baadhi ya wadau wa Bavaria
wakibadilishana mawazo wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na
jovet Tanzania limited wasambazaji wa kinywaji cha Bavaria eneo la
afrika mashariki
Ndugu Justus kyolike meneja masoko mkazi wa Bavaria akiteta na wadau wa Bavaria
Mkurugenzi mkuu wa Jovet Tanzania
Limited ndugu John Kessy akitafakari jambo wakati wa chakula cha jioni
alichowaandalia wakala wa Bavaria eneo la afrika ya mashariki.
Ndugu John Kessy mkurugenzi wa kampuni ya Bavaria akimpongeza innocent gasangwa, wakala wa Bavaria kutoka nchini Rwanda
………………………………………………………………………………………………………………..
Wakati uchumi wa Tanzania
ukiendelea kukua siku hadi siku, ongezeko la wananchi wenye kipato cha
kati nalo limezidi kukua, na hivyo kuleta changamoto mpya katika masoko
ya bidhaa mbalimbali hapa nchini.
Waagizaji wa kinywaji Kutoka
Uholanzi cha Bavaria eneo la Afrika ya Mashariki, Jovet (Tanzania)
Limited wamedhamiria kuleta changamoto hiyo baada ya kuzindua kampeni
rasmi ya mbio za kuelekea kileleni, na hivyo kuongeza wigo wake katika
soko hili la Afrika ya Mashariki, ambalo limekua likikua kwa kasi
kiuchumi.
Akiongea katika chakula cha jioni
na mawakala wakubwa wa kinywaji hicho katika eneo la Afrika ya Mashariki
katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, bwana John Kessy,
Mkurugenzi mkuu wa Jovet (Tanzania) Limited, alisema, Kampeni hii ya
Bavaria ya kuelekea kileleni imelenga kuleta changamoto kubwa katika
eneo hili la Afrika ya mashariki, kwa kuwa litasaidia kutengeneza ajira
zaidi, na kuongeza kipato binafsi na kwa serikali kwa ujumla. Bwana
Kessy aliongeza na kusema kuwa, Tumeweza kupenya katika soko hili na
kutengeneza mahusiano mazuri na wafanyabiashara. Tutaendelea kukua siku
hadi siku tukiwapatia wateja wetu kilicho bora zaidi.
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia
hamsini ya wanywaji wa vinywaji vya shayiri wako eneo la Mashariki ya
kati na Afrika na asilimia hii hutumia hektolita milioni 18 kwa mwaka,
na hii imetokana na kwamba watu wengi wamekua wakijali zaidi afya zao,
na hivyo Bavaria inataka kutumia fursa hii kujikita zaidi katika eneo
hili, na kuwapa fursa walaji kupata uchaguzi zaidi.
Mawakala hawa pia waliweza kupata
fursa ya kujifunza mengi kuhusu kinywaji cha Bavaria, na pia mbinu za
kufanya biashara katika siko hili ambalo limekua likikua kwa kasi na
lenye ushindani mkubwa. Pamoja na kujifunza mengi kuhusu Bavaria na
mbinu za kibiashara, mawakala hao pia waliweza kujishindia zawadi
mbalimbali, zikiwemo seti za Televisheni, Simu za Mkononi na vinywaji
mbalimbali vya familia ya Bavaria.
Takwimu za hivi karibuni za mwaka
2010-2015 zinaonyesha kuwa soko la vinywaji linatarajiwa kukua na
kuzalisha zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.9, na tafiti hii
imefanywa na kampuni ya MarketLine.
0 maoni:
Post a Comment