Sunday, January 5, 2014



Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Mengele ‘Nyerere’ akizungumza mara baada ya kuchagulia kushika wadhifa huo wa uenyekiti,Steve alisema kuwa atahakikisha haki inatendeka kwa kila msanii wa filamu,kuhakikisha kipato kinaongezeka katika tasnia yao,kama vile haitoshi alieleza kuwa atakutana wasambazaji wote wa filamu kuzungumza mikakati mbalimali ya kuhakikisha tasnia hiyo wasanii wake wananufaika na kazi zao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.Steve anashika nafasi hiyo ya Uenyekiti iliokuwa imeachwa wazi na Msanii Vincent Kigosi a.k.a Ray.
“Tatizo kubwa kwa wasanii wa Bongo Movie hawajitambui kama wao ni watu wakubwa. Wanajiuza kirahisi kwa wasambazaji wakati karibu kila nyumba ya Mtanzania haukosi filamu moja ya Bongo Movie,” Aliongeza Nyerere ambaye pia anafahamika kwa jina la ‘Kata simu’.
“Wasanii wa Bongo Movie tunadhulumiwa kwa sababu hatutambui haki zetu. Leo wasanii watatu wanakwenda Mwanza wanapewa shilingi milioni mbili, Diamond peke yake
anapewa shilingi milioni 15,”alisema Nyerere



  
 


Ray akifafanua jambo 




Baadhi ya Wasanii wa Bongo.
  



 
 
 
Baadhi ya Wasanii wa Bongo

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog