Jina Joseph Kimwaga sio geni katika soka la Tanzania hususani katika vilabu vya Azam FC na Simba, Kimwaga alianza kusikika katika soka akiwa katika klabu ya Azam FC kabla ya dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015 kuomba kwenda katika klabu ya Simba kwa mkopo wa muda mrefu.
Kimwaga
ambaye ana umri wa miaka 19 ni miongoni mwa mastaa chipukizi wa mchezo
wa soka wanaofanya vizuri kwa sasa, stori za ushirikina katika soka zipo
na zimewahi kumfikia Joseph Kimwaga
ila yeye huwa anaamini katika dini yake ya kikristo na kuvaa rozari,
licha ya kuwa rozari hukatazwa mchezaji kuvaa wakati wa mechi Kimwaga huwa anaifunga katika bukta yake ili refa asijue kwa imani yake anaamini inamlinda.
Staa huyo ambaye amewahi kuingia katika headlines baada ya kufunga goli la ushindi kwa klabu yake ya Azam FC dhidi ya Yanga amepewa rozari hiyo iliyotoka kwa Papa kutoka Italia na padri wake, ndio aliompatia hivyo kwa sababu imebarikiwa na Papa sio rahisi kwa vitu vya imani za giza kumpata Kimwaga.
“Kuna
majaribu ambayo yanatokea katika soka kiukweli ila kama una roho fupi
unaweza ukaacha lakini ni vitu ambavyo mimi na imani kwa sababu
nikikumbuka tu msemo mmoja nilioambiwa na paroko kuwa ukiingia tu katika
imani ndio majaribu yatakavyozidi kwa hiyo mimi na imani na ndio maana
navaa rozari muda wote” >>> Joseph Kimwaga