Monday, October 14, 2013


UFOO SARO MWANDISHI WA ITV

Alfajiri  ya  jana, mtangazaji  wa  ITV   anayejulikana  kwa  jina  la  Ufoo Saro  amejeruhiwa  vibaya  kwa  kupigwa  risasi  na  mchumba  wake ambaye baada ya tukio hilo naye alijipiga risasi na kujiua.

Akizungumza na mnyetishaji wetu,  kamanda Wambura  ambaye  nikamanda  wa polisi wa  mkoa wa kipolisi wa kinondoni  amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya jana.
 
Kamanda wambura amedai  kuwa mwanaume  aliyetenda  mauaji  hayo ni  mchumba  wake  na  alikuwa anafanya  kazi  katika umoja wa mataifa ( UN ) huko sudani ila bado haijafahamika  kitengo alichokuwa  akifanyia  kazi.

Kwa  mujibu  wa  Kamanda Wambura, inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) ili  awasuluhishe

Baada  ya  usuluhishi  kuanza  na  kuonekana  kuwa  tatizo  liko  kwa  mwanaume, mwanaume huyo alimshutumu mama mkwe wake kwamba amekuwa  na  mazoea  ya  kumtetea mwanae   na  ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro risasi ya kichwa na kumuua papo hapo....

Alipomuua  mama  huyo, mwanaume huyo  alimpiga Ufoo Saro risasi mbili , moja ya tumboni na nyingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo

MATUKIO KATIKA PICHA:

 Ufoo Saro baada ya kufanyiwa upasuaji huo.

 Muuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akimpeleka wodini Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufo Saro,  baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa risasi kufuatia kushambuliwa kwa silaha ya moto nyumbani kwa mama yake  Kibamba jijini Dar es Salaam leo na   mchumba wake ambaye pia alimuua mama yake na kisha kujiua.

 Wanahabari wakimpiga picha Ufoo Saro baada ya kuondolewa chumba cha upasuaji.

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsindikiza Ufoo Saro wakati akipelekwa wodini.

waliotembelea blog