Tuesday, July 9, 2013

MAKAMANDA WA CHADEMA WANAOKABILIWA NA KESI YA UGAIDI WAREJESHWA RUMANDE-TABORA 

Makamanda watano wa Chadema wakiingizwa ukumbi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoani Tabora kufuatia kesi ya Ugaidi inayowakabili akiwemo kaimu Katibu wa Chama hicho mkoa wa Dar-es-Salaam Bw.Henry Kileo aliyeshika Kitabu mkononi. 
Wanachama watano wa chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA wanaokabiliwa na mashitaka ya Ugaidi wamerejeshwa tena rumande pasipo maombi yao kusikilizwa hadi tarehe 22/07/2013 kesi hiyo itakapotajwa tena.
Akitoa uamuzi huo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Tabora Issa Magoli amesema kuwa kwa vile mahakama yake haina uwezo kisheria kusikiliza shauri hilo kesi hiyo inahairishwa hadi hapo upande wa utetezi wakiendelea na taratibu za kupeleka hoja zao Mahakama kuu.
Hakimu Magoli kabla ya kuahirisha shauri hilo aliwashauri mawakili wa upande wa utetezi wawasilishe hoja zao mahakama kuu ya Tanzania ndipo watakapoweza kupatiwa ufumbuzi wa kisheria.
Akizungumza nje ya Mahakama,Wakili wa washtakiwa hao,Peter Kibatala,alisema wanafanya utaratibu wa kupeleka shauri lao Mahakama Kuu baada ya kupewa nakala ya uamuzi uliotolewa na mahakama ya hakimu Mkazi Tabora.
Alisema katika maombi yao Mahakama kuu wataomba ipitie shauri hilo na pia kuona kama ni halali kisheria kwa washtakiwa hao kufunguliwa kesi hiyo baada ya awali washtakiwa wanne ukimuondoa Kilewo mashtaka yao kuondolewa na kasha kushtakiwa tena na Kilewo.
Wakili Kibatala mbali ya kusema ana imani na Mahakama lakini alieleza wana Imani zaidi na mahakama Kuu kwa vile alidai ipo huru
Alisisitiza kama mawakili wa washtakiwa wanapambana kuhakikisha haki inatendeka na kuwaomba wana ndugu na jamaa kuwa watulivu na wawategemee.
“Nawaomba ndugu na jamaa wa washtakiwa kuwa watulivu wakituacha mawakili wao tukipambana katika suala hili na tunawatia moyo msikate tama kwani kesi ni suala la mchakato na linaweza kuchukua muda mrefu”Alisema
Kwa upande wake Mke wa mshtakiwa Henry Kilewo,Joyce Kiria,alisema yeye alipoamua kuolewa na Kilewo alijua ni mwanaharakati lakini kwa vile anampenda alikubali kuolewa naye.
Alisema yupo naye katika kipindi hiki na bado anampenda na kuwatia moyo wanawake kuwa bega na waume zao pale wanapokuwa na matatizo.
“Nataka niwaambie kuwa hii sasa ndio wanawake live ni lazima wanawake tuwe wavumilivu katika kupambana na tusibaki kulia lia”Alisema.
Shauri hilo lilivutia umati wa wapenzi wa CHADEMA waliojitokeza kwa wingi huku ulinzi ukiwa mkali ambapo Askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia walitanda wakiwa na silaha.
Watuhumiwa hao watano akiwemo kaimu katibu wa Chadema Bw.Henry Kilewo,Evodius Justian,Oscar Kaijage,Seif Kabuta na Rajabu Kihawa wamerejeshwa rumande hadi hapo tarehe 22 Julai mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.|Na KapipiJHabari

 

 


Hii ndio picha ya kwanza ya Amber Rose na Wiz Khalifa baada ya kufunga ndoa.




Mastaa Amber Rose na rapper Wiz Khalifa wamefunga ndoa rasmi jana July 8 2013 na sasa ni Mr.  and Mrs. Thomaz ambapo muda mfupi baada ya ndoa Amber alitweet “Yay me and my baby are officially married!!!” na kuweka hiyo picha instagram iliyokua na maneno yanasema 







 

AGNESS MASOGANGE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA AFRIKA KUSINI

 HATIMAYE  wale Wanawake wawili walionaswa  na  madawa ya  kulevya  Afrika  kusini wametambuliwa kuwa  ni  mabinti  wa  KITANZANIA ..

Mabinti  hao  wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wetu  jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald (MASOGANGE)  ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita mtandao huu  ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.

Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.
 

Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.

Melezo Kwa hisani ya Nipashe.

 

 

 

NANDO NA FEZA KESSY WAENDELEA KUPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA NDANI YA BIG BROTHER......HAKUNA ALIYEINGIA KIKAANGONI 


 
Wiki hii Watanzania na mashabiki wa shindano la Big Brother Africa hawana haja ya kuwa wasiwasi ya kuwaokoa washiriki wao kwakuwa Nando na Feza Kessy wako safe. 


Kilichobaki ni kuvuta tu viti virefu na kuendelea na bata huku tukiwaangalia wengine wakihaha kuokoa washiriki wao.


Hata hivyo Evictions ya wiki hii inatarajiwa kuwa ya aina yake tangu show ianze hasa kwakuwa waliotajwa kuondoka ni washiriki ngangari.
 Ni nani kati ya Cleo, Natasha, Pokello, Selly, Melvin na Annabel anayeweza kubwaga manyanga kwenye mchezo huo wa ‘kufukuzana’? Afrika itaamua.

waliotembelea blog