UEFA Leo imempa Tuzo yao ya Mchezaji Bora wa Mwaka Cristiano Ronaldo baada ya kuwabwaga kwenye Kura Kipa wa Mabingwa wa Dunia Germany, Manuel Neuer na Mchezaji mwenzake wa Klabu ya Bayern Munich anaechezea Holland, Arjen Robben.
Ronaldo, Miaka 29, alifunga Bao 17 katika Mechi 11 za Ulaya wakati Real Madrid inaelekea kutwaa Taji lao la 10 la Ulaya walipobeba Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI na pia kuisaidia Klabu yake kutwaa Copa del Rey Msimu uliopita huko Spain.
Baada ya kukabidhiwa Tuzo yake, Ronaldo alisema: “Nimefurahi kweli kweli. Lazima niwashukuru Wachezaji wenzangu, Familia yangu, Marafiki zangu. Sina Kombe hili kwenye Makumbusho yangu, nitaliweka!”
Awali Majina ya Wachezaji 35 yalipigiwa Kura na kubakia 10 na kutangazwa hapo Julai 18 na kisha kubakishwa Matatu ambayo hii Leo ndio Mshindi kapatikana.
Wapigaji Kura ya Tuzo hii ni Jopo la Wanahabari maalum toka Nchi zote Wanachama wa UEFA.
Tuzo hii ilianzisha na UEFA Mwaka 2011 ili kuziba pengo la Ballon d'Or ambayo iliunganishwa na Tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora Duniani na pia kuibadili ile Tuzo ya zamani ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Klabu.
WASHINDI WALIOPITA:
2010–11 Lionel Messi [Barcelona]
2011–12 Andrés Iniesta [Barcelona]
2012–13 Franck Ribéry [Bayern Munich]
0 maoni:
Post a Comment