Friday, November 6, 2015


Klabu ya Chelsea ya Uingereza Jumamosi ya November 7 itasafiri kuifuata Klabu ya Stoke City kucheza mchezo wake wa wa Ligi Kuu Uingereza bila kuwa na kocha wao Jose Mourinho ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja sambamba na faini ya pound 40,000/= kwa kosa alilolifanya la kutoa lugha chafu kwa waamuzi wa mechi ya Chelsea dhidi ya West Ham United.
Jose Mourinho ambaye anajulikana kwa tabia yake ya kupenda timu yake ipate matokeo mazuri wakati wote, wengi walitegemea kuona akikata rufaa ya adhabu hiyo licha ya kuwa hakufanya hivyo na sio kawaida yake kukubali kushindwa mapema. November 7 Mourinho amejibu sababu za yeye kutokata rufaa ya adhabu hiyo, ni kweli amekubali alikosea au?
Jose-Mourinho-617546
“Mechi ni kesho na najua majibu ya rufaa kama ningekuwa nimekata, hivyo niliamua kukata tamaa na maamuzi hayo, nafikiri ni ujinga kupambana pambano ambalo tayari unaamini ulishashindwa” >>> Jose Mourinho

waliotembelea blog