Wayne Rooney ameibuka na kumpa sapoti kubwa Meneja wake David Moyes na kuwalaumu Wachezaji wenzake wa Manchester United kumwangusha Meneja wao huyo huku wakati huo huo akisisitiza England itafuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia Mwakani huko Brazil.
Amesema: “Ni wazi Meneja yuko kwenye presha kidogo lakini tunajua kama Timu ni sisi tuliomwangusha. Lazima tukusanye nguvu pamoja na kuonyesha upiganaji wetu tuliouzoea hapa!”
Rooney alisisitiza kuwa huu ni wakati wa mpito kwa sababu wana Meneja mpya na staili ni tofauti lakini ni juu yao kubadilika.
Akiongea baada ya kuifunga Sunderland 2-1 hapo Jumamosi, Rooney alisema: “Hilo ndio tulihitaji, kupata Pointi 3 na kuonyesha uimara wetu. Ushindi kama huo unabadilisha vitu!”
Pia Rooney alisisitiza yuko fiti kuichezea England Mechi dhidi ya Poland na Montenegro hapo Oktoba 11 na 15 za Kundi lao ambazo ndizo zitaamua kama watakwenda Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwakani baada ya kuzikosa Mechi mbili zilizopita dhidi ya Moldova na Ukraine baada kuumia usoni. Kocha wa United David Moyes