Njia za kumfanya mpenzi asitoke nje 1. TAMBUA THAMANI YAKE |
Unapokuwa Umeapa Kuwa Utampenda Mwenzako Hadi Kifo Kitakapowatenganisha, Uwe
Umefanya Hivyo Kwenye Nyumba Ya Ibada Au Kwingine, Lazima Ufahamu Jinsi Ya Kutambua
Juhudi Za Mpenzi Au Mwenzi Wako, Ili Kuepukana Na Uwezekano Wa Mwenzi Wako Kukuona
Kama Vile Unamchukulia Kawaida Na Hujali Jitihada Zake. Mtu Anapodhani Mwenzake
Hajali Jitihada Zake Ni Rahisi Kushawishika Kutoka Na Kwenda Kwa Mtu Atakayeitambua
Thamani Yake.
Ili Kuondoa Uwezekano Wa Mwenzako Kudhani Humjali Wala Kuthamini Juhudi Zake, Mara
Kwa Mara Jiulize Unaweza Kumfanyia Nini Ili Kumwonesha Kuwa Unamtambua. Jambo
Lenyewe La Kumfanyia Linaweza Kuwa Rahisi Tu, Mathalani Kumtumia Ujumbe Mfupi Kwa
Ajili Tu Ya Kumwambia Kuwa Yuko Mawazoni Mwako. Iwapo Utajenga Mazingira Ya
Kuitambua Thamani Ya Mwenzako Mara Kwa Mara Haitakuwa Rahisi Kwa Mwenzako Huyo
Kufikiria Kuchepuka.
2. JENGA UKARIBU NAYE
Mara Nyingi Jamii Huwachukulia Wanaume Kama Watumwa Wa Ashiki Zao, Lakini Matukio
Mengi Ya Kukosekana Kwa Uaminifu Hutokana Zaidi Na Mahusiano Ya Kikaribu Baina Ya
Mwanamke Na Mwanamume Na Si Tamaa Ya Mwili Ya Mwanamume. Iwapo Wanawake Wote
Wataufahamu Ukweli Huu, Watajua Jinsi Ya Kujenga Ukaribu Na Wanaume Zao Ili
Kuwaondolea Uwezekano Wa Kutekwa Na Wanawake Wengine.
Ni Kweli Kuwa Wapo Wanaume Wasioweza Kujenga Mshikamano Wa Kihisia Katika Suala La
Mapenzi, Lakini Huku Bado Wakiendelea Kuvutika Kimwili. Jambo Kubwa Ambalo Mwanamke
Anaweza Kulifanya Na Kumwepusha Mwanamume Kutoka Ni Kuhakikisha Ndiye Mtu Wake Wa
Karibu, Huku Mara Kwa Mara Akiwa Ndiye Mwanzilishi Wa Wazo La Kufanya Mapenzi.
3. MSIKILIZE VEMA MWENZAKO
Wanawake/Wasichana Huwa Na Mazoea Ya Kusemezana Na Marafiki Zao Mambo Mengi Ikiwa Ni
Pamoja Na Siri. Hata Hivyo, Wanaume Huogopa Kuwashirikisha Wenzao Mambo Binafsi Ya
Ndani. Ili Uweze Kuishi Vema Na Mwanamume, Lazima Ujue Jinsi Ya Kumhakikishia
Mwanamume Kuendelea Kuwa Mwanamume Hata Unapomweleza Mambo Yaamshayo Mihemko.
Kwako Wewe Mwanamke, Iwapo Utahisi Kuwa Mwanamume Wako Anataka Kuwa Wazi Katika
Mambo Fulani Binafsi Lakini Anahisi Tu Kuwa Atapoteza Uanaume Wake Kwa Kueleza Mambo
Yake, Mwekee Mazingira Ya Kumhakikishia Kuwa Ataendelea Kuwa Mwanamume. Msikilize Na
Usimlaumu, Muulize Maswali Yanayohitaji Majibu Chanya. Utashangaa Jinsi
Utakavyoboresha Ukaribu Wako Na Mwanamume Huyu Hivyo Kupunguza Uwezekano Wa
Kukusaliti.
4. MWACHE AWE NA MARAFIKI
Jambo Jingine Ambalo Linaweza Kumpunguzia Mwanamume Uwezekano Wa Kufanya Mapenzi Nje
Ya Uhusiano Ni Kumhakikishia Urafiki Na Wanaume Wenzake. Kwa Vyovyote Vile, Lazima
Mwanamume Wako Utakuwa Ulimkuta Na Marafiki. Usimzuie Kuendelea Kuwa Nao.
Unapomuunga Mkono Mwanamume Katika Kampani Yake Na Wanaume Wenzake Utakuwa
Umemwongezea Mwanamume Huyu Fursa Ya Kuendeleza Ukaribu Na Watu Wake, Hivyo
Kupunguza Fursa Ya Kujipenyeza Kwa Wanawake Wengine Katika Maisha Yake. Ukimbanabana
Halafu Na Wewe Ukashindwa Kuwa Rafiki Kwake, Akimpata Mwanamke Aliye Tayari
Atashikamana Naye.
5. TEKELEZA MALENGO NAYE
Hata Kama Uhusiano Wako Na Mpenzi Wako Umedumu Tangu Mlipokuwa Vijana Wadogo Chuoni,
Bado Haitoshi Kujihakikishia Kuwa Mmeshakua Pamoja. Ili Kuweza Kuepukana Na
Uwezekano Wa Mwenzako Kukusaliti, Lazima Nyote Msaidiane Katika Kutekeleza Mambo
Muhimu. Huku Ndiko Kukua Pamoja.
Njia Rahisi Zaidi Ya Kukua Pamoja Na Mpenzi Wako Au Mwenzi Wako Wa Maisha Ni Kuweka
Malengo Na Kuyatekeleza Kwa Pamoja. Mfano, Kama Mmeishi Katika Nyumba Ile Ile Kwa
Miaka Kadhaa Na Mazingira Yamewachosha (Pengine Nyumba Yenyewe Ni Ya Kupanga),
Pendekeza Kuhamia Sehemu Nyingine — Unaweza Kukuta Hata Mwenzako Kumbe Ana Hisia
Kama Hizo. Iwapo Utazigusa Hisia Zake Kwa Pendekezo Lako, Mpenzi Wako Atajihisi
Kuonekana Wa Tofauti Machoni Pako. Na Kwa Kuwa Baadhi Ya Watu Wanaotoka Nje Ya Ndoa
Huenda Kutafuta Utofauti, Utakuwa Umemzuia.
6. JITAHIDI KUMWELEWA
Mojawapo Ya Vishawishi Vikuu Vya Mwanamume Kujiingiza Katika Mapenzi Ni Kumpata Mtu
Ambaye Atamwelewa. Kama Huna Sifa Hii, Ni Rahisi Kwa Mwanamume Wako Kutoka Kwa Ajili
Ya Kuitafuta Kwingine.
Ili Kumzuia Mwanamume Kutoka, Onesha Jitihada Za Kutaka Kumwelewa Na Kufahamu
Matakwa Yake Ili Uweze Kuyatimiza. Katika Hili Usiogope Kumuuliza Maswali Magumu,
Mathalani Waweza Kumuuliza “Unajisikiaje Kuhusiana Na Uhusiano Wetu?” Au “Ni Kitu
Gani Ulichokuwa Unakitaka Katika Uhusiano/Ndoa Ambacho Hujakipata Mpaka Sasa?” Namna
Hii Utakuwa Umeonesha Jitihada Za Kutaka Kumfahamu Na Kumridhisha.
7. SISITIZA ZAIDI MATENDO
Wanawake Wana Utamaduni Wa Kupenda Kuyazungumza Mambo Yao, Ikiwa Ni Pamoja Na
Matatizo. Hili Ni Jambo Jema, Isipokuwa Tu Kinachotakiwa Ni Kuweka Uwiano Kati Ya
Maneno Na Matendo.
Mwanamke Hapaswi Kujiondoa Katika Hulka Yake Asilia Ya Kupenda Kusema Ili Aweze
Kudumisha Uhusiano Wake Na Mwanamume, Lakini Mara Kwa Mara Ni Vema Badala Ya Kusema
Tu Ukafanya Shughuli Kama Mbadala Wa Kusema. Badala Ya Kusema Sana, Unaweza
Kumshirikisha Mwanamume Katika Shughuli Fulani Ambayo Nyote Mnaipenda, Jambo Ambalo
Litaonesha Umoja Wenu, Huku Kila Mmoja Akipata Jibu Kwa Nini Alichagua Kuishi Na
Mwenzake.
Mathalani, Badala Ya Kuzungumzia Jinsi Usivyojisikia Vema Kwa Namna Msivyopata Muda
Mwingi Wa Kuwa Pamoja Na Kuzungumza, Tumia Fursa Hiyo Kuzungumza Kile Ambacho
Umekuwa Ukitaka Kuzungumza Na Mpenzi Wako, Maana Sasa Yupo. Badala Ya Kuzungumzia
Jinsi Unavyopenda Kujifunza Mapishi Fulani, Chukua Hatua Ya Kwenda Kujifunza, Na
Ikibidi Uende Na Mwenzako. Namna Hii Utaonekana Zaidi Kama Mtu Ambaye Unatenda
Maneno Yako, Si Kuzungumza Tu. Kwa Jinsi Hii Mpenzi Wako Atavutika Kwako Zaidi.
8. USIMWONDOLEE UJINSIA WAKE
Watu Wengi Katika Makuzi Yao Huwa Na Dhana Kuhusiana Na Jinsi Mwanamume Au Mwanamke
Anavyopaswa Kuwa. Kwa Mwanamume, Wengi Huamini Kuwa Atakuwa Mtendaji Kuliko Msemaji,
Asiyetawaliwa Na Mihemko, Mtawala, Jasiri, Hodari Na Kadhalika. Lakini Katika
Kipindi Cha Takriban Miongo Mitano Iliyopita, Hadhi Na Hulka Za Wanaume Na Wanawake
Zimebadilika. Isipokuwa, Bado Wanaume Halisi Wameendelea Kuwa Wanaume, Kama Ambavyo
Wanawake Halisi Wameendelea Kuwa Wanawake.
Iwapo Utakuwa Na Mazoea Ya Kumlazimisha Mwanamume Wako Kufanya Mambo Ambayo Si Ya
Kianaume, Au Ambayo Hayadhanii Kuwa Ya Kianaume, Mwanamume Huyu Anaweza Kulazimika
Kwenda Kumtafuta Mwanamke Ambaye Anampa Fursa Ya Kuendelea Kuwa Mwanamume.
Ili Kuondoa Uwezekano Wa Mwanamume Kutafuta Mahala Ambapo Uanaume Wake Utatambuliwa,
Jaribu Kufikiria Mambo Ambayo Humfanya Mwanamume Kujihisi Kuwa Mwanamume Kweli.
Namna Hiyo Utaongeza Mapenzi Yake Kwako.
9. PUNGUZA TAHADHARI
Mojawapo Ya Mambo Ambayo Huzuia Mahusiano Kufikia Ukamilifu Wake Ni Watu Kuishi Kwa
Tahadhari Wakiogopa Kuingia Katika Maeneo Ambayo Yanaweza Kuondoa Furaha Yao,
Pengine Kwa Mmoja Wa Wenza Hao Kukwazika. Ni Kweli Kuna Umuhimu Wa Kuepuka Kumkwaza
Mwenzako, Lakini Mnapoishi Kwa Tahadhari Kubwa Ni Vigumu Kufikia Ukamilifu Wa
Uhusiano Wenu Na Ni Rahisi Kwa Mwenza Kutoka Kwa Ajili Ya Kupata Uhuru Na Amani
Zaidi.
Ili Kuepusha Balaa, Jiulize Ni Wapi Wewe Na Mwenzako Hamkubaliani. Ukishayapata
Mambo Ambayo Hamkubaliani, Jaribu Kuweka Uwiano Na Kumpa Uhuru Mwenzako Katika
Kuyafanya Hayo. Namna Hii Utaongeza Ukamilifu Katika Uhusiano Wenu Na Hisia Za
Kubanwa Zitaondoka.
10. JISHUGHULISHE AKUKOSE
Wanawake Hupenda Zaidi Vitu Ambavyo Ni Haba Au Hupatikana Kwa Nadra. Katika Uhusiano
Wa Kimapenzi Mwanamke Hatakwambia Kuwa Anataka Uondoke Ili Aweze Kupata Fursa Ya
Kukumisi Na Kutamani Kukuona, Lakini Ukweli Ni Kwamba Ukipatikana Kwa Nadra
Utaongeza Mvuto Wako Kwake, Ilimradi Tu Uwe Na Sababu Ya Kupatikana Kwa Nadra.
Lazima Ujue Jinsi Ya Kumfanya Mpenzi Wako Akuhitaji. Jishughulishe Na Uchakarike,
Kwani Kwa Kufanya Hivyo Utaongeza Kipato Chako Na Kumwongezea Usalama Na Uhakika
Mpenzi Wako, Lakini Pia Utampa Mpenzi Wako Fursa Ya Kukumisi Na Kupunguza Uwezekano
Wa Kukusaliti.
MSHIKE MWENZIO
Huwezi Kumzuia Mpenzi Wako Kutoka Na Wanaume/Wanawake Wengine Kwa Kuwa Na Wivu Na
Kumfuatiliafuatilia. Lakini Kwa Kuzingatia Mambo Haya Yaliyobainishwa Hapa, Utakuwa
Umeondoa Sababu Nyingi Za Mpenzi Wako Kufikiria Kuwa Na Uhusiano Na Mtu Wa Nje.