Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.
Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, Mkoani Iringa kwa maziko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.
Mke wa baba wa TAIFA Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho.
Mwshimiwa Spika wa Bunge Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana heshima za mwisho.
Mweshimiwa wa CHADEMA Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho.
Mawaziriki wakiwa wanaenda kutoa heshima za mwisho
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa
Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria shughuli hiyo ya kuuwaga mwili wa marehemu