Tuesday, September 10, 2013

usiku wa Saida Wafana Bukoba!

Tamasha la Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili nchini Saida Karoli limefana usiku huu kwenye ukumbu wa Lina's Night Club Bukoba. Tamasha lililokuwa linaitwa "usiku wa Saida Kaoli" huku watu wengi wakijitokeza kumuona kwa mara ntingine hapa Bukoba Tangu azushiwe na wadau kwamba alifariki Dunia katika ajali ya boti miezi michache iliyopita habari iliyokuwa ya uzushi mtupu na ya uhongo. Leo hii jumamosi akiwa amesindikizwa na wasanii wa hapa Nyumbani Bukoba Bk Sande, Papaa Kishaju, wanamuziki wa VISION MUSIC AMBASSADOR wanaodhaminiwa na 100.0 Vision fm Radio BUKOBA na Kundi la Ka Jay Poda kutoka Kenya wameusindikiza usiku wa SAIDA KAROLI vilivyo na kukamua kisawasawa kwenye ukumbi LINA'S usiku huu. 
Saida Karoli akiimba baadhi ya nyimbo zake mpya
Willy Kiroyera kulia akicheza na Saida Karoli
Saida karoli mizuka ikimpanda
Baadhi ya wageni rasmi meza kuu kushoto ni Afisa Utamaduni
Ilifika nafasi ya msanii wa kizazi kipya BK Sande nae akapanda kwenye steji  kuporomosha nyimbo zake kuwaburudisha mashabiki wake ukumbini.
Bk Sande mtoto wa Nyumbani akiendelea kuimba
Bk Sande
Kulia Mkuu wa Chuo cha KCC Bw. Subira  na mkewe wakiburudishwa hapa na wanamuziki wa hapa Nyumbani


Saida na Wanamuziki wake wakiendelea kuimba
Ukumbi ukiburudika vilivyo usiku huu

Saida akiimba

Kweli bado jembe saida!!
Usiku wa Saida na Saida akiutendea haki hapa!!
Baadhi ya wadau waliojitokeza usiku huu
Saida Karoli akiendelea kuburudisha
Kundi ka Ka jay Poda kutoka Kenya likitumbuiza ukumbini
Tanzania safii...Raha ya Nyumbani, angalia na wazungu nao wapo wakiburudishwa.
Kiongozi wa kundi la ka jay poda!! kutoka kenya akikata mauno usiku huu
Kiongozi wa kundi la ka jay poda!! kutoka kenya
Wadau mbalimbali
Bw. Muganyizi
Kulia ni Mgeni Rasmi Afisa Utamaduni na kushoto ni mwandaaji wa Tamasha hili ambaye ni mkuugenzi wa Tivol Studio ya jijini Mwanza.
Wageni Rasmi.

Bw. Willy O Rutta ( Kiroyera) kulia na Bw. Ernest Nyambo wakicheki kisawasawa burudaniDada akibaki mdomo wazi huku akiwa aamini macho yake kwa kile alichoburudishwa kutoka kwa msanii mkongwe Saida Karoli.
Kila mtu hapa alitamani kusimama na kucheza maana nyimbo zenyewe zilihamasisha kucheza
Chezea Saida wewe!!
Usikubali kupitwa na wakati!!!
Dada ilibidi wanyanyuke na wamsogelee Saida huku ngoma ikicharazwa na Saida mwenyewe!!
Wakati ndio huu!!!

Kesho Jumapili Tarehe 8.9.2013 Saida ataendelea kwenye tamasha la pili katika uwanja wa Kaitaba Kiingilio ni Tsh.2500/= tu. Saida Karoli atasindikizwa na Jopo la wasanii lukuki waliowahi kurekodia nyimbo zao ndani ya Tivol Studio wakiwemo wasanii wa nchi Jirani na wa hapa nyumbani Bukoba.
Hapa umefika!!
Ni yeye kweli au!!
Hapa ni nyumbani kukamua lazima!!1
wewe!!eee
Dada akitokelezea kwenye jicho la kamera
Wadau. kulia ni Bw. jamal kurumuna

waliotembelea blog