Friday, August 29, 2014
1:41 AM
Unknown
UEFA Leo imempa Tuzo yao ya Mchezaji Bora wa Mwaka Cristiano Ronaldo baada ya kuwabwaga kwenye Kura Kipa wa Mabingwa wa Dunia Germany, Manuel Neuer na Mchezaji mwenzake wa Klabu ya Bayern Munich anaechezea Holland, Arjen Robben.
Ronaldo, Miaka 29, alifunga Bao 17 katika Mechi 11 za Ulaya wakati Real Madrid inaelekea kutwaa Taji lao la 10 la Ulaya walipobeba Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI na pia kuisaidia Klabu yake kutwaa Copa del Rey Msimu uliopita huko Spain.
Baada ya kukabidhiwa Tuzo yake, Ronaldo alisema: “Nimefurahi kweli kweli. Lazima niwashukuru Wachezaji wenzangu, Familia yangu, Marafiki zangu. Sina Kombe hili kwenye Makumbusho yangu, nitaliweka!”
Awali Majina ya Wachezaji 35 yalipigiwa Kura na kubakia 10 na kutangazwa hapo Julai 18 na kisha kubakishwa Matatu ambayo hii Leo ndio Mshindi kapatikana.
Wapigaji Kura ya Tuzo hii ni Jopo la Wanahabari maalum toka Nchi zote Wanachama wa UEFA.
Tuzo hii ilianzisha na UEFA Mwaka 2011 ili kuziba pengo la Ballon d'Or ambayo iliunganishwa na Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na pia kuibadili ile Tuzo ya zamani ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Klabu.
WASHINDI WALIOPITA:
2010–11 Lionel Messi [Barcelona]
2011–12 Andrés Iniesta [Barcelona]
2012–13 Franck Ribéry [Bayern Munich]
1:37 AM
Unknown
DROO
ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI imefanyika leo hii usiku huko Monaco na
Timu 4 za England, Manchester City, Liverpool, Chelsea,na Arsenal zimepata timu za kucheza nazo.
Taswira huko MonacoRonaldo Mchezaji Bora 2014 Ulaya.Ronaldo akibusu tuzo yake yake baada ya kuchaguliwa mchezaji boraRonaldo amewabwaga chini wachezaji wa Bayern Munich kipa Manuel Neuer na Arjen RobbenMchezaji wa zaani wa Real madrid captain Fernando Hierro akionesha karatasi ya kuonesha City Kundi E kundi ambalo linaonekana gumu.
Kipa wa Spain Iker Casillas alionesha Chelsea kwenye kundi G
Droo ya UEFA Champions League ni kama ifuatavyo:-
DROO YA MAKUNDI - UEFA CHAMPIONS
Kundi A: Atletico Madrid, Juventus, Olympiakos, Malmo
Kundi B: Real Madrid, Basel, Liverpool, Ludogorets Razgrad
Kundi C: Benfica, Zenit St Petersburg, Bayer Leverkusen, Monaco
Kundi D: Arsenal, Borussia Dortmund, Galatasaray, Anderlecht
Kundi E: Bayern Munich, Manchester City, CSKA Moscow, Roma
Kundi F: Barcelona, Paris St-Germain, Ajax, APOEL Nicosia
Kundi G: Chelsea, Schalke, Sporting Lisbon, Maribor
Kundi H: Porto, Shakhtar Donetsk, Athletic Bilbao, BATE Borisov
1:37 AM
Unknown
KEPTENI wa Manchester United Wayne Rooney ndie ameteuliwa Nahodha mpya wa England na Meneja wa Timu Roy Hodgson.
Rooney, mwenye Miaka 28, anachukua wadhifa huo kutoka kwa Steven Gerrard wa Liverpool ambae amestaafu kuichezea England mara baada ya Nchi hiyo kutolewa hatua ya Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia Mwezi Juni huko Brazil.
Rooney ameichezea England mara 95 na kufunga Bao 40 na Mwezi uliopita aliteuliwa kuwa Nahodha wa Manchester United na Meneja Louis van Gaal.
Mechi za kwanza kwa Rooney kama Nahodha wa England hapo Septemba 3 wakati England itacheza Mechi ya Kirafiki na Norway Uwanjani Wembley na kisha Septemba 8 kusafiri kwenda kucheza na Uswisi katika Mechi yao ya kwanza ya EURO 2016.
Mara baada ya kuteuliwa Rooney, Meneja Roy Hodgson alitangaza Kikosi chake cha England chenye Wachezaji wapya Wanne.
Wapya hao nI beki wa Arsenal mwenye Miaka 19, Calum Chambers, Mchezaji wa Newcastle Jack Colback, Danny Rose wa Tottenham na Fabian Delph wa Aston Villa, wote wakiwa na Umri wa Miaka 24.
KIKOSI CHA ENGLAND:
Makipa: Fraser Forster (Southampton), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City)
Mabeki: Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Calum Chambers (Arsenal), Phil Jagielka (Everton), Phil Jones (Manchester United), Danny Rose (Tottenham Hotspur), John Stones (Everton)
Viungo: Jack Colback (Newcastle United), Fabian Delph (Aston Villa), Jordan Henderson (Liverpool), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal) Raheem Sterling (Liverpool), Andros Townsend (Tottenham Hotspur), Jack Wilshere (Arsenal)
Mafowadi: Rickie Lambert (Liverpool), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United)

1:32 AM
Unknown
Emanuel Okwi wa Uganda ambaye msimu uliopita alikuwa anaichezea Yanga,
akiwa na jezi namba 25 aliyokabidhiwa mara baada ya kusaini tena Simba
baada ya kukachwa na Yanga katika usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara inayotarajia kuanza mwezi ujao.
Yametimia, hatimaye Emmanuel Okwi amerejea katika kikosi chake cha zamani cha Simba.
Okwi rasmi anasaini leo kujiunga na Simba baada ya kuelewana na uongozi wa klabu hiyo.
Mganda huyo amechukua uamuzi wa kusaini kuichezea Simba baada ya Yanga kumtema.
Okwi rasmi anasaini leo kujiunga na Simba baada ya kuelewana na uongozi wa klabu hiyo.
Mganda huyo amechukua uamuzi wa kusaini kuichezea Simba baada ya Yanga kumtema.
Subscribe to:
Posts (Atom)