Friday, November 13, 2015



Kuelekea michuano ya mataifa ya Ulaya yatakayofanyika mwaka 2016, shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza mpira maalum kwa ajili ya kutumika katika mashindano hayo, mpira wa utaotumika katika mashindano hayo ya mataifa ya Ulaya kwa mwaka 2016 umetengenezwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya kijerumani ADIDAS.
2E5E9C7500000578-0-image-a-42_1447327190930
Mpira huo maalum wa Euro unaoitwa kwa jina la kifaransa la ‘Beau Jeu’ ambapo kwa kiingereza unatafsiriwa kwa jina la ‘the beautiful game’ unatajwa kufanana na mpira (Brazuca) uliotumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 iliyofanyika Brazil . Mpira wa ‘Beau Jeu’ ulitengenezwa kwa zaidi ya miezi 18.
Michuano ya Euro 2016 itafafanyika Ufaransa lakini ADIDAS imekuwa ikipokea tenda ya kutengeneza mipira ya mashindano hayo kwa miaka mingi sasa.
download (2)
Hii ni List ya mipira ya Euro iliyokuwa inatumika kuanzia mwaka 1960 hadi utakaotumika mwaka 2016
1E7EDE1B00000578-3315271-image-a-53_1447328424468
Huu ni mpira wa Brazuca ambo ulitumika mwaka 2014 katika michuano ya Kombe la Dunia Brazil ila unatajwa kufanana na wa Euro 2016


Wakati mwingine katika maisha unaweza pata matatizo ya kiafya na baadhi ya wataalam wanaweza kusema kuwa unaumwa hiki lakini ukawa ni uchunguzi batili. November 12 beki wa kimataifa wa Ufaransa aliyewahi kuichezea Man United ya Uingereza kwa miaka 7 Patrice Evra amegundua chakula kilichokuwa kina mdhuru wakati yupo Man United.
Patrice_Evra_20120611
Evra alikuwa akila mayai kila siku licha ya kuwa alikuwa hajui kama anaaleji nayo kitu ambacho kilimpelekea kila siku kutapika mazoezini wakati yupo Man United, aliwahi kwenda hospitali wakati yupo Uingereza lakini aliambiwa kuwa ana tatizo la vidonda vya tumbo kitu ambacho sio kweli na tatizo lake limepatiwa majibu akiwa Juventus ya Italia.
“Nilipo jiunga na Juventus ndio waliniambia kuwa nina allergic na mayai ila nilikuwa nakula kila siku wakati nikiwa Man United nilikuwa nikitapika mazoezini lakini nilipoenda hospitali wakaniambia ninacheza soka huku nikiwa na vidonda vya tumbo sema nilikuwa na bahati kwa sababu vilikuwa havipo katika hali mbaya” >>> Evra
_86648597_evra
Patrice Evra ambaye ana umri wa miaka 34 alijiunga na Juventus ya Italia mwaka 2014 katika dirisha la usajili la majira ya joto na amecheza jumla ya mechi 47 toka ajiunge na Mabingwa hao wa Italia.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo anaripotiwa kutumia mkwanja mrefu kununua ndege binafsi, Staa huyo anayeongoza katika list ya rekodi ya watu maarufu wanaongoza kupata likes nyingi katika mtandao wa facebook amenunua ndege binafsi aina ya Gulfstream G200 Business Jet.
CTmoKwwUkAALhqc
Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 anatajwa kununua ndege hiyo kwa thamani ya pound milioni 13.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 44 za kibongo kwa ajili ya kuzunguuka sehemu mbalimbali duniani kuhusiana na mipango yake ya kujitanua kibiashara, ndege ya staa huyo inatajwa kuwa na uwezo wa kubeba watu 8 hadi 10, jiko la umeme, bafu, friji, makabati, simu na internet.
CTmoLGsUwAAD05O
Staa huyo ambaye anaonekana kujiimarisha zaidi kibiashara tayari amezindua movie ya maisha yake halisi aliyoizindua hivi karibuni Uingereza ila mwaka 2015 alitajwa kuzindua perfume, brand ya viatu vyake.
CTmoLjrU8AA1tuN
Sports-people-and-Private-jets
Cristiano Ronaldo akiwasili uwanja wa ndege wa Centrair International airport uliyopo Nagoya Japan kwa ndege yake binafsi.
GettyImages-79579622-742x505

waliotembelea blog