Saturday, April 18, 2015

MSIMAMO ULIVYO KWA SASA: CHELSEA KILELENI.
English Premier League
#
Team
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Chelsea
31
22
7
2
64
26
38
73
2
Arsenal
32
20
6
6
63
32
31
66
3
Man United
32
19
8
5
59
30
29
65
4
Man City
32
18
7
7
65
34
31
61
5
Liverpool
32
17
6
9
47
36
11
57
6
Southampton
32
17
5
10
44
22
22
56
7
Tottenham
32
16
6
10
50
46
4
54
8
Swansea City
32
13
8
11
38
40
-2
47
9
West Ham
32
11
10
11
42
40
2
43
10
Stoke City
32
12
7
13
36
40
-4
43
11
Crystal Palace
32
11
9
12
42
43
-1
42
12
Everton
32
9
11
12
40
43
-3
38
13
Newcastle
32
9
8
15
33
51
-18
35
14
West Brom
32
8
9
15
30
46
-16
33
15
Aston Villa
33
8
8
17
24
45
-21
32
16
Sunderland
32
5
14
13
25
48
-23
29
17
Hull City
32
6
10
16
29
45
-16
28
18
QPR
33
7
5
21
38
59
-21
26
19
Burnley FC
32
5
11
16
26
50
-24
26
20
Leicester City
31
6
7
18
32
51
-19
25



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Msangi.

MSHITUKO wa matukio ya mfululizo ya ajali, umeendelea kugubika nchi, baada ya watu 20 kupoteza maisha katika ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace, iliyotokea jana wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Ajali hiyo ambayo taarifa na picha zake zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, imesababisha taharuki kutokana na ukaribu wake na matukio mengine ya ajali yaliyotokea wiki hii.


Baadhi ya wakazi wa jirani na eneola tukio wakitazama gari lilivyopata ajali kando kando ya mto Kiwira.

Tangu Jumapili iliyopita mpaka jana, siku zisizozidi sita kumetokea ajali kubwa tatu zilizohusisha mabasi ya abiria na kuteketeza maisha ya watu 40.

Mbali na ajali hizo, wiki hii Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alitoa takwimu zilizosababisha huzuni kwa Watanzania, kwamba kati ya Januari mosi na Aprili 12 sawa na siku 102, watu 969 walipoteza maisha katika ajali za barabarani.

Wananchi wa Kiwira wakiangalia baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Ajali za wiki
Jumatano wiki hii, basi la Air Jordan lililokuwa likitokea mkoani Mwanza kwenda Arusha, lilipata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 20.

Ajali hiyo ilitokea wakati Watanzania wakiwa na kumbukumbu ya ajali iliyotokea Jumapili ya wiki jana, ambapo watu 19 waliteketea kwa moto, baada ya basi la Kampuni ya Nganga Express na lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la Iyovi, Milima ya Udzungwa, mkoani Morogoro.

Ajali ya Mbeya
Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Msangi, alisema ajali hiyo mpya imetokea katika eneo la Ilongo ambalo limebatizwa jina la Uwanja wa Ndege karibu na Kiwira, ambapo watu 18 walipoteza maisha papo hapo.

“Watu wanne waliojeruhiwa, mmoja alikuwa katika hali mbaya na kwa bahati mbaya alifia njiani wakati akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa matibabu,” alisema Kamanda Msangi.
Kamanda Msangi alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na dereva kutokuwa makini katika uendeshaji wake. Taarifa zilizotufikia baadae, zilieleza kuwa abiria mwingine aliyekuwa akipatiwa matibabu, alifariki akiwa hospitalini.

Mashuhuda
Mashuhuda wa ajali hiyo walidai kuwa chanzo cha ajali ni mwendokasi uliosababisha dereva ashindwe kumudu gari hilo katika mteremko wenye kona, akajikuta gari likimshinda na kutumbukia katika Mto Kiwira.
Walidai kuna uwezekano dereva huyo alikuwa akikimbizwa na baadhi ya madereva wa mabasi aina ya Toyota Coaster, yanayofanya safari zake kati ya Mbeya, Tukuyu na Kyela.


Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.

Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo.

Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga


Wajumbe wa Imetosha
Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.


Wachezaji wa Coastal Union wakipata darasa kutoka kwa Kiongozi (Meneja) wa Klabu hiyo ya Tanga Jamhuri Kihwelo wakati wa Mazoezi yao.

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo
‘Julio’ amewaambia wachezaji wake wanatakiwa kufanya kila linaliwezekana kuhakikishaw anashinda mechi yao inayofuata.
Coastal Union itakipiga dhidi ya Polisi Moro ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Julio amewaambia wachezaji wake mara tu baada ya kumaliza mazoezi kwamba ni lazima washinde na hawatakuwa na sababu ya kujitetea.
“Hatuna cha kusema kama sababu ya kupoteza, kikosi chetuni imara na ushirikiano tunaopata ni mkubwa. Hivyo tupambane na kuibuka na ushindi.

waliotembelea blog