Tuesday, August 18, 2015



Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Mega Trade Edmundi Rutaraka, akimkabidhi hundi ya Ts 1.5 Milioni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,Mussa Juma kwa ajili ya tamasha la 10 waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Manyara na Dar es salam na wadau wa habari ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa sheikh Amri Abeid, hafla hiyo ilifanyika jana, Palace Hoteli Jijini.habari na libeneke la kaskazini blog
Tamasha la 10 la vyombo vya habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa Juma, alisema tayari maandalizi muhimu yamekamilika.
Juma alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa, litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.

"tunapenda kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu inawezekana"alisema
Alisema katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha.

Nahodha wa timu ya TASWA Arusha, Ramadhani Siwayombe akikabidhiwa jezi kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha ambalo litafanyika Augosti 29 Sheikh Amri Abeid, anayemkabidhi ni Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay hafla hiyo, ilifanyika Palace hotel

Wakizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Masoko wa kampuni ya Mega Trade Edmund Rutaraka, Meneja masoko wa kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma na Meneja wa Faidika Arusha,Eliya Mlay walisema wamedhamini Tamasha hilo ili kuendeleza michezo.

waliotembelea blog