Mwimbaji wa muziki wa injili Rose
Muhando akiimba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw.
Alex Msama kulia na mwimbaji wa muziki wa injili Bonny Mwaiteje
katikati na Mwimbaji Chengula kushoto wakati wa tamasha la uzinduzi wa
Albam ya “Shikilia Pindo la Yesu” uliofanyika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza leo akisindikizwa na waimbaji malimbali wa muziki
huo akiwemo Ephraimu Sekereti kutoka nchini Zambia, Albam hiyo
imezinduliwa na Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula
ambaye alimwwakilisha Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari
Makamba, Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa ujumbe
aliouwakilsha katika uzinduzi huo kutoka kwa Mh. Januari Makamba .
Mabula ameuelezea ujumbe huo kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo
kushawishi makampuni mbalimbali ili yadhamini pia matamasha ya muziki wa
injili kama ambavyo yamekuwa yakifuturisha vikundi na waumini
mbalimbali wakati wa mfungo mtukufu wa wezi wa ramadhan, kwakuwa muziki
wa injili pia unaeneza amani na upendo kwa jamii ya watanzania, Hii
itasaidia kupunguza gharama za uandaaji jambo ambalo kwa namna moja au
nyingine litakuwa linarahisisha uandaaji wa matamasha hayo ambayo
yamekuwa ni chachu ya watu kuachana na maovu na kuwa watu wema katika
jamii
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba wakati wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
Meya wa jiji la
Mwanza ya Mhe.Stanslaus Mabula akinyanyua juu albam za mwimbaji Rose
Muhando wakati alipozindua albam hiyo mkoani Mwanza leo kwenye uwanja wa
CCM Kirumba.
Meya wa jiji la
Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula kulia akiwa amesimama na Mkurugenzi wa
kampuni ya Msama Promotion wakati wa uzinduzi huo kutoa kulia ni
waimbaji Chengula Bony Mwaiteje , Tumaini Njole na Rose Muhando.
Mmoja wa waratibu wa uzinduzi huo Bw. Hudson Kampga akizunguza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Alex Msama.
Meya wa jiji la
Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Msama Promotion wa Msama Alex, kulia anayefurahia ni mwimbaji Rose
Muhando.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akigawa albam ya Rose Muhando kwa Mh. Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Maaskofu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza machache katika uzinduzi huo.
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose
Muhando akikamua na wacheza shoo wake wakati wa tamasha hilo kwenye
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose
Muhando akipagawisha mashabiki wake wakati wa tamasha hilo kwenye
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
Umati wa maelfu ya wa waliohudhuria katika uzinduzi hu wakinyanyua mikono juu juu.
Mwimbaji Bony Mwaiteje akifanya vitu vya sarakasi jukwaani.
Miwmbaji wa kimataifa kutoka zambia Ephraim Sekereti ni mmoja wa waimbaji waliokonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa injili.
Noa Vicoria Singers wakafanya vitu vyao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akifanya vitu vyake na MC Mwakipesile.
Miwmbaji Tumaini Njole akafanya mambo yake pia katika uzinduzi huo
Ni Full Burudani ya muziki wa injili.
Miwmbaji Tumaini Njole akiimba kwa hisia kali katika uzinduzi huo
0 maoni:
Post a Comment