Thursday, May 8, 2014


Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Timu ya Nigeria (Flying Eagles) imewasili nchini kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) itakayochezwa Jumapili (Mei 11 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Flying Eagles yenye msafara wa watu 32 imewasili leo (Mei 8 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya Ethiopian Airlines ambapo imefikia hoteli ya Sapphire. Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itafanyika kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nigeria inayofundishwa na kocha Manu Garba itafanya mazoezi leo (Mei 8 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi siku ya Jumapili.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa sehemu zote wakati upande wa VIP itakuwa ni sh. 5,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi katika magari maalumu.
Ngorongoro Heroes ambayo katika raundi ya kwanza iliitoa Kenya kwa jumla ya mabao 4-3 inaendelea kujinoa jijini Dar es Salaam chini ya Kocha wake John Simkoko na Msaidizi wake Mohamed Ayoub kujiweka sawa kwa mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na washabiki wa mpira wa miguu nchini.
Nigeria kama ilivyo kwa nchi nyingine 12 imeanzia moja kwa moja raundi ya pili kutokana na ratiba iliyopangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Nchi hizo ni Afrika Kusini, Angola, Benin, Burkina Faso, Cameroon, Gabon, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Mali, Misri, Morocco na Zambia.
PLUIJMKITAMBI


SAM_2259 Aliyekuwa Kocha mkuu wa Yanga sc, Hans Van Der Pluijm ( wa kwanza kulia) akiwa na wasaidizi wake, Boniface Mkwasa ( wa pili kulia) na Juma Pondamali ( wa tatu kulia)

KOCHA  mkuu wa Young Africans, Mholanzi, Hans Van der Pluijm amepata kazi mpya nchini Saudi Arabia na tayari ameshaaga rasmi mchana huu kwa wachezaji wake, viongozi, wapenzi na wanachama wa klabu hiyo.
Pluijm aliyejiunga na Yanga mapema januari mwaka huu umepata shavu hilo katika klabu ya Al Shoalah FC inayoshiriki ligi kuu soka nchini Saudi Arabia.
Mholanzi huyo amemaliza mkataba wake wa miezi sita na klabu ya Yanga, lakini mbaya zaidi ameshindwa kuwasaidia wanajangwani kutetea ubingwa wao msimu huu uliomalizika aprili 19 mwaka huu. 
Yanga chini ya Pluijm ilimaliza katika nafasi ya pili, huku Azam fc chini ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog wakibeba taji lao la kwanza tangu wapande ligi kuu msimu wa 2008/2009. 
Pluijm alirithi mikoba ya mholanzi mwenzake, Ernie Brandts aliyetimuliwa mwezi desemba mwaka jana baada ya kufungwa mabao 3-1 na Simba katika mechi ya Nani Mtani Jembe.
Brandts aliondoka pamoja na wasaidizi wake Fredy Felix Minziro na kocha wa makipa Mkenya Razak Ssiwa na nafasi zao kuchukuliwa  na Pluijm, Charles Boniface Mkwasa na Juma Pondamali `Mensah`.
Taarifa rasmi kutoka Yanga inaeleza kuwa Pluijm aliyeiongoza Yanga kwa miezi mitano imesema  kuwa Puijm ametoa shukurani zake kwa ushirikiano  mkubwa aliokuwa anapewa kwa kipindi chote alichokaa na Yanga.
Pluijm amekaririwa akisema: "Najua wengi itawashangaza kuona naondoka,  lakini ukweli ni kwamba nilikua na hii dili hata kabla ya kuja Yanga”.
“ Nilikuwa na makubaliano na timu ya Al Shoalah FC, ambayo yanaanza mwezi ujao, hivyo nilikubaliana na viongozi wa Yanga kuja kufanya kazi kwa kipindi cha miezi sita tu”.
“Nashukuru tumefanya kazi salama na baada ya mkataba huo kumalizika nipo tayari kurudi kuja kufanya kazi Tanzania" alisema Pluijm.
Aidha , Pluijm alieleza kuwa tayari ameshajaza fomu ya uanachama wa Yanga,  hivyo anajiona ni sehemu ya klabu hiyo yenye makazi yake makutano ya Twiga na Jangwani, Kariokoo,  jijini Dar es salaam.
Kocha huyo aliongeza kuwa yupo tayari kuisaidia Yanga kupata wachezaji wazuri watakaoisaidia klabu katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao na michuano ya kombe la shirikisho.
Pluijm anaondoka leo nchini kwenda Ghana kisha atakwea pipa kwenda nchini Saudi Arabia tayari kwa kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu nchini humo.
Mkataba wa Pluijm na klabu hiyo ya Saudia ni wa mwaka mmoja.
Tayari  kocha huyo ameshakabithi ripoti jana, kinachofuata ni viongzoi kuifanyia kazi na baadaye kuweka wazi nini mapendekezo yake.


All alone: One devastated Liverpool fan looks on after the Reds' 3-3 draw with Crystal Palace on Monday nightTears: It all got too much as the fan appeared to break down in tears after the Reds had been pegged backGutting: The same supporter later reflects on the game long after many fans had left Selhurst ParkShell-shocked: One Liverpool fan puts his hands to his face after Dwight Gayle equalised for Palace late onDisbelief: Liverpool had led the game 3-0 courtesy of goals from Joe Allen, Daniel Sturridge and Luis SuarezDon't look now: One Liverpool supporter covers his face with his hooded top following the 3-3 drawDevastated: Suarez just couldn't compose himself after what had been an unbelievable end to the gamePraying for a City defeat: One fan tries to comes to terms with the result after Liverpool had led 3-0Wanting the ground to eat him up: Suarez was disconsolate as he watched his back four capitulateHelping hand: Liverpool captain Steven Gerrard does his best to console Suarez after the full-time whistle


Paying the price: Carlo Ancelotti (top left), Claudio Ranieri (top right) and Avram Grant (bottom left) were all sacked after trophyless seasons while Jose Mourinho (bottom right) looks set to end this year without any silverware
Jose Mourinho anaweza kuwa kocha wa nne kumaliza msimu bila kombe kwa klabu ya Chelsea tokea Roman Abramovich aanze kuimiliki klabu hiyo. Alianza Claudio Ranieri kukosa kombe akafukuzwa kazi akifuatiwa na Carlo Ancelotti na Avram Grant. Hadi sasa klabu ya Chelsea imeshatolewa kwenye michuano yote ya ndani na nje ya England huku ikiwa nafasi ya tatu kwenye ligi kuu. Ni wazi kuwa Chelsea haitaweza kushinda kombe la ligi kuu na hivyo kumfanya Mourinho kumaliza msimu bila kombe lolote. Lakini hadi sasa hakuna fufunu zozote kuwa Mourinho atafukuzwa kazi kutokana na ugeni wake ndani ya klabu baada ya kurudi akitokea Madrid. Ukweli ni kwamba Mourinho ataendelea kuifundisha Chelsea kwa msimu mwingine zaidi ili kuirudisha klabu tena Chelsea kwenye kiwango chake kilichozoeleka. Tatizo kubwa la klabu ya Chelsea msimu huu lilikuwa ni safu ya ushambualiji na tayari Mourinho ameshaonesha nia ya kumsajili Diego Costa (Atl. Madrid) baada ya kushinda kumnasa Rooney.

486618_545707472135474_901587883_n
TAYARI mchakato wa uchaguzi katika klabu ya Simba sc umeshaanza  na tayari  mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Damas Ndumbaro ametangaza kuwa juni 29 mwaka huu uchaguzi utafanyika
Wapo watu wengi wanaotamani kuiongoza klabu ya Simba ambayo kwasasa ipo katika hali ngumu kwa soka la uwanjani.
Kumaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga na Azam fc ni jambo linalowaumiza wana Simba wote.
Ni msimu wa pili mfufulizo Simba wanakosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa. Kwa ukongwe wake ni jambo la fedheha kubwa japokuwa mpira uko hivyo.
Hatuwezi kuwakosoa Simba kwa matokeo waliyokuwa wanapata kwasababu mpira wa miguu huwa unabadilika, lakini makosa yanapotokea kwasababu ya watu fulani kutowajibika, hapo lazima ukosoaji uhusike.
Kwa mfano wachezaji kushindwa kucheza vizuri kwasababu hawajalipwa posho na mishahara, unashindwaje kuukosoa uongozi kwa kushindwa kuwajibika?
Kumekuwapo na mivutano ya muda mrefu baina ya mwenyekiti wa Simba, sasa Rais, Ismail Aden Rage na  baadhi ya wajumbe wake wa kamati ya utendaji pamoja na baadhi ya wanachama.
Sinema nyingi zimeonekana na zimeandikwa, kila mtu anafahamu yaliyokuwa yanatokea Simba sc




 DSC_4575
Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
MOJA ya kilio kikubwa cha watanzania ni kutaka kuona timu ya Taifa ya Tanzania,  Taifa stars inafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
Tangu iliposhiriki kwa mara mwisho fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria, Taifa Stars haijafanikiwa kupata nafasi kama hiyo.
Kuelekea fainali za mataifa ya Afrika, AFCON zitakazofanyika mwakani 2015 nchini Morocco, uongozi wa shirikisho la soka Tanzania TFF umeanza kampeni za kuisaidia Stars ifuzu kushiriki fainali hizo.
Kabla ya kuondoka kwake, kocha wa Taifa stars aliyevunjiwa mkataba mwaka huu, Kim Poulsen aliweka mikakati ya kuivusha Taifa stars kucheza fainali za AFCON mwakani.
Mara zote Kim alikuwa anasema ndoto zake zinaweza kutimia kwa kutumia wachezaji waliopo sasa Taifa stars na kutafuta wengine wapya wanaoshiriki michuano ya ligi kuu.
Moja ya mkakati wa Kim ilikuwa ni kutafuta wachezaji wengi zaidi na akalazimika kuwa na timu mbili za Taifa.
Moja ilibaki kuwa Taifa Stars iliyozoeleka, lakini akaongeza  nyingine ya `Young Future Taifa Stars`.
Timu hii ya `Young Future Taifa stars`  ilijumuisha wachezaji wanaotoka klabu za ligi kuu, lakini hawakuwa na nafasi timu ya Taifa.
Lengo la Kim lilikuwa ni kupata uwanja mpana wa kutafuta wachezaji wa kumsaidia kufuzu AFCON mwakani.
Hakika mpango huu uliungwa mkono na wadau wa soka na wengi wao walijenga hoja yao kuwa ungewashitua wachezaji waliopo Stars kuwa kuna wenzetu wapo nyuma yetu kama watazembea.
Chini ya Kim, Taifa stars ilibadilika kiuchezaji, japokuwa haikufanikiwa kufanya vizuri katika mashindano makubwa.
Lakini iliweza kuzifunga timu kama Morocco, Zambia, Gambia, Cameroon na kuonesha kiwango kizuri.
Baada ya mabadiliko ya uongozi ndani ya TFF, Rais mpya wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi alikuja na mipango yake.
malinzi
Rais wa TFF, Jamal Malinzi
Moja ya vitu alivyofanya siku za kwanza ni kubadili watu katika maeneo mengi ya uongozi wake.
Malinzi aliwaondoa watendaji wengi waliokuwa chini ya Rais aliyemaliza muda wake, Leodger Chila Tenga.
Rungu hili la mabadiliko lilimwangua  kocha wa Taifa stars, Kim Poulsen ambaye alivunjiwa mkataba kwa madai ya kushindwa kuifanikisha Taifa stars na amelewa Mholanzi, Mart Nooij.
Kilio kikubwa cha makocha wengi na wapenda soka nchini Tanzania ni kukosa mfumo mzuri wa soka la vijana.
Makocha wengi wanadai wachezaji wengi wa kitanzania wamekosa mambo ya msingi katika mpira kwasababu wengi wao wameanza kujifunza mpira ukubwani.
Kwa misingi hiyo, makocha wengi wanapendekeza nguvu kubwa kuwekezwa katika maendeleo ya soka la vijana.
Malinzi alikuja na mpango mzuri wa soka la Tanzania, na moja ya vitu vikubwa alivyoahidi kuwekea mkazo ni kuifanikisha Taifa stars kufuzu AFCON mwakani nchini Morocco.
Pia alisema anataka kujenga vituo kadhaa vya kukuza viapji vya vijana yaani akademi.
Lengo si kuandika ahadi zake, lakini makala hii inajaribu kuona mpango wa Malinzi na Taifa stars.
Rais huyo aliwashitua wengi baada ya kuja na mpango mpya wa maboresho ya Taifa stars.
Alitumia makocha wengi wa soka waliocheza soka zamani kujadili namna ya kuboresha Taifa stars.
Kwa pamoja, makocha hawa walikubaliana kuwa Tanzania kuna vipaji vingi  vilivyofichika, hivyo liundwe jopo la kuzunguka mikoani kutafuta vijana wa kuwaingiza Taifa stars.
Toka mwanzo, makocha wengi wa kisasa walikuwa na mashaka na mfumo huu, lakini TFF wakasisitiza utasaidia sana kuipeleka Stars AFCON.
Malinzi alisema watatafutwa vijana wengi na kuchujwa ili kupata wachache watakaojiunga na Stars. Na kweli zoezi likaanza na kupatikana vijana hao.
Wachezaji hawa wa maboresho ya Taifa stars waliwekwa kambini mjini Tukuyu na kwa mara ya kwanza waliletwa jijini Dar es salaam kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Burundi.
Staz
Taifa Stars ya maboresho iliyochapwa mabao 3-0 na Burundi aprili 26 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
 Mechi hii ilikuwa siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar aprili 26 mwaka huu, na hamu ya wapenzi wengi wa soka ilikuwa kuiona Stars ya maboresho iliyosifiwa na baadhi ya wadau walioshauriana na Malinzi.
Kama kawaida, vijana hawa walitandikwa mabao 3-0, na si kufungwa tu, hata mpira walichezewa.
Katika mechi hiyo walioonekana kucheza ni wale wanaocheza ligi kuu kama akina Saimon Msuva, Frank Domayo na wengine wachache, lakini vijana wa maboresho kila mtu aliona walichofanya.
Baada ya mechi hiyo, jambo jipya likalipuka ambapo TFF walikosolewa kwa mpango huu na nadhani wao pia waliona hakuna walichofanya.
Mechi dhidi ya Malawi kule Mbeya, Kocha mkuu, Mart Nooij aliwabwaga wachezaji wote wa maboresho ya Taifa stars na kuwadhihirishia TFF na makocha waliopanga mfumo huu na watanzania wote kuwa tumepoteza pesa bure.
Wadau wengi wamekuwa wakikosoa mfumo huu wa Malinzi na kupendekeza wakae tena na makocha wao kubuni njia mbadala ya kuisaidia Taifa stars.
Kila binadamu ana udhaifu wake, na kwa bahati mbaya Watanzania wengi huwa hatukubali kirahisi  kukosolewa.
Mnapokaa makocha 40 kujadili namna ya kuendeleza soka la nchi ndani ya chumba, mnaweza kukubaliana mfumo fulani utumike kama huu wa mabaoresho kwasababu tu mnafafana mawazo.
Lakini kuna jambo moja la msingi  sana hapa, sidhani kama makocha wote kwa moyo mmoja waliunga mkono mfumo huu. Naamini wapo walioona kabisa ni kupoteza muda, lakini walishindwa kushauri kwasababu zao .
Inawezekana walikuwa waoga kwasababu walikuwa nyuma ya mwamvuli wa watu fulani. Labda kuna watu yatari waliingia na majibu yao kwa maana ya mpango kupangwa na makocha kuitwa ili waubarik na kuanza kusaidia kuzunguka kuzunguka mikoani.
Lakini kama kweli walikuwa na nia ya dhati ya kuisaidia Stars ifuzu AFCON, hatudhani kama wangekuja na mpango huu wa maboresho.
Haya sasa, ukweli umeonekana, cha msingi ni TFF kukubali kukosea na kujipanga upya.
Kukosea jambo la kawaida, lakini kukabiliana na kosa ni jambo jema zaidi.
Nadhani TFF ni wasikivu na wanasikia kilio cha watanzania kuwa mfumo wa huu wa maboresho ya Taifa stars ni mzuri, lakini unahitaji muda na si mpango wa haraka.
Huwezi kutafuta wachezaji wa timu ya taifa mikoani zaidi ya timu hizi za ligi kuu.
Wachezaji ni hawa hawa akina Ngassa, Domayo, Bocco, Canavaro, Yondan, Nyoni, Singano, Msuva, Kiemba, Samatta, Ulimwengu na wengineo. Hawa wa maboresho si wakutupeleka AFCON mwakani.
Waongezwe wengine kutoka timu za ligi kuu au waliopo waandaliwe vizuri.
TFF mkipata nafasi ya kujadili tena na kutathimini mavuno ya mpango wa maboresha ya Taifa stars, fikirieni upya juu la wazo lenu ili mje na njia sahihi.
Ongezeni makocha wa kisasa waje na mipango mipya na msitumie historia kuwa fulani alitolewa mkoani akaja kuisaidia Taifa stars.
Maisha yamebadilika na soka la kisasa linahitaji utaalamu, lakini kwa haraka haraka kazaneni na mpango wa akademi, hapo nadhani kutakuwa na jambo zuri la kuzungumza.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha mpya, Mart Nooij tayari ipo jijini Mbeya kujiwinda kwa mechi hiyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa jijini Dar es Salaam kati ya Mei 16 na 18 mwaka huu.
Kukubali kosa si dhambi hata kidogo. Asubuhi njema kwako msomaji wetu.


Dakika ya 12 tu Jack Colback aliipachikia Sunderland bao, Bao la pili lilifungwa na Fabio Borini katika dakika ya 31 baada ya kupata mpira kutoka kwa Sebastian Larsson.
 Fabio Borini akitupia katika dakika ya 31 na kufanya 2-0 kabla ya kwenda mapumziko.
Kama kawaida kwa Fabio Borini akishangilia aina yake ile alipoipachikia bao la pili Sunderland.
VIKOSI:
Sunderland: Mannone, Vergini, O'Shea, Brown, Alonso, Cattermole, Johnson, Larsson, Colback, Borini, Wickham.
Subs: Bardsley, Altidore, Ba, Giaccherini, Bridcutt, Scocco, Ustari.

West Brom: Foster, Reid, Lugano, McAuley, Brunt, Anichebe, Yacob, Morrison, Dorrans, Sessegnon, Berahino. 

Subs: Olsson, Sinclair, Myhill, Vydra, Mulumbu, Dawson, O'Neil.
Referee: Lee Mason


Doubt: Ronaldo lies on the pitch after being tackled during Wednesday's must-win match
Real Madrid walilazimishwa Sare ya Bao 1-1 na Real Vallodolid na hilo ni pigo kwao kutwaa Ubingwa na pia kumpoteza Staa wao mkubwa Cristiano Ronaldo aliecheza Dakika 8 tu za kwanza na kupumzishwa baada kujisikia maumivu na nafasi yake kuchukuliwa na Chipukizi Alvaro Morata.
Hivi karibuni Ronaldo amekuwa akikabiliwa na tatizo la Musuli za Pajani ambalo lilimweka nje kwa Wiki 3.
Real sasa wako Pointi 4 nyuma ya Vinara Atletico Madrid na Mechi zimebaki 2 tu.Kipindi cha kwanza dakika ya 34 Sergio Ramos ndiye aliyeziona nyavu za Valladolid na kuwapatia bao la kwanza Real Madrid kwa kufanya 1-0 dhidi ya wenyeji Valladolid.Stunner: Real Madrid's Sergio Ramos celebrates scoring the opening goal against Real ValladolidRamos akishangilia bao lakeCrucial: Ramos celebrates his goal with Real Madrid coach Carlo Ancelotti
Dakika za lala salama, Dakika ya 85 Humberto Osorio aliyeingia akitokea benchi katika dakika ya 74 ndie aliyewamaliza kwa   kusawazishia bao kwa kufanya 1-1.
VIKOSI:
Valladolid: Jaime, Rukavina, Valiente, Mitrovic, Pena, Alvaro Rubio, Perez, Jeffen, Oscar, Bergdich, Guerra
Subs: Marino, Rueda, Baraja, Sastre, Omar, Larsson, Osorio
Real Madrid: Casillas, Pepe, Ramos, Coentrao, Ronaldo (Morata 9'), Benzema, Alonso, Nacho, Modric, Di Maria, Isco.
Subs: Diego Lopez, Khedira, Marcelo, Casemiro, Illarra, Llorente



Edin Dzeko akishangilia vikali baada ya kuifungia bao mbili City na kupanda kileleni usiku huu. Mtanange wao wa mwisho kuamua nani Bingwa kati yao na Liverpool, Huku Ushindi wa City wa bao 4-0 ukiwakalisha kileleni na pointi zao 83 na Liverpool wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 81.

Dzeko hapa aliwaunganisha wachezaji wa City kwa pamoja na kumpongeza.Edin Dzeko
Kipindi cha kwanza kilimalizika wote wakiwa 0-0. Kipindi cha pili dakika ya 64 Manchester City walifanya mashambulizi na hatimaye Edin Dzeko kuipachikia bao la kwanza kwa kufanya 1-0 dhidi ya Aston Villa baada ya Dzeko kupata krosi iliyowapita mabeki ikipigwa na Pablo Zabaleta.Pleading: Joe Hart reacts as his side move within inches of the Premier League title
Dakika ya 72 tena Edin Dzeko aliifungia bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Aston Villa. Bao la tatu lilifungwa na Stevan Jovetic akipewa pasi safi na Yaya Toure, Huku bao la Mwisho likifungwa na Yaya Touré katika dakika za majeruhi baada ya kuwachomoka wachezaji mabeki wa Aston Villa.Vincent Kompany
Yaya Toure alikokota Mpira toka Nusu yake ya Uwanja na kutembea nao  Mchezaji mmoja baada ya mwingine wa Villa na kupachika Bao la 100 la Ligi kwa City Msimu huu kitu ambacho hakijafanyika kwenye Ligi ya Juu England tangu Miaka ya 1950.Making his point: Paul Lambert shouts instructions to his side from his technical area
Nafasi pekee na safi waliyopata Villa ya kufunga ni pale Kichwa cha Weimann kugonga Posti ya Juu na kudunda chini nje ya Mstari wa Goli na kumwacha Mshambuliaji huyo asiamini nini kimetokea.
Ligi Kuu Engand inamalizika Jumapili kwa City kucheza Nyumbani na West Ham na wanahitaji Pointi 1 tu kutwaa Ubingwa labda Liverpool washinde, huku City wakitoka Sare, na kufuta Tofauti ya Mabao 13 ya City au City wafungwe Mechi hiyo na Liverpool kushinda.
Mechi ya Leo pia imefuta kabisa matumaini ya Chelsea kutwaa Ubingwa.
Can't even watch: Manuel Pellegrini can barely look with his side on the brink of a Premier League titleKocha wa City Manuel PellegriniAcrobatic: City captain Vincent Kompany attempts an audacious overhead kick
VIKOSI:
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov, Javi Garcia, Toure, Milner, Silva, Nasri, Dzeko. 

Subs: Richards, Lescott, Negredo, Clichy, Fernandinho, Pantilimon, Jovetic.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Clark, El Ahmadi, Westwood, Delph, Weimann, Bowery, Bertrand. 
Subs: Bacuna, Steer, Sylla, Tonev, Holt, Robinson, Grealish.


WACHEZAJI maarufu wa Klabu ya AC Milan ya Italy, Kaka na Robinho, sasa ni rasmi hawatacheza Timu ya Taifa ya Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza kuchezwa Nchini Brazil kuanzia Juni 12 hadi Julai 13 baada Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari', Leo kutangaza Kikosi chake cha awali cha Wachezaji 23.
Pamoja na hao wawili pia hawamo Mkongwe Ronaldinho na Winga wa PSG, Lucas Moura.
Wachezaji wanne wa Chelsea, David Luiz, Oscar, Ramires na Willian, wote wamo ila Viungo wawili wa Liverpool, Philippe Coutinho na Lucas Leiva, wamekosa namba, huku Paulinho wa Tottenham na Fernandinho wa Man City, wakiwemo kundini.
Brazil reveal World Cup squad as Kaka, Robinho and Lucas Moura miss out
Brazil, pamoja na Nchi nyingine zote zinazocheza Fainali, zinapaswa kusajili Vikosi vyao vya Wachezaji 23 kwa FIFA ifikapo Juni 2.
Brazil, ambao kwenye Fainali za Kombe la Dunia wapo KUNDI A pamoja na Croatia, Mexico na Cameroon, watacheza Mechi ya Kirafiki na Panama Juni 3 huko Golania, Brazil na kisha Juni 6 kuivaa Serbia huko Sao Paulo, Brazil.
Brazil watafungua rasmi Kombe la Dunia hapo Juni 12 kwa kuivaa Croatia katika Mechi ya KUNDI A.


KIKOSI KAMILI:
MAKIPA:
Julio Cesar (Toronto FC, Mkopo toka QPR), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico Mineiro).
MABEKI: Marcelo (Real Madrid), Daniel Alves (Barcelona), Maicon (AS Roma), Maxwell and Thiago Silva (both Paris St-Germain), David Luiz (Chelsea), Dante (Bayern Munich), Henrique (Napoli).
VIUNGO: Paulinho (Tottenham Hotspur), Ramires (Chelsea), Willian (Chelsea), Oscar (Chelsea), Hernanes (Inter Milan), Luiz Gustavo (Wolfsburg), Fernandinho (Manchester City).
MAFOWADI: Bernard (Shakhtar Donetsk), Neymar (Barcelona), Fred (Fluminense), Jo (Atletico Mineiro), Hulk (Zenit St Petersburg).


RATIBA:Mechi za Ufunguzi:
Alhamisi 12 Juni 2014
KUNDI A
23:00 Brazil vs Croatia
Ijumaa 13 Juni 2014
19:00 Mexico V Cameroon

waliotembelea blog