Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar
es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es
Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia
ni katibu wa Baraza la wazee wa Dar es Salaam Mzee Mtulia.
Rais Jakaya Kiwete akihutubia taifa hii leo katika ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam kupitia wazee wa jiji hilo.
Pampoja na mambo mbalimbali Rais Kikwete amezungumzia Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa uliofanyika nchini kote na kuunga mkono maamuzi ya
Waziri TAMISEMI, Hawa Ghasia juu ya maamuzi ya kuwatimua kazi,
kusimamisha, kuwashusha vyema na kuwapa maonyo ya madaraja mbalimbali
watendaji wote waliohusika na kuharibika kwa uchaguzi huo katika maeneo
yao.
Rais Kikwete hivi sasa anazungumzia sakata la ESCROW ambapo kwa mambo
kadhaa ambayo yalikuwa yakisubiri uamuzi wake ikiwa ni pamoja na
kuwaondoa mawaziri tajwa.
Rais Kikwete amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali tayari amejiuzulu,
Bodi ya Tanesco imeshamaliza muda wake na tayari amesha teua Mwenyekiti
Mpya wa Bodi huku Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof.
Anna Tibaijuka akisema amesha zungumza nae na amemuomba apishe nafasi
yake ateuliwe mtu mwingine.
Upande wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameomba
amuweke kiporo yeye na Katibu Mkuu wake, Eliakim Maswi kupisha uchunguzi
dhidi yao.
Baadhi
ya wazee na wananchi wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete wakati alipokuwa akilihutubia taifa kupitia wazee wa Dar es
Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo.
Wanahabari wakichukua kumbukumbu kwenye mkutano huo wa Mh.Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es
Salaam leo Desemba 22, 2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar
es Salaam.
Bofya Link hiyo kumsikiliza