Edin Dzeko akishangilia vikali baada ya kuifungia bao mbili City na kupanda kileleni usiku huu. Mtanange wao wa mwisho kuamua nani Bingwa kati yao na Liverpool, Huku Ushindi wa City wa bao 4-0 ukiwakalisha kileleni na pointi zao 83 na Liverpool wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 81.
Dzeko hapa aliwaunganisha wachezaji wa City kwa pamoja na kumpongeza.
Kipindi cha kwanza kilimalizika wote wakiwa 0-0. Kipindi cha pili dakika ya 64 Manchester City walifanya mashambulizi na hatimaye Edin Dzeko kuipachikia bao la kwanza kwa kufanya 1-0 dhidi ya Aston Villa baada ya Dzeko kupata krosi iliyowapita mabeki ikipigwa na Pablo Zabaleta.
Yaya Toure alikokota Mpira toka Nusu yake ya Uwanja na kutembea nao Mchezaji mmoja baada ya mwingine wa Villa na kupachika Bao la 100 la Ligi kwa City Msimu huu kitu ambacho hakijafanyika kwenye Ligi ya Juu England tangu Miaka ya 1950.
Nafasi pekee na safi waliyopata Villa ya kufunga ni pale Kichwa cha Weimann kugonga Posti ya Juu na kudunda chini nje ya Mstari wa Goli na kumwacha Mshambuliaji huyo asiamini nini kimetokea.
Ligi Kuu Engand inamalizika Jumapili kwa City kucheza Nyumbani na West Ham na wanahitaji Pointi 1 tu kutwaa Ubingwa labda Liverpool washinde, huku City wakitoka Sare, na kufuta Tofauti ya Mabao 13 ya City au City wafungwe Mechi hiyo na Liverpool kushinda.
Mechi ya Leo pia imefuta kabisa matumaini ya Chelsea kutwaa Ubingwa.Kocha wa City Manuel Pellegrini
VIKOSI:
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov, Javi Garcia, Toure, Milner, Silva, Nasri, Dzeko.
Subs: Richards, Lescott, Negredo, Clichy, Fernandinho, Pantilimon, Jovetic.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Clark, El Ahmadi, Westwood, Delph, Weimann, Bowery, Bertrand.
Subs: Bacuna, Steer, Sylla, Tonev, Holt, Robinson, Grealish.
0 maoni:
Post a Comment