Wednesday, October 8, 2014


RAIS wa Shirikisho la Soka la Italy, FIGC, Carlo Tavecchio, amefungiwa Miezi 6 na UEFA kwa matamshi yake ya Kibaguzi.
Tavecchio, mwenye Miaka 71, alitoa kauli ya Kibaguzi wakati wa Kampeni za Uchaguzi wake wa wadhifa huo Mwezi Julai alipotamka kuwa Wachezaji wa Kigeni ni ‘wala ndizi.’
Baadae Mheshimiwa huyo aliomba radhi.

Adhabu hii ya UEFA inamaanisha hawezi kushika wadhifa wowote wa UEFA na pia hataruhusiwa kuhudhuria Kongresi ya UEFA itakayofanyika Mwezi Machi 2015.
Mbali ya hayo, ‘Mbaguzi’ huyo haruhusiwi kutimiza wajibu wake kama Mwanakamati wa Kamati ya Vijana na Soka la Ridhaa ya UEFA na vile vile ameamrishwa na UEFA kuandaa programu maalum huko Italy ili kuleta mwamko wa kupinga Ubaguzi wa Rangi. Hata hivyo, wadhifa wa Tavecchio ndani ya FIGC hautaguswa baada ya Waendesha Mashtaka Nchini Italy kuamua kutomburuza Mahakamani kwa matamshi yake.

Tavecchio alichaguliwa Rais wa FIGC Mwezi Agosti baada ya kumshinda Mchezaji wa zamani wa AC Milan Demetrio Albertini lakini Mchezaji wa zamani wa Juventus na Nigeria, Sunday Oliseh, aliuelezea uchaguzi huo kama ‘Siku Mbaya kwa Soka!’

waliotembelea blog