Monday, December 29, 2014


Mshambuliaji wa Chelsea na Spain Fernando Torres atajiunga moja kwa moja na AC Milan hapo Januari 5.
Torres, mwenye Miaka 30, alijiunga na AC Milan ya Italy kwa Mkopo tangu Mwezi Agosti lakini sasa Mkataba utabadilishwa na kujiunga kwa kudumu na Klabu hiyo ya Serie A.

Torres alijiunga na Chelsea kutoka Liverpool Januari 2011 katika Uhamisho ulioweka Rekodi ya Uingereza wakati huo wa Dau la Pauni Milioni 50.

Akiwa na Chelsea, Torres alifanikiwa kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI, EUROPA LIGI na FA CUP.
Kwenye Taarifa yao, Chelsea wamemshukuru Torres kwa utumishi wake kwao wa Miaka Minne na kumtakia kila la kheri katika maisha yake ya baadae.

 Ac Milan yajipanga kumchukua moja kwa moja

Torres alishaichezea Atletico Madrid dhidi ya  Barcelona kipindi cha nyuma mwaka  2006.
Lakini, habari za ndani zinadai Torres hatakaa AC Milan bali atapelekwa kwa Mkopo huko Spain kwenye Klabu yake ya zamani Atletico Madrid katika Dili ya kumbadili yeye na Straika wa Atletico Madrid Alessio Cerci ambae atatua AC Milan.
Dili hiyo itamfanya Torres aende Atletico kwa Mkopo wa Miezi 18 na Cerci, ambae ni Winga wa zamani wa Torino, atue AC Milan kwa Mkopo wa Miezi 6.
Tangu atue AC Milan, Torres amefunga Bao 1 tu kwenye Ligi Serie A katika Mechi 10 na hivi sasa ametupwa nje ya Kikosi cha Kwanza wakati Cerci nae hana namba huko Atletico.
Hivi sasa Ligi ya Serie A imesimama kwa mapumziko ya Krismasi na Mwaka mpya na itarejea hapo Januari 5.

Torres pia alishaichezea Liverpool kabla ya kwenda Chelsea kwa  £50million mwezi  January 2011

waliotembelea blog