Friday, October 31, 2014



Wachezaji wa timu za Boom FC na Vijana ya Ilala wakisalimiana kabla ya mchezo wao wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup 2014 uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.

Kikosi cha timu ya Vijana ya Ilala kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Boom FC katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha timu ya Boom FC kikiwa katika picha ya pamoja.

Mashabiki wa timu ya Boom FC, wakipiga ngoma wakati timu yao ikicheza na Vijana ya Ilala.

Nahodha wa timu ya Vijana Ilala (kushoto) akisalimiana na mwenzake wa Boom FC, kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.

Mshambuliaji wa timu ya Vijana Ilala, Matola Selemani, kushoto akiwania mpira na winga wa timu ya Boom FC, Nambongo Hussein katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.

Mshambuliaji wa timu ya Boom FC,Issac Tesha (katikati) akijaribu kufunga bao katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup

Winga wa timu ya Boom FC, akiwatoka mabeki wa timu ya Vijana ya Ilala katika mchezo wa Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.

Beki wa timu ya Vijana Ilala Ramadhani Yasini, (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa timu ya Boom Ally Kondo, katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup.

Baadhi ya wadau wa Soka wakifuatilia mechi kati ya Tabata FC na Sifa Politan kwenye Uwanja wa Bandari.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Sifa Politan, Mathayo Edward (kulia) akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa timu ya Tabata FC, katika Ligi ya Dk. Mwaka Sports Extra Ndondo Cup mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Bandari Dar es Salaam. Tabata ilishinda kwa Penati 4-3.

Mashabiki wa timu ya Sifa Politan wakishangilia timu yao.

Thursday, October 30, 2014


Kikosi cha Young Africans kimewasili jana mjini Kahama ambapo kitaweka kambi ya siku ya tatu kabla ya kuelekea mjini Bukoba kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara siku ya jumamosi dhidi ya wenyeji timu ya Kagera Sugar.
Young Africans ikiwa mjini Kahama itacheza mchezo wa kirafiki siku ya jumatano dhidi ya wenyeji timu ya Ambassador FC ikiwa ni sehem ya maandalizi ya kocha kuelekea mchezo wa wakata miwa wa mkoa Kagera.
Kocha Marcio Maximo leo asubuhi amekiongoza kikosi chake kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa mjini hapa ikiwa ni maandalizi ya mechi ya mwishoni mwa wiki dhidi ya Kagera Sugar baada ya kupata pointi tatu katika mchezo dhidi ya Stand United.

Sunday, October 26, 2014

Kocha wa Liverpool, Rogers baada ya Balotelli kubadilishana jezi Meneja wa Liverpool Brendan Rogers amesema atachukua hatua dhidi ya Baloteli baada ya Balotelli kubadilishana jezi na Pepe mchezajiwa Real Madrid muda wa mapumziko Jumatano katika mchezo wa klabu bungwa Ulaya ambapo liverpool ilifungwa 3-0 na mabingwa watetezi wa kombe hilo uwanja wa Anfield.
Rogers alisema “ kama unataka kufanya hivyo fanya mwisho wa mchezo. Nikitu ambacho nitakifanyia kazi alhamisi(leo)” Mario Balotelli dakika 45 za kwanza dhidi ya real Madrid alipiga mashuti mawili lakini yote yalizuiwa na walinzi wa Madrid huku akionekana kupiga pasi chache zaidi ya wachezaji wote (17) sawa na Lazar Markovic ambaye alicheza kwa dakika 23 tu.
Rogaers ambaye aligharifika baada ya msimu uliopita kushuhudia mlinzi wake Mamadou Sakho akibadilishana jezi na Samuel Etoo kwenye mchezo wao dhidi ya Chelsea  alisema: “ tulikuwa na hali hii mwaka jana na tuli ishughulikia ndani ya club”
Rogers , amemkosoa Mtaliano huyo baada ya Liverpool kucheza chini ya kiwango dhidi ya mabingwa hao wa Ulaya ambao walijipatia goli la kwanza kupitia kwa Cristiano Ronaldo ambaye alifunga goli la 70 katika michuano hiyo na mengine yakifungwa na Karim Benzema.
Balotelli alitolewa na nafasi yake ilichukuliwa na Adam Lallana baada ya mapumziko.


VIKOSI:
Manchester United XI: 
De Gea, Rafael, Smalling, Rojo, Shaw, Blind, Fellaini, Januzaj, Di Maria, Mata, van Persie.
Chelsea XI
Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Felipe Luis, Fabregas, Matic, Willian, Oscar, Hazard, Drogba
Chelsea kuendelea kutema cheche tena leo?Diego Costa wenda akacheza kipindi cha pili!Radamel Falcao aliumia wenda hasicheze mtanange huu


Sammy Ameobi akishangilia bao lake la kusawazisha.1-1. Ayoze Pérez 
Newcastle United wametoka nyuma ya bao 1-0 na kuwapita Spurs kwa bao 2-1 katika kipindi cha pili. Bao la kusawazisha lilifungwa kipindi cha pili mapema dakika ya 46 kupitia kwa
Sammy Ameobi na bao la kuongoza lilifungwa na Ayoze Pérez katika dakika ya 58.

Emmanuel Adebayor aliwafungulia mlango Everton katika dakika ya 18 na kufanya 1-0 dhidi ya Newcastle.Emmanuel Adebayor alivyotupia bao lake kipindi cha kwanza.

Wednesday, October 22, 2014

3-0!!Wachezaji wa Real wakimpongeza mwenzao Karim Benzema baada ya kufunga bao la tatu kipindi cha kwanza cha dakika 45.Cristiano Ronaldo akishangilia bao lake la kwanza...
Bao la tatu lilifungwa na Karim Benzema tena baada ya kupigwa kona na Pepe kujitwisha kichwa kwenye eneo hatari ndani ya box na hatimae Karim Benzema kuupata na kuusindikiza langoni mwa Liverpool na kumfunga kipa Mignolet na kufanya 3-0 katika dakika ya 41.Karim Benzema akiruka juu na kufunga bao la pili.Cristiano Ronaldo akikatiza mbele..Cristiano Ronaldo aliipachikia bao la kwanza kipindi cha kkwanza dakika ya 23 baada ya kutengeneza pasi na kurudishiwa na James Rodríguez na kufunga bao hilo na kufanya 1-0 dhidi ya Wenyeji Liverpool. Bao la pili lilifungwa na Karim Benzema dakika ya 30 kwa kichwa baada ya kupokea Krosi safi kutoka kwa Toni Kroos.


Dakika za lala salama dakika ya 89 Gibbs ndie aliyeisawazishia bao Arsenal na kufanya 1-1 hapo hapo kwenye dakika za nyongeza Lukas Podolski alifunga bao la Ushindi na kufanya 2-1 dhidi ya RSC Anderlecht .
Dakika ya 71 kipindi cha pili Arsenal walifungwa bao na mchezaji Andy Najar baada ya kupata krosi kama kona kutoka kwa Dennis Praet na kujitwisha kichwa na kumfunga kipa wa Arsenal.
Andy Najar akishangilia bao lake la kwanza na la pekee.Alexis sanchez akiwakusanya!!!!Emiliano Martinez wa  Arsenal akipasha leo hii kabla ya Mchezo wao wa Klabu bingwa Ulaya  (Champions League) Ugenini.
 Alex Oxlade-Chamberlain akipasha nae kwenye Uwanja wa  Vanden Stock
Aaron Ramsey akipasha tayari kwa kipute  dhidi ya Anderlecht
You might also like:

MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya nchini,Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya kuonekana na mavazi halisi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Tamasha la Fiesta lililofanyika jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Diamond amejikuta akifikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya Meneja wake Babu Tale kamatwa na jana kwa kuhojiwa na kulala mahabusu kuhusiana na matumizi hayo ya mavazi ya kijeshi katika onyesho la Fiesta mwishoni wiki.
Kufuatia tukio la Diamond Platinumz kuonekana akiperform na sare zinazoaminika kuwa za jeshi la Wananchi (JWTZ), imeelezwa kuwa jeshi la Polisi limemshikilia meneja wa Diamond, Babu Tale na inaelezwa kuwa alilala selo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa katika eneo la kituo cha polisi cha Osterbay, Dar es Salaam jana (October 21), Babu Tale alifikishwa katika kituo hicho ambapo maafisa kadhaa wa jeshi na polisi walionekana katika eneo hilo.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa Uongozi wa Diamond ulipewa muda wa kujieleza kabla ya saa mbili asubuhi, October 21 lakini haukufanya hivyo na ndipo hatua hiyo ikachukuliwa. Haijafahamika bado kwa nini jeshi la Polisi lilimshikilia Babu Tale peke yake bila Diamond lakini vyanzo vimeeleza kuwa mwanamuziki huyo yuko safarini. Hadi habari hii inaenda hewani, namba ya simu ya Babu Tale ilikuwa haipatikani.

Tovuti ya Times Fm imeongea na kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Dar es Salaam, Camillus Wambura ambaye amesema bado hajawasiliana na kituo cha Osterbay kuhusu suala hilo na hajapata taarifa kwa kuwa kesi hiyo inachunguzwa na iko chini ya mkuu wa upelelezi wa Mkoa.

“Mimi ninachojua kuwa suala hilo liko chini ya uchunguzi. Habari ya kushikiliwa watu na mimi bado sijafahamu. Najua tu suala hilo liko chini ya uchunguzi na linafanyiwa uchunguzi. Hiyo ni kesi ambayo iko chini ya mkuu wa upelelezi wa Wilaya, chini ya mkuu wa upelelezi wa Mkoa. Kwa hiyo sijapokea taarifa ya uchunguzi huo ulipofika.” Ameiambia tovuti ya Times Fm.


Akijibu kuhusu taarifa za uongozi wa Diamond na Diamond kupewa muda wa kujieleza, Kamanda Wambura alijibu:
“Uchunguzi unafanywa huko. Kwa sasa hivi sina taarifa hiyo nina mambo mengi sana. Kwa hiyo kwa sasa hivi uchunguzi unafanywa chini ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa. Kwa hiyo sijapata nafasi ya kujua wamefikia wapi katika uchunguzi wa suala hilo,”ameongeza kamanda Wambura.

Mapema wiki hii, jeshi la wananchi Tanzania lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari likipiga marufuku raia kuvaa sare za jeshi.
NeymaJr aliendeleza tabia yake ya kufunga, huku Lionel Messi akiendelea kushindana na Cristiano Ronaldo katika orodha ya kuwania ‘ heshima ya mfungaji bora wa muda wote’ wa ligi ya mabingwa Ulaya. Messi pamoja na Ronaldo wamebakiza mabao mawili mawili kila mmoja ili kufikia rekodi ya muda mrefu ya mabao 69 ambayo inashikiliwa na mshambulizi wa zamani wa Hispania na klabu ya Real Madris, Raul Gonzalez Blanco.
Barcelona ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa pili msimu huu baada ya kupoteza mchezo dhidi ya vinara wa kumdi hilo, PSG wiki tatu zilizopita. Ushindi wa usiku wa jana dhidi ya Ajax umewafanya mabingwa hao wa zamani kufikisha pointi sita, pointi moja nyuma ya mabingwa wa Ufaransa ambao walishinda ushindi mwembamba dhidi ya Apoel Nicosia katika uwanja wa Neo GSP Stadium, shukrani kwa bao la dakika ya 87 kutoka kwa Edson Cavani.
Anwar El-Ghazi aliwafungia Ajax bao la kufutia machozi katika dakika ya 88 lakini kinda Sandro Ramirez ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Neymar alifunga bao la tatu kwa wenyeji na kutengeneza ushindi wa mabao 3-1 katika dimba la Camp Nou
Didier Drogba alifunga bao lake la kwanza katika kikosi cha Chelsea. Drogba mara ya mwisho aliifungia Chelsea katika mchezo wa fainali wa michuano hiyo dhidi ya Bayern Munich miaka miwili iliyopita. Akiingia uwanjani kuchukua nafasi ya Loic Remy aliyeumia katika dakika ya 16, Drogba alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika saba baadae. Chelsea ilichomoza na ushindi wa kishindo wa mabao 6-0 dhidi NK Maribor.
Remy alifunga bao la kuongoza katika uwanja wa Stamford Bridge katika dakika ya 13, nahodha, John Terry alifunga bao tatu katika dakika ya 31 na kufanya wenyeji kupumzika wakiwa na mabao 3-0. Mlinzi wa Maribor, Mitja Viler alijifunga katika dakika ya 54, EDem Hazard akafunga kwa mkwaju wa penalti zikiwa zimesalia dakika 13 mchezo umalizike na Hazard akarudi kwa mara nyingine kuhitimisha ushindi wa Chelsea kwa bao la dakika ya mwisho ya mchezo.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, mshambulizi, Maxim Choupo-Moting alifunga bao la ushindi katika mchezo ambao ulitoa mabao saba. Wenyeji, Svhalke 04 waliduwazwa na bao la mapema la kiungo-mshambulizi, Nani. Chinedu Obasi aliwafungia wenyeji bao la kusawazisha na kufanya hadi mapumziko ubao wa matokeo kusoma ‘ FC Schalke 1-1 Sporting Lisbon.
Wageni walicheza pungufu kwa dakika 60 baada ya kiungo ,Mbrazil, Mauricio Dos Santos Nascimento kuondoshwa uwanjani kwa kasi nyekundu katika dakika ya 33. Mshambulizi, Klans Jan Huntelaar aliwafungia wenyeji bao la pili dakika tano bsaada ya kuanza kwa kipindi cha pili, mlinzi Benedikt Howedes alifunga bao lingine katika dakika ya 60 lakini Sporting walirudi kwa kasi wakiwa pungufu na kufunga bao la mkwaju wa penalti kupitia kwa Adrien Silva dakika nne baada ya Schalke kufunga bao la tatu.
Raia huyo wa Brazil alifunga bao lingine dakika ya 78 na kutengeneza matokeo ya 3-3 kabla ya kupoteza mchezo huo dakika ya mwisho. Kwa matokeo hayo, Chelsea Chelsea wanaongoza kundi hilo wakiwa na pointi saba, wakifuatiwa na Schalke 04 wenye pointi tano, Maribor wanashika nafasi ya tati wakiwa na pointi mbili wakati Sporting wanaburuza mkia wakiwa na pointi moja. Kila timu I,echeza michezo mitatu.


Bayern Munich wakipongezana..Kipindi cha kwanza Bayern Munich wanaongoza bao 5-0 dhidi ya As Roma
Robben aanza kutema cheche!! Afungua pazia kwa kufunga bao na kuitanguliza Bayern mbele ya bao 1-0. Arjen Robben ndie aliyeanza kufunga bao la mapema dakika ya 8.
Mario Götze akaongeza bao la pili dakika ya 23, Huku Robert Lewandowski akichapa bao la tatu dakika chache kupita kwenye dakika ya 25, Arjen Robben aliongeza bao tena kwenye dakika ya 30 na Thomas Müller kushona bao la tano dakika ya 36 kwa 

mkwaju wa penati. Bao la As Roma limefungwa na Gervinho dakika ya 66' Bao la sita lilifungwa na F. Ribéry katika dakika ya 78 huku  X. Shaqiri akimaliza mchezo dakika 80 kwa kupachika bao la saba na kufanya 7-1 dhidi ya As Roma.


Kipindi cha kwanza dakika ya 13 Loïc Remy anaipachikia bao Chelsea baada ya kuwakaanga mabeki wa NK Maribor akipata pasi toka kwa kepteni John Tery  na kuwatanguliza mbele ya bao 1-0 dhidi ya NK Maribor. 
D. Drogba aliifungia bao la pili dakika ya 23 kwa mkwaju maridadi wa penati na bao la tatu alifunga Timu Kepteni wao John Terry katika dakika ya 31. Kipindi cha pili dakika ya 54 mchezaji wa Nk Maribor Mitja Viler alijifunga bao na kuwapa bao la nne Chelsea. 
Dakika ya 64 Agim Ibraimi alikosa penati baada ya mpira kugonga posti. Chelsea bao lake la tano limefungwa kwa mkwaju wa penati na Eden Hazard katika dakika ya 77 kipindi cha pili. Eden Hazard alimaliza mchezo kwa kufunga bao la mwisho la 6 katika dakika ya majeruhi ya 90 na mchezo kumalizika 6-0.Wachezaji wa Chelsea wakijifua tayari kwa kuumana uso kwa uso kwa uwakaribisha NK MariborUEFA CHAMPIONS LEAGUE
RATIBA/MATOKEO
Jumanne Oktoba 21
KUNDI E

CSKA Moscow 2 vs 2 Man City FT
AS Roma vs Bayern Munich

KUNDI F
APOEL Nicosia vs Paris St-Germain
Barcelona vs Ajax

KUNDI G
Chelsea vs NK Maribor
FC Schalke 04 vs Sporting Lisbon

KUNDI H
BATE Borisovs vs Shakhtar Donetsk
FC Porto vs Athletic Bilbao

waliotembelea blog