Steven Gerrard alionekana mweny huzuni baada ya kuchapwa 3-1 na West Ham
BRENDAN Rodgers ametetea kiwango cha Steven Gerrard, akisisitza kuwa nahodha huyo mkongwe wa Liverpool hahitaji kupumzika zaidi.
Gerrard mwenye miaka 34, amecheza kila
dakika msimu huu, zikiwemo mechi tatu katika wiki na kushuhudia
Liverpool akipoteza michezo miwili ya ligi kuu mbele ya Aston Villa na
West Ham.
Pia alicheza na kufunga penalti katika mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya wakali wa Bulgaria, Ludogorets.
Rodgers na wasaidizi wake wanafahamu kuwa katika mechi zote za ligi kuu Gabriel
Agbonlahor na Stewart Downing walifanikiwa zaidi na kumzidi kete
Gerrard ambaye alishindwa kugawa mipira kama alivyozoeleka.
Kocha wa wekundu wa Anfield, Brendan Rodgers akimpa maelekezo nahodha wake katika uwanja wa Upton Park
Liverpool wataikaribsiaha Middlesbrough
leo jumanne katika mechi ya Capital One cup, ambayo itamtumia nyota
wake aliye katika kiwango cha juu, Grant Leadbitter (kushoto)
Nahodha huyo wa zamani wa England
alikosea pasi 11 dhidi ya West Ham katika kipindi cha kwanza na
alishindwa kumiliki mpira mara 14.
Rodgers alikuwa na mipango ya
kumpumzisha Gerrard wakati Liverpool inacheza mechi ya Capital One leo
dhidi ya Middlesbrough, lakini kila kitu kimevurugika baada ya Jordan
Henderson na Philippe Coutinho kupata majeruhi.
Alipoulizwa kiwango cha nahodha wake
jana, Rodgers alisema: "Hakuna tatizo. Ni mchezaji muhimu kwetu. Kiwango
cha timu hakikuwa kizuri. Tumejitahidi kuimarisha kiwango chake kwa
misimu miwili iliyopita na wakati huo alikuwa anacheza soka la
kimataifa. Ukiangalia idadi ya mechi alizocheza, amekuwa mzuri sana".
"Yupo katika umri ambao tunatakiwa
kumtunza yeye binafsi. Tunamtaka kuhusika katika mechi kubwa kwasababu
ya uzoefu wake na siku zote tutafanya kila linalowezekana kumfanya awe
bora"
"Tutawafahamisha kama atapumzishwa. Baadhi ya wachezaji vijana watahusishwa katika kikosi".