Monday, September 22, 2014


Mathieu Debuchy atakuwa nje ya Uwanja kwa Miezi Mitatu baada ya kufanyiwa operesheni ya Enka yake.
Debuchy, mwenye Miaka 29, aliumia na kutolewa nje kwa Machela Arsenal walipocheza na Manchester City na kutoka Sare 2-2 hapo Septemba 13.

Akithibitisha habari hizi, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema operesheni ya Mchezaji huyo wa Kimataifa wa France ilienda vyema lakini kuwepo nje kwake kwa muda mrefu ni pigo kubwa sana kwao.
Debuchy alinunuliwa kutoka Newcastle mapema Julai mahsusi kumbadili Bacary Sagna aliehamia Man City mwanzoni mwa Msimu huu baada ya Mkataba wake kumalizika na mwenyewe kukataa kuongeza.

Wenger amesema: “Tutajua baadae pigo hili ni kubwa kiasi gani tukishajua tumembadilisha kivipi. Lakini ndio maana tulimnunua Calum Chambers!”

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog