Wednesday, March 18, 2015



Ligi Kuu Vodacom, VPL, Leo ipo dimbani kwa Mechi 3 za Jijini Dar es Salaam, Mbeya na huko Tanga huku Yanga wakiwa na nafasi poa kutwaa uongozi wakishinda.
Yanga Leo watakuwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Kagera Sugar na ushindi kwao utawashusha Mabingwa Watetezi Azam FC kutoka kileleni.


Lakini Kagera Sugar ni Timu ngumu ambayo katika Mechi ya kwanza ya Ligi Msimu huu iliichapa Yanga 1-0 huko Kaitaba, Bukoba.
Simba Leo hii wako huko Mkwakwani Tanga kuivaa Mgambo JKT wakiwa kwenye wimbi la ushindi wa Mechi 3 mfululizo kwa kuzichapa Tanzania Prisons 5-0, Yanga 1-0 na Mtibwa Sugar 1-0 ambalo limewafanya wajikite Nafasi ya 3.
Huko Sokoine, Mbeya, wana wa Nyumbani Mbeya City wataivaa Timu isiyotabirika Stand United ya Shinyanga.
VPL inaongozwa na Azam FC wenye Pointi 33 kwa Mechi 17 wakifuata Yanga wenye Pointi 31 kwa Mechi 16 na Simba ni wa 3 wakiwa na Pointi 29 kwa Mechi 18.

Kikosi cha Yanga
RATIBA YA MECHI ZA LEO:
Jumatano Machi 18

Yanga v Kagera Sugar
Mgambo JKT v Simba
Mbeya City v Stand United

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: LEO JUMATANO HAPATOSHI!! BARCELONA vs MANCHESTER CITY HUKO NOU CAMP

Manchester City wana kibarua kigumu kusonga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa mara yao ya kwanza kabisa.
City Jumatano Usiku wapo Nou Camp kurudiana na Barcelona baada ya kuchapwa 2-1 na Barca wakiwa kwao Etihad Wiki 3 zilizopita katika Mechi ya kwanza.
Kwenye Mechi hiyo ambayo Barca walitawala, City wangekuwa na kazi ngumu zaidi kama si uhodari w Kipa wao Joe Hart kuokoa Penati ya Dakika za Majeruhi ya Lionel Messi.
Kwa hali za Timu hizi mbili hivi sasa, Barca wako vyema zaidi baada ya kupanda kileleni mwa La Liga kufuatia ushindi wao wa Mechi 16 kati ya 17 zilizopita.
Kwa City hali hivi sasa ni tete na Jumamosi walipigwa 1-0 na Timu ya mkiani Burnley na kuharibu matumaini yao ya kutetea Taji lao la Ubingwa wa England.
Hata hivyo, Meneja wa City anaetoka Chile, Manuel Pellegrini, amesisitiza bado wana matumaini ya kuibwaga Barca kwao.
Lakini hiyo si kazi rahisi hata kidogo ukichukulia fomu ya Barca hivi sasa na ukali wa Fowadi yao ya Mtu 3 ya Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez.
Kwenye Mechi hii Barca itamkosa Majeruhi Sergio Busquets na hivyo Jeremy Mathieu kucheza badala yake na hili litamfanya Javier Mascherano acheze kama Kiungo Mkabaji.
City itamkosa Fulbeki wake Gael Clichy ambae yupo Kifungoni baada ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika Mechi ya kwanza.



Arsenal iliichapa AS Monaco 2-0 kwao Stade Louis II Jijini Monaco ambako hawajafungwa tangu 2005 lakini wametupwa nje ya UEFA kwa Bao za Ugenini na hii ni mara ya 5 mfululizo kwa Arsenal kushindwa kutinga Robo Fainali.
Arsenal walifungwa kwao Emirates Bao 3-1 na matokeo ya usiku huu kufanya Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili kuwa 3-3 na AS Monaco kutinga Robo Fainali kwa Ubora wa Bao za Ugenini.
Hii ni mara ya kwanza kwa AS Monaco kufika Robo Fainali tangu 2004.
Dakika ya 79 kipindi cha pili Aaron Ramsey aliwapachikia bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya As Monaco.
Nje!Kocha Wenger akitoka Uwanjani baada ya kupokea matokeoGibbs akiwa kichwa chini!Mdebwedooo!Masikitiko Makubwa!!Kilio kwa Mesut Ozil!!Upande mwingine furaha ....harusi!!Kocha wa As Monaco akiwa aamini!!Mtajiju!! Tunasonga mbele sisi!!
Santi Cazorla akijionea Arsenal wakitupwa nje kwenye  Champions Ligi huko  Monaco usiku huu ambapo waliweza kuifunga bao 2-0 lakini bao la Ugenini kuibeba Monaco

Wachezji wa Monaco pamoja na Baadhid ya Viongozi wakishangilia baada ya kuiondosha Arsenal kwenye Uefa Champions League.
Yannick Ferreira Carrasco akishangilia baada ya mpira kumalizika

Olivier Giroud hoi

Mesut Ozil hivyo hivyo nae kachoka mbaya!!
Giroud aliwapa matumaini baada ya kufunga bao lakini mambo yakawa tofauti kwenye bao la Ugenini

waliotembelea blog