Sunday, August 10, 2014

  Daniel Sturridge akicheza muziki kama kawaida yake baada ya kufunga bao lake katika dakika ya 10 dhidi ya  Borussia Dortmund

Kocha wa Liverpool  Brendan Rodgers akisalimiana na kocha Jurgen Klopp kabla ya mtanange kuanza

 Glen Johnson akimtawanya mchezaji wa  Borussia Dortmund Patrick Aubameyang
Sturridge alifunga bao na kufanya  1-0 dhidi ya Dortmund ndani ya dakika 10 tuu

 Dejan Lovren akifunga bao lake

 Henrikh Mkhitaryan akichuana vikali na  Jordan Henderson juu kwa juu ili amtoe mpira

 Martin Skrtel na Jordan Henderson wakifurahia ushindi

Lukas Piszczek akigombea mpira na Raheem SterlingKocha wa Liverpool Brendan Rodgers
VIKOSI VILIVYOKUWA:
Liverpool:
Mignolet; Manquillo (Kelly 85'), Johnson (Enrique 61'), Skrtel, Lovren; Gerrard, Can (Lucas 46'), Henderson (Allen 80'), Sterling, Coutinho (Ibe 72'); Sturridge (Lambert 76').
Subs (not used): Jones, Toure, Sakho, Coates, Suso
Goals: Sturridge 10' Lovren 14' Coutinho 49' Henderson 61'
Borussia Dortmund: Langerak; Piszczek (Großkreutz 58'), Sokratis (Knystock 81'), Ginter, Schmelzer (Sarr 81'); Kehl (Bender 46'), Kirch (Immobile 46'), Mkhitaryan (Ji 64'), Aubameyang (Bandowski 76'), Jojic (Amini 77'); Ramos (Hofmann 46')
Subs (not used): Bonmann, Subotic

Nyota wa muziki wa bongo fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platinum' akilitawala jukwaa pamoja na baadhi ya wacheza shoo wake katika onyesho la kwanza la tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza lililofanyika mwishoni mwa wiki,tamasha hilo litaendelea kwenye miji mingine ya Bukoba na Kahama mwishoni mwa wiki.

Baada ya kazi ya kuwaburudisha mashabiki wake,Mara Wema Sepetu a.k.a shemeji nae akajiunga kumpa sapoti mpenzi wake jukwaani.

Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2014 lililoanza rasmi katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

Diamond na Ney wa Mitego wakioneshana umwamba wa kuwateka mashabiki kila mmoja kwa staili yake,huku miluzi na Shangwe ikiwa imtawala ndani ya uwanja.
Mmoja wa wasanii anaefanya vyema kwa sasa katika anga ya muziki wa bongofleva Vanessa Mdee a.k.a V Money akitumbuiza mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza (hawapo pichani) waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mrindimo wa tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo,tamasha hilo limefanyika mwishoni mwa wiki.

Miss Ethiopia akifurahia taji la kuwa Miss Africa katika mashindano hayo yaliyofanyika Rockville, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Mshiriki wa Tanzania, Joy Kalemera ameshika nafasi ya 4 kati ya washiriki 20 walioingia fainali hizo.
Washiriki watano waliopata nafasi ya kuingia tano bora kutoka kushoto ni Miss Tanzania aliyeshika na 4, Miss Uganda aliyeshika na 2, Miss Ethiopia aliyeshinda, Miss Guinea aliyeshika namba 3 na Miss Nigeria aliyeshika namba 5.

Washindi namba 2 mpaka 4 wakiangalia Miss Ethiopia akivishwa taji, kushoto ni miss Cameoon aliyekua Miss Africa USA msimu uliopita.

Washiriki wote 20 katika picha ya pamoja.

Miss Ethiopia akipata picha ya pamoja na washindi namba 2 na 3 ambaye ni Miss Uganda na Miss Guinea.

Miss Ethiopia katika picha ya pamoja na mshindi namba 2 Miss Uganda.

Miss Ethiaopia akipata picha na wageni akiwepo Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

PBP_4315
baadhi ya wadau wa Bavaria wakibadilishana mawazo wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na jovet Tanzania limited wasambazaji wa kinywaji cha Bavaria eneo la afrika mashariki
PBP_4328
Ndugu Justus kyolike meneja masoko mkazi wa Bavaria akiteta na wadau wa Bavaria
PBP_4484
Mkurugenzi mkuu wa Jovet Tanzania Limited ndugu John Kessy akitafakari jambo wakati wa chakula cha jioni alichowaandalia wakala wa Bavaria eneo la afrika ya mashariki.
PBP_4677
Ndugu John Kessy mkurugenzi wa kampuni ya Bavaria akimpongeza innocent gasangwa, wakala wa Bavaria kutoka nchini Rwanda
………………………………………………………………………………………………………………..
Wakati uchumi wa Tanzania ukiendelea kukua siku hadi siku, ongezeko la wananchi wenye kipato cha kati nalo limezidi kukua, na hivyo kuleta changamoto mpya katika masoko ya bidhaa mbalimbali hapa nchini.
Waagizaji wa kinywaji Kutoka Uholanzi cha Bavaria eneo la Afrika ya Mashariki, Jovet (Tanzania) Limited wamedhamiria kuleta changamoto hiyo baada ya kuzindua kampeni rasmi ya mbio za kuelekea kileleni, na hivyo kuongeza wigo wake katika soko hili la Afrika ya Mashariki, ambalo limekua likikua kwa kasi kiuchumi.
Akiongea katika chakula cha jioni na mawakala wakubwa wa kinywaji hicho katika eneo la Afrika ya Mashariki katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, bwana John Kessy, Mkurugenzi mkuu wa Jovet (Tanzania) Limited, alisema, Kampeni hii ya Bavaria ya kuelekea kileleni imelenga kuleta changamoto kubwa katika eneo hili la Afrika ya mashariki, kwa kuwa litasaidia kutengeneza ajira zaidi, na kuongeza kipato binafsi na kwa serikali kwa ujumla. Bwana Kessy aliongeza na kusema kuwa, Tumeweza kupenya katika soko hili na kutengeneza mahusiano mazuri na wafanyabiashara. Tutaendelea kukua siku hadi siku tukiwapatia wateja wetu kilicho bora zaidi.
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia hamsini ya wanywaji wa vinywaji vya shayiri wako eneo la Mashariki ya kati na Afrika na asilimia hii hutumia hektolita milioni 18 kwa mwaka, na hii imetokana na kwamba watu wengi wamekua wakijali zaidi afya zao, na hivyo Bavaria inataka kutumia fursa hii kujikita zaidi katika eneo hili, na kuwapa fursa walaji kupata uchaguzi zaidi.
Mawakala hawa pia waliweza kupata fursa ya kujifunza mengi kuhusu kinywaji cha Bavaria, na pia mbinu za kufanya biashara katika siko hili ambalo limekua likikua kwa kasi na lenye ushindani mkubwa. Pamoja na kujifunza mengi kuhusu Bavaria na mbinu za kibiashara, mawakala hao pia waliweza kujishindia zawadi mbalimbali, zikiwemo seti za Televisheni, Simu za Mkononi na vinywaji mbalimbali vya familia ya Bavaria.
Takwimu za hivi karibuni za mwaka 2010-2015 zinaonyesha kuwa soko la vinywaji linatarajiwa kukua na kuzalisha zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.9, na tafiti hii imefanywa na kampuni ya MarketLine.

01
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya  Msama  Promotion Bw. Alex Msama kulia na mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje katikati na Mwimbaji Chengula kushoto wakati wa tamasha la uzinduzi wa Albam ya “Shikilia Pindo la Yesu” uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo akisindikizwa na waimbaji malimbali wa muziki huo akiwemo Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia, Albam hiyo imezinduliwa na Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula ambaye alimwwakilisha Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari Makamba, Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa ujumbe aliouwakilsha katika uzinduzi huo kutoka kwa Mh. Januari Makamba . Mabula ameuelezea ujumbe huo kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kushawishi makampuni mbalimbali ili yadhamini pia matamasha ya muziki wa injili kama  ambavyo yamekuwa yakifuturisha vikundi na waumini mbalimbali wakati wa mfungo mtukufu wa wezi wa ramadhan,  kwakuwa muziki wa injili pia unaeneza amani na upendo kwa jamii ya watanzania, Hii itasaidia  kupunguza gharama  za uandaaji jambo ambalo kwa namna moja au nyingine litakuwa linarahisisha uandaaji wa matamasha hayo ambayo yamekuwa ni chachu ya watu kuachana na maovu na kuwa watu wema katika jamii
7
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba wakati wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
1
Meya wa  jiji la Mwanza ya Mhe.Stanslaus Mabula akinyanyua juu albam za mwimbaji Rose Muhando wakati alipozindua albam hiyo mkoani Mwanza leo kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
2
Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula kulia akiwa amesimama na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati wa uzinduzi huo kutoa kulia ni waimbaji Chengula Bony Mwaiteje , Tumaini Njole na Rose Muhando.
3
Mmoja wa waratibu wa uzinduzi huo Bw. Hudson Kampga akizunguza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Alex Msama.
4
Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion wa  Msama Alex, kulia anayefurahia ni mwimbaji Rose Muhando.
5
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama  akigawa albam ya Rose Muhando kwa Mh. Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Maaskofu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
6 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw.  Alex Msama akizungumza machache katika uzinduzi huo.
8
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akikamua na wacheza shoo wake  wakati wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
9
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akipagawisha mashabiki wake  wakati wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
10
Umati wa maelfu ya wa waliohudhuria katika uzinduzi hu wakinyanyua mikono juu juu.
11 12 13
Mwimbaji Bony Mwaiteje akifanya vitu vya sarakasi jukwaani.
14
Miwmbaji wa kimataifa kutoka zambia Ephraim Sekereti ni mmoja wa waimbaji waliokonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa injili.
15
Noa Vicoria Singers wakafanya vitu vyao.
16
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama  akifanya vitu vyake na MC Mwakipesile.
17
Miwmbaji Tumaini Njole akafanya mambo yake pia katika uzinduzi huo
18
Ni Full Burudani ya muziki wa injili.
19
Miwmbaji Tumaini Njole akiimba kwa hisia kali katika uzinduzi huo

Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa washindi.

Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akikabidhi zawadi ya jezi na mpira kwa washindi.

Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John na wageni wa meza kuu wakifuraia jambo.

Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akisalimiana na wachezaji kabla ya kipute kuanza.

Picha ya pamoja kati ya wachezaji na mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa pamoja na Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John.

Mashindano ya Mbagala Cup
Mashindano ya Mbagala Cup
Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi.
Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi.
Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi. Kushoto ni Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John.

Mashabiki wa Que Bac washindi wakiwa wamembeba goli kipa wao wakishangilia.
Mashabiki wa Que Bac washindi wakiwa wamembeba goli kipa wao wakishangilia.
mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) akikabidhi zawadi kwa golikipa bora.
mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) akikabidhi zawadi kwa golikipa bora.
Mchezaji bora akipokea kitita cha shilingi laki moja toka kwa mgeni rasmi Mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa.

Timu kapteni wa Kipati akikabidhiwa zawadi ya timu yao na mgeni rasmi.
Timu kapteni wa Kipati akikabidhiwa zawadi ya timu yao na mgeni rasmi.
TIMU ya Vijana ya Mpira wa Miguu ya Que Bac ya Mbagala Kipati jijini Dar es Salaam jana imeibuka bingwa wa Mashindano ya Mbagala Cup baada ya kuibugiza timu ya mpira wa miguu ya Kipati magoli 2 kwa bila. Que Bac imetawazwa mabingwa na kukabidhiwa Mbuzi, seti moja ya jezi pamoja na mpira.
Que Bac ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Kipati ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza ambapo mshambuliaji wao hatari, Yahya Tumbo (9) alikwamisha mpira katika nyavu za wapinzani baada ya kuunganisha pasi kutoka kwa mchezaji mwenzake. Lakini hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Que Bac walikuwa mbele kwa goli moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo wachezaji wa Kipati waliongeza mashambulizi kwa wapinzani wao kutaka kusawazisha goli lakini goli kipa wa Que Bac pamoja na walinzi wake walikuwa makini na kuondoa hatari zote mara kadhaa langoni mwao.
Jahazi la Kipati lilizamishwa zaidi na mshambuliaji wa Que Bac, Shine Duu jezi namba 17 ambaye alifanikiwa kuifungia timu yake goli la pili na kuongeza matumaini ya kutangazwa Mabingwa wa Mashindano hayo (Mbagala Cup). Hadi kipenga cha mwisho Que Bac 2 na Kipati 0.
Akizungumza mara baada ya mchezo wa fainali, Mratibu wa Mashindano hayo, Musa Hemed (Kibwetele) alisema mashindano hayo yalianza rasmi Aprili 5, 2014 ambapo timu 16 zilishiriki katika mashindano huku zikiwa katika makundi mawili, yaani A na B na kila kundi lilikuwa na timu nane. Alisema mshindi wa pili katika mashindano hayo amefanikiwa kupata seti moja ya jezi pamoja na mpira, huku zawadi mbalimbali zikitolewa kwa wachezaji na timu yenye nidhamu.
Alisema lengo la mashindano hayo ilikuwa kuwakuza vijana katika vipaji vyao kwenye fani ya mpira wa miguu pamoja na kuwaunganisha vijana kushiriki katika michezo kwa pamoja. “…Sisi eneo letu tumezoea kuona mashindano ambayo yanaanzishwa labda na diwani lakini tena mara moja kwa muda mrefu. Sasa mimi nikakaa na kufikiria nasie vijana tunaweza kujipanga na kuanzisha mashindano kama hayo,…nikazialika timu tukachangishana ada kidogo na hatimaye tukapata mlezi wa mashindano na yamefanyika,” alisema Kibwetele.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi, mgeni rasmi katika fainali hizo alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia na Mawasiliano Mamlaka ya Bandari (TPA) ambaye pia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Temeke (MNEC), Phares Magesa ameahidi kuyafadhili mashindano hayo kuanzia sasa na atakuwa akiwezesha kufanyika kwake.
Mbali na kiongozi huyo kuyafadhili liongeza zawadi kwenye mashindano hayo ambapo alitoa shilingi laki moja moja kwa mchezaji bora, kipa bora na waamuzi na kamati ya maandalizi wa mashindano hayo.
Naye Mlezi wa Mashindano hayo, Emmanuel John alisema lengo la mashindano hayo ni kutaka kuwaleta vijana karibu, kuleta upendo dhidi yao na kudumisha umoja na amani kwa vijana wote. Alisema mashindano kama hayo yanawatoa vijana kutoka katika mtizamo ya wao kukaa vijiweni na kujishughulisha na michezo zaidi ambayo inamanufaa kwao kuliko kushinda wakipiga soga kwenye makundi vijiweni. Zimeshiriki Kata tano za Kata ya Mbagala, Kata ya Kiburugwa, Kata ya Kijichi, Mbagala Kuu
“Unajua vijana wengi mitaa yetu wanakaa vijiweni si kwamba wanapenda kufanya hivi, wanafanya tu kwasababu wanakosa cha kufanya…sasa kuna kila sababu watu wenye nafasi kujitokea na kuwawezesha ili kuwatoa walipo, nimetokea mimi nimedhamini mashindano yamefanyika, wameshindana na vijana wamepata burudani, upendo na amani pia mshindi kapatikana,” alisema.
Aidha alisema wapo vijana wengi wenye vipaji ambao wanaitaji kupewa nafasi za kushiriki katika mashindano kama hayo na hatimaye vipaji vyao kuonekana na kuendelezwa katika mashindano ya juu. “…Tumeona leo hapa vijana wameondoka na zawadi mbalimbali wachezaji bora wamezawadiwa, timu bora, golikipa bora kapatikana, timu zimejishindia jezi na mipira vyote vyao…timu hizi awali zilikuwa zikicheza na jezi za kukodisha lakini leo wamepata za kwao baada ya kushinda,” alisema.
Kijana huyo alisema anajivunia kuwa sehemu ya kupunguza maovu kwa vijana kwani katika kipindi chote cha mashindano hayo vijana walielekeza nguvu zao nyingi kwenye michezo kimashindano jambo ambalo anaamini limepunguza baadhi wenye nia ovu kubadili mienendo yao kutokana na mashindano hayo. Pamoja na hayo aliishauri Serikali na vyama vya soka kushuka ngazi ya chini mitaani kusaka vipaji vya michezo anuai kwani zipo vingi lakini vinakosa fursa ya kuonekana.

waliotembelea blog