charles Itandje-Cameroon
Ingawa ungetegemea mchezaji kama Samuel
E’too kuendelea kuwa star na tegemeo zaidi katika timu ya Cameroon,
golikipa Charles Itandje ndio tegemeo na ambaye wengi watapenda kumuona
akiokoa mikwaji. Charles ambaye anachezea timu ya Konyaspor nchini
Uturuki[kwa mkopo kutoka PAOK FC ya Ugiriki] aling’ara vilivyo katika
mchezo dhidi ya Tunisia wakati wa kuwania nafasi ya kwenda Brazil.Google
utaona alichofanya.
Diego Costa-Spain
Ingawa bado kuna utata kuhusu hali yake na kama
atakuwa fit kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia huko
Brazil,Diego Costa mshambuliaji mahiri wa timu ya Atletico Madrid
anatarajiwa kuwa nyota wa Spain. Lakini pia huenda akawa ndiye mchezaji
atakayezomewa zaidi huko Brazil kwani Diego ni mzaliwa wa Brazil na
angeweza kabisa kuchezea Brazil mwaka huu kama asingeamua kuchezea
Spain[pia ni raia wa Spain].Wabrazil hawajaipenda hiyo.
Arjen Robben-Holland[The Netherlands]Robben,mshambuliaji
mahiri ambaye hivi sasa anaendelea kuwika na timu ya Bayern Munich
nchini Ujerumani,ndiye mchezaji ambaye ni star zaidi na ambaye
ameonyesha kuwa na kile kiwango kinachoitwa “cha dunia”. Ana miaka 30
hivi sasa.HABARI ZAIDI BOFYA LINK HIYO HAPO