Monday, March 2, 2015


Kocha wa Juve Massimiliano Allegri APAGAWA Baada ya timu yake kutoka sare
Ndani ya Uwanja wa  Stadio Olimpico usiku huu ilishindukana  kutoa mshindi baada ya Wenyeji AS Roma kutoka Sare na Juventus ya Bao 1-1 kwenye Mechi ya Ligi Serie A.
Matokeo hayo yameifanya Juve iendelee kuongoza Ligi hiyo ya Italy ikiwa Pointi 9 mbele ya Timu ya Pili AS Roma.
Juve walifunga Bao lao kwa Frikiki ya Dakika ya 64 iliyotolewa baada ya Vasilis Torosidis kumchezea Rafu Vidal na Beki huyo wa AS Roma akapewa Kadi Nyekundu.
Licha ya kucheza Mtu 10 AS Roma walisawazisha Dakika ya 78 kwa Kichwa cha Seydou Keita alieunganisha Frikiki ambacho kilimgonga Marchisio na kutinga.

VIKOSI:
Juventus XI (3-5-2)
Buffon, Caceres, Bonucci, Chiellini, Evra, Lichtsteiner, Vidal, Marchisio, Pereyra, Tevez, Morata.
Roma XI (4-3-3)
De Sanctis, Torosidis, Manolas, Mapou, Cholevas, Pjanic, De Rossi, Keita, Gervinho, Totti, Ljajic

Patashika kipindi cha kwanza ambapo Timu zilienda mapumziko zikiwa 0-0.


Ligi Kuu England itaendelea Jumanne na Jumatano kwa Timu zote 20 kucheza Mechi.
Hapo Jumanne Machi 3 zipo Mechi 3 kuanzia Villa Park ambako Aston Villa watacheza na West Bromwich Albion wakati Hull City wataivaa Sunderland na Southampton kucheza na Crystal Palace.
Jumatano zipo Mechi 7 ambapo Mabingwa Watetezi Manchester City watakuwa kwao kucheza na Leicester City huku Jirani zao, Man United, wakiwa Ugenini huko Saint James Park kucheza na Newcastle.
Nao Vinara wa Ligi, Chelsea, watakuwa Ugenini huko Upton Park kucheza na West Ham na pia Arsenal kuwa Ugenini kuivaa QPR wakati Liverpool wako Nyumbani kucheza na Burnley.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumanne Machi 3

22:45 Aston Villa v West Brom
22:45 Hull v Sunderland
22:45 Southampton v Crystal Palace

Jumatano Machi 4
22:45 Man City v Leicester
22:45 Newcastle v Man United
22:45 QPR v Arsenal
22:45 Stoke v Everton
22:45 Tottenham v Swansea
22:45 West Ham v Chelsea
23:00 Liverpool v Burnley


Na Bertha Lumala, Dar es Salam
Kipigo cha mabao 3-0 ugenini dhidi ya El-Merrikh ya Sudan, kimemponza kocha Joseph Omog baada ya uongozi wa Azam FC kuamua kumtimua.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa facebook wa Azam FC muda mfupi uliopita, Uongozi wa Azam FC umetangaza kumtimua raia huyo wa Cameroon.
Taarifa hiyo inasomeka: “Uongozi wa Azam FC unatangaza kuachana na kocha wake mkuu Joseph Omog baada ya kuwa naye kwa miezi 14.
Omog aliyeipa Azam FC ubingwa wa kwanza msimu uliopita ameondoka pamoja na msaidiI wake Ibrahim Shikanda.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya George Best Nsimbe.”


Jose Mourinho ameelezea nia yake kutwaa Mataji mengine mara baada ya Jana Uwanjani Wembley Jijini London Timu yake Chelsea kuichapa Tottenham Hotspur Bao 2-0 na kubeba Capital One Cup likiwa ni Kombe lake la kwanza tangu arejee kwa mara ya pili Klabuni Chelsea.
Bao za Chelsea hapo Jana zilifungwa na Nahodha John Terry na Kyle Walker aliejifunga mwenyewe.kiongea mara baada ya Mechi hiyo, Jose Mourinho alisema: “Mie ni kama mtoto alieshinda mara ya kwanza. Ni ngumu kwangu kuishi bila Mataji. Nahitaji kutwaa Makombe!”
Mourinho, ambae alikuwa Chelsea kwa mara ya kwanza kati ya Miaka 2004 na 2007 na kurejea 2013, sasa ameshatwaa Vikombe 7 akiwa na Chelsea.
Chelsea hivi sasa wanaongoza Ligi Kuu England wakiwa Pointi 5 mbele ya Mabingwa Watetezi Manchester City huku wakiwa wamecheza Mechi 1 pungufu.

CAPITAL ONE CUP
WASHINDI WALIOPITA:

1961 - Aston Villa
1962 - Norwich City
1963 - Birmingham City
1964 - Leicester City
1965 - Chelsea
1966 - West Bromwich Albion
1967 - Queens Park Rangers
1968 - Leeds United
1969 - Swindon Town
1970 - Manchester City



Jeneza lenye mwili wa aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM,Marehemu Kapteni John Komba likiwa kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam,wakati wa shughuli ya kuaga.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Litui wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma.

Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na wake zake Mama Asha na Mama Zakhia wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Rais Mstaafu wa awamu ya pili,Alhaj Ali Hassa Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania,Luteni Kanali Samuel Ndomba akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba,mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. Jenista Mhagama akitoa heshima za mwisho akifuatana na Naibu IGP,Abdulrahman Kaniki.

Kingunge Ngombale–Mwiru akitoa heshima za mwisho.

Kamanda Kova.

Baadhi wa Waheshimiwa Wabunge wakiifariji familia ya Marehemu.

Mhe. Ole Sendeka akibubujikwa na machozi kuondokewa na Mbunge mwenzake.
Soma Zaidi Hapa »

Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM marehemu John Damiano Kumba ukipokelewa katika uwanja wa ndege wa Songe na umati mkubwa wa waombolezaji wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Mhe.Mwambungu,Mhe.John Nchimbi,Mbunge wa Songea Mjini,na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Kazi Maalum)Mark Mwandosya,kulia. Marehemu anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Kesho. Picha na Michuzi blog

waliotembelea blog