Thursday, October 10, 2013


 Navy SEAL ni kikosi maalumu cha askari wa Marekani ambacho hutumwa kutekeleza oparesheni maalumu ikiwemo kuwakamata watuhumiwa maalumu wa kimataifa ambao wamekuwa wakitafutwa kwa muda mrefu. 
NAIROBI, Kenya
Imebainika kwamba mtu aliyekuwa akitafutwa na kikosi maalumu cha Navy SEAL mwishoni mwa wiki ni raia wa Kenya ambaye alipanga kuvamia ofisi za Bunge na ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa za kiusalama kutoka Serikali ya Kenya, kikosi hicho cha askari maalumu wa Marekani kilikuwa kikimtafuta mtu huyo usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, lakini walishindwa kumnasa baada ya kukutana na upinzani mkali kutoka kwa wapiganaji wa Al Shabaab.
Navy SEAL ni kikosi maalumu cha askari wa Marekani ambacho hutumwa kutekeleza oparesheni maalumu ikiwemo kuwakamata watuhumiwa maalumu wa kimataifa ambao wamekuwa wakitafutwa kwa muda mrefu.
Taarifa hiyo ilimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Abdulkadir Mohamed Abdulkadir ambaye pia hufahamika kwa jina la Ikrima, kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na AP.
Askari wa kikosi hicho maalumu waliripotiwa kushindwa kutimiza lengo la kumnasa mtuhumiwa huyo kama ilivyopangwa, kwa mujibu wa mmoja wa maofisa ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Kwa mujibu wa ripoti ya ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa la Kenya, Abdulkadir ni mtu anayetajwa kuwa kiongozi wa kupanga mashambulizi yote ya kigaidi akipata maelekezo kutoka kwa wakuu wa Al Qaeda huko Pakistan ambaye amekuwa akisimamia mashambulizi yote yaliyofanyika Kenya kati ya mwaka 2011 na mwanzoni mwa mwaka 2012.
AP ilieleza kwamba mashambulio kadhaa miongoni mwa hayo yaliyokuwa yamepangwa na Al Shabaab yaliweza kuvurugwa kabla hayajatekelezwa.
Taarifa hiyo iliyotolewa kwa shirika la habari la AP na mengine kadhaa ilikuwa ikieleza mikakati ya baada ya uvamisi wa jengo la kibiashara la Westgate Mall mjini Nairobi uliofanywa na wapiganaji wa Al-Shabaab Septemba 21 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 60, huku mwanamama raia wa Uingereza, Samantha Lewthwaite maarufu kama ‘White Widow’ akitajwa kuhusika.
Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba mwanamama huyo ni miongoni mwa waliokuwa wamepangwa kutekeleza uvamizi huo mpya wa ukumbi wa Bunge, ofisi za UN mjini Nairobi, Ofisi za makao makuu ya jeshi na maeneo mengine.
Pia wanadaiwa kupanga kutekeleza mauaji ya maofisa wa juu wa Serikali ya Kenya, wanasiasa na maofisa usalama.
Idara ya Usalama wa Taifa ya Kenya ilieleza katika taarifa yake ya awali kwamba kabla ya uvamizi wa Septemba 21, walipata taarifa za kuwepo kwa wanamgambo wa Al Shabaab mjini Nairobi na kwamba walipanga katika tarehe na siku isiyojulikana watavamia jengo hilo la Wastgate Mall na Kanisa Kuu la Holy Family Basilica.

Rais wa Cameroon Paul Biya amemsihi 
mshambulizi wa timu ya taifa ya soka 
Samuel Eto'o kutostaafu kucheza soka la Kimataifa.
Mshambulizi huyo wa Chelsea amekutana 
na wawakilishi wa rais Biya jijini Yaounde 
kujadiliana kuhusu hatima ya Eto'o ambaye tayari 
alikuwa ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa.
Baada ya kikao hicho Eto'o alikubali kuichezea tena Cameoon na sasa atasafiri Ufaransa kujiunga na kikosi cha Indomitable Lions kinachojiandaa kumenyana na Tunisia katika mchuano wa kufuzu kwa kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 baada ya mchuano wa makundi dhidi ya Libya aliwaambia wachezaji wenzake kuwa alikuwa amestaafu kucheza soka la Kimataifa.
Licha ya Eto kutoa tangazo hilo, kocha wa Cameroon Volker Finke alikuwa amemjumuisha katika kikosi chake cha mwisho.

Awali, Eto'o amekuwa na uhusiano mbaya na shirikisho la soka nchini Cameroon baada ya kuongoza mgomo wa wachezaji mwaka 2011 na kususia mchuano wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Algeria.
Hatua hiyo ilimsababishia kupewa adhabu ya kufungiwa mechi 15 na baadaye kupunguzwa hadi mechi nane baada ya kukata rufaa.
Licha ya adhabu yake kukamilikia Eto'o, alisusia kuichezea timu yake ya taifa kwa miezi kadhaa.

Mbali na Eto'o rais Biya pia aliwahi kumsihi mchezaji maarufu wa zamani Roger Milla kuicheza katika kombe la dunia mwaka 1990.

 Uongozi wa chuo cha ualimu -ERA kinachotarajiwa
 kufunguliwa januari mwakani,wameongea na wanafunzi 
wa shule ya sekondari bilele na kuwataka kuzingati mambo
 ya msingi wakati wakifanya mtihani wa mwisho kuhitimu
 kidato cha nne.(baadhi ya majengo ya chuo cha ualim
 Mwl  ocham .o. collins na mwl  Pauline ngina 
wakisaini  kitabu cha wageni shule ya bilele
 Mwl Tulla william (mwl wa taaluma) akiwakaribisha
 uongozi kutoka chuo cha ualimu ERA kuongea na wanafunzi.
                                                                   umakini..
                                                             wanafunzi wakisikiliza kwa makini
                                                            Bw mushobozi na mwl wa bilele
                                                            bw jeremiah mdau wa ERA
                                                                    wanafunzi wakisikiliza
 mwl ocham .o. collins  (kutoka sauti) akieleza
 maswala muhimu ya wanafunzi kuzingatia kabla ya mtihani wa mwisho
 Mwl Pauline ambae ni mkuu wa chuo  ERA 
mtarajiwa akiwaeleza wanafunzi mafunzo
 yatakayotolewa na chuo cha ERA,CHUO
 KITATOA MAFUNZO kozi ya ualimu daraja la 3A, Stashahada(diploma ya ualimu)
kwa miaka miwili, kituo cha kufanyia mitihani 
ya kujitegemea, Darasa la wanaorudia mitihani 
ya kidato cha nne (pc) kwa mwaka mmoja
                                 wanafunzi wakipata soda kama kiburudisho, wakati wakisikiliza
                                                          picha ya pamoja baada ya kufundwa
Bi Paskazia barongo mkurugenzi wa passy community service ltd na mkurugenzi mkuu wa chuo cha ERA,ambae yuko nchini sweden kwa maandalizi ya ufunguzi wa chuo mwakani.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), na kuzikubalia kampuni tano za simu nchini kujiunga katika kesi ya kupinga tozo ya kodi za simu ya Sh 1,000 kwa kila laini kwa mwezi. 
SOMA ZAIDI.......
Kampuni hizo zinaungana na Chama cha Kutetea Walaji kupinga utekelezaji wa kodi hizo uliotakiwa kuanza Julai mwaka huu, baada ya kupitishwa bungeni Juni mwaka huu.

Akitoa uamuzi wa jopo, Mwenyekiti wa Jopo la majaji, Jaji Aloysius Mujuluzi, alisema wamekubaliana na hoja zilizowasilishwa na wakili wa kampuni tano za simu, Fatuma Karume, kwamba hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani na wateja wake iko sahihi.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali akimwakilisha AG aliwasilisha pingamizi la awali kupinga maombi ya kampuni za simu kujiunga katika kesi akidai kwamba, hati ya kiapo ilikosewa kisheria kwani aliyeapa ni mmoja, Tumaini Shija wa Kampuni ya TTCL.

“Tunakubaliana na hoja za Karume kwamba hoja za kupinga maombi ya kampuni za simu kujiunga katika kesi hayana msingi, kwa sababu sheria ina ruhusu mtu kuapa kwa niaba ya wengine.

“Kampuni tano za simu, MIC Tanzania Limited, Vodacom, Airtel, ZANTEL na TTCL zimekubaliwa kuingia katika kesi, watakuwa mlalamikaji namba mbili mpaka sita, mlalamikaji namba moja ni Chama cha Kutetea Walaji,” alisema Jaji Mujuluzi.

Jaji Mujuluzi alisema walalamikaji hao baada ya kuungana watafanya marekebisho ya hati ya maombi yao, na Oktoba 15 mwaka huu wataiwasilisha mahakamani, Jamhuri itawasilisha majibu, kisha Oktoba 21 maombi ya kupinga tozo za simu yatasikilizwa.

Mdaiwa katika kesi hiyo ni Wizara ya Fedha na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Chama cha Walaji kiliwasilisha maombi mahakamani dhidi Wizara ya Fedha hivi karibuni wakipinga tozo hiyo kwa madai kwamba inawaumiza wateja wao.

Wakili Karume akiziwakilisha kampuni za simu, aliwasilisha maombi mahakamani wakitaka waruhisiwe kujiunga katika kesi hiyo na wamekubaliwa.

Majaji wanaosikiliza kesi hiyo ni majaji watatu, Aloysius Mujuluzi (Mwenyekiti wa jopo), Jaji Laurence Kaduli na Jaji Salvatory Bongole.

Walalamikaji hao sita wamewasilisha maombi mahakamani hapo wakipinga sheria mbalimbali zinazokiuka Katiba.

 
Wanadai wateja wao hawana uwezo wa kulipa kodi ya Sh 1000 kwa kila laini ya simu iliyopitishwa bungeni Juni mwaka huu, hivyo wanaitaka Mahakama kuzuia



RATIBA:
Jumamosi Oktoba 12
Kagera Sugar v Yanga
Simba v Tanzania Prisons


Jumapili Oktoba 13

Ashanti United v Coastal Union
Ruvu Shooting v Rhino Rangers
Mgambo JKT v Mbeya City
Azam FC v JKT Ruvu
Mtibwa Sugar v JKT Oljoro


MSIMAMO ULIVYO MPAKA SASA 2013-2014
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
GF
POINTI
1
Simba SC
7
4
3
0
11
16
15
2
Azam
8
3
5
0
6
11
14
3
Mbeya City
8
3
5
0
7
11
14
4
Coastal Union
7
3
4
0
2
6
13
5
Yanga SC
7
3
3
1
7
13
12
6
JKT Ruvu
8
3
2
3
7
9
12
7
Kagera Sugar
7
3
2
2
2
7
11
8
Ruvu Shooting
8
3
2
3
7
9
11
9
Mtibwa Sugar
8
2
4
2
-1
7
10
10
Prisons FC
8
3
2
3
-3
5
7
11
Rhino Rangers
7
1
4
2
-5
4
6
12
JKT Oljoro
7
1
2
4
-3
4
6
13
Mgambo JKT
7
1
2
4
-9
2
5
14
Ashanti United
7
0
2
5
-11
4
2


Mapema Asubuhi hii Ndege ya Precision Air ikiingia kwenye uwanja wa Ndege wa Bukoba, kuwaleta wachezaji wa Yanga ambao wanatarajia kucheza mchezo wao na Wenyeji Kagera Sugar kesho kutwa Jumamosi.
Wachezaji wa Yanga wakishuka, mbele ni Mbuyu Twite wakishuka uwanja wa Ndege Bukoba
Nizar Khalfani nae yupo kwenye kikosi
Wachezaji wakiendelea kushuka kwenye ndege
Tayari wamekanyaga Ardhi ya Bukoba
Kama kawaida: kushoto ni Khalfan Ngassa kulia ni Niyonzima
Picha ya Pamoja Viongozi na wachezaji
Dida kushoto akipata picha ya pamoja na wenzake
Kocha mkuu wa timu ya Yanga
Asante tumefika salama kazi ni moja ...ushindi ni muhimu KaitabaNiyonzima akiwa na Mdau wake wa bukobasports.com
Kelvin Yondani akifurahia baada ya kutua Bukoba asubuhi hii.

Bw. Jamal kalumuna kushoto akiwa na kiongozi wa Yanga
Smart Hotel
Wachezaji wakiingia Smart Hotel


EnglandDamiel Sturridge akifanya mazoezi na wenzake wa England tayari kujiwefa sawa kupambana na Montenegro michuano ya kwenda kucheza kombe la Dunia Brazil 2014.Three reasons why England WILL qualify for the World CupKocha mkuu wa England Roy Hodgson kwenye mazoezi akiangalia vijana wakeHappy days: Daniel Sturridge and Daniel Welbeck share a joke during the England training session at London Colney on Thursday
Daniel Sturridge na Daniel Welbeck wakiteta jambo na kufurrahia leo kwenye mazoezi kwenye uwanja wa Colney leo AlhamisThree reasons why England WILL qualify for the World Cup 
Wayne Rooney na Daniel Sturridge ajiwa kufanya maajabu kupeleka timu yao Brazil 
 l
Skipper: Steven Gerrard faces Phil Jones and Tom Cleverley, during a training session at London ColneySteven Gerrard, Phil Jones na Tom Cleverley, leo kwenye mazoezi yao huko London Colney
Having a laugh: Wayne Rooney shares a joke with midfielder James Milner and striker Jermain DefoeWayne Rooney na James Milner pamoja na striker Jermain Defoe wakiteta jambo na kucheka hapa..
Hitman: Rooney was in a relaxed mood at London Colney as England prepare for their World Cup qualifiersMchezaji wa Manchester United Rooney nae ni moja ya jembe linalotegemewa kwenye kikosi cha kuchuana kwenye mashindano hayo ya kugombea nafasi ya kucheza Kombe la dunia 2014 huko Brazil.
The boss: Roy Hodgson watches his England players train on Thursday morning at Arsenal's London Colney facilities
Kocha mkuu Roy Hodgson akiangalia wachezaji wake wanaokipiga katika timu ya Arsenal Under pressure: Joe Hart will be hoping for a solid performance in goal after criticism in some of his recent performances for Man City
Kipa Joe Hart wa Man City nae ni moja ya wachezaji wa England anayetarajiwa kucheza kikosi cha kwanza.
On your toes! Tom Cleverley, Jack Wilshere, Phil Jones and Chris Smalling work on their footworkTom Cleverley, Jack Wilshere, Phil Jones na Chris Smalling wakifanya mazoezi leo hii..
  nhjuy78

waliotembelea blog