Thursday, January 7, 2016



Bado saa zinasogea na kila mpenda soka macho na akili yake kaelekeza Abuja Nigeria kusubiri nini kitatokea, Mbwana Samatta atafanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anayecheza Ligi ya ndani? lakinia vipi kwa upande wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa jumla nani atatwaa Pierre Emerick, Yaya Toure? Andrew Ayew? Naomba nikusogezee vitu 7 ambavyo huenda hufahamu kuhusu tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla ambapo wachezaji wanaowania hii ni Yaya Toure, Andrew Ayew na Pierre-Emerick Aubameyang .
1- Emanuel Amuneke ambaye ni winga wa zamani wa Nigeria ndio mchezaji pekee aliyekuwa anacheza ndani ya Afrika aliwahi kutwaa tuzo hiyo. Amuneke aliwahi kutwaa tuzo hiyo mwaka 1994 akiwa na klabu ya Zamalek ya Misri. Hii ndio list ya washindi wa tuzo hiyo kuanzia mwaka 1994 – 2014
1994 Emmauel Amuneke (Zamalek/Misri)
1995 – George Weah (PSG/AC Milan)
1996 – Nwankwo Kanu (Ajax/Inter Milan)
1997 – Victor Ikpeba (AS Monaco)
1998 РMustapha Hadji (Deportivo La Coru̱a)
1999 – Nwankwo Kanu (Arsenal)
2000 – Patrick Mboma (Parma/Cagliari)
2001 – El Hadji Diouf (RC Lens)
2002 – El Hadji Diouf (RC Lens/Liverpool)
2003 – Samuel Eto’o (Marlloca)
2004 – Samuel Eto’o (Marlloca/Barcelona)
2005 – Samuel Eto’o (Barcelona)
2006 – Didier Drogba (Chelsea)
2007 РFr̩d̩ric Kanout̩ (Sevilla)
2008 – Emmanuel Adebayor (Arsenal)
2009 – Didier Drogba (Chelsea)
2010 – Samuel Eto’o (Inter Milan)
2011 – Yaya Toure (Manchester City)
2012 – Yaya Toure (Manchester City)
2013 – Yaya Toure (Manchester City)
2014 – Yaya Toure (Manchester City)
2015 –  ………………………. ?
wpid-twitter-3-600x398
2- Cameroon ndio nchi iliowahi kutoa wachezaji wengi na kushinda tuzo hiyo. Hadi sasa kuna wachezaji sita wa Cameroon ambao wamewahi kushinda tuzo hiyo mara 11. Roger Milla (1976,1990), Thomas Nkono (1979,1982), Jean-Manga Onguene (1980), Theophile Abega (1984), Patrick Mboma (2000) na Samuel Eto’o (2003, 2004, 2005, 2010).
3 – Licha ya kufanikiwa kutwaa Kombe la mataifa ya Afrika mara saba, Misri imewahi kutoa mshindi wa tuzo hiyo mara moja pekee. Mahmoud Al-Khatib ndio mchezaji pekee wa Misri aliyewahi kutwaa tuzo ya mwaka 1983.
4 – Katika historia ya tuzo hizo, takwimu zinaonesha nchi za Afrika Magharibi ndio zinaongoza kutwaa tuzo hiyo. Baadhi ya nchi hizo ni Nigeria, Ghana, Guinea, Mali, Liberia, Togo na Ivory Coast wakifuatiwa na nchi za Afrika Kaskazini Algeria, Misri, Morocco na Tunisia.
23
Hawa ndio wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla
5 – Hizi ni nchi 5 ambazo zimewahi kutwaa tuzo hiyo lakini hazijwahi kushinda taji la mataifa ya Afrika Guinea (Cherif Souleymane, 1972); Togo (Emmanuel Adebayor, 2008); Liberia (George Weah, 1989, 1995); Senegal (El Hadji Diouf, 2001, 2002); na Mali (Salif Keita, 1970 na Frederic Kanoute, 2007).
6- Morocco ndio nchi inayoongoza kwa kutwaa tuzo hiyo mara nyingi zaidi kwa nchi za Afrika Kaskazini. Morocco imewahi kushnda Kombe ka mataifa ya Afrika mwaka 1976 . Mchezaji wa kwanza wa Morocco kushinda tuzo hiyo alikuwa  Ahmed Faras 1975, Mohamed Timoumi 1985, Badou Zaki 1986 na Mustapha Hadji 1998 alitangazwa kuwa mshindi.
MMWEEEE
Hawa ndio wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani
7 – Yaya Toure ndio mchezaji aliyetwaa tuzo hiyo mara nne mfululizo, baada ya kuchukua mwaka mwaka 2011 hadi mwaka 2014 lakini kwa mwaka 2015 bado anawania tuzo hiyo na Andrew Ayew na Pierre-Emerick Aubemayang. January 7 ndio siku ya utolewaji wa tuzo hizo zitakazofanyika Abuja Nigeria.

waliotembelea blog