Sunday, February 5, 2017



Usiku wa February 5 ndio siku ambayo mchezo wa fainali ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON 2017 ulichezwa,  mchezo wa fainali ya AFCON 2017 ulikuwa unazikutanisha timu za Misri dhidi ya Cameroon, lakini Cameroon wamefanikiwa kufuta uteja kwa kufungwa fainali mbili na Misri.

Cameroon wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1, Nicolas N’koulou alifunga goli la kusawazishia Cameroon dakika ya 58 baada ya Mohamed Elneny kuifungia Misri goli la uongozi dakika ya 22, Vincent Aboubakar ndio alizima ndoto za Misri baada ya dakika ya 88 kufunga goli la ushindi.

Ushindi huo unakuja baada ya Cameroon kufumgwa fainali mbili za AFCON na Misri, alifungwa fainali ya AFCON 2008 goli 1-0 Mohamed Aboutrika akifunga goli hilo, lakini walipoteza fainali ya AFCON 1986, Cameroon wanakuwa wamechukua taji lao la tano la AFCON wakati Misri wanabakia na rekodi yao ya kuchukua mataji nane ya AFCON.

Rekodi nyingine zilizowekwa katika AFCON na Cameroon ni kuwa inakuwa timu ya kwanza kuwahi kuifunga Misri goli katika fainali za AFCON baada ya Ethiopia, huku kocha wa Misri Hector Raul  Cuper akiendeleza rekodi yake mbovu kwa kupoteza fainali yake ya sita katika soka akiwa kama kocha wa timu tofauti.


Ibra akishangilia bao lake MANCHESTER UNITED imewatandika Mabingwa wa England Leicester City 3-0 wakiwa kwao King Power Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Ushindi huu umewabakiza Man United Nafasi ya 6 lakini sasa wapo Pointi 1 nyuma ya Timu ya 5 Liverpool, Pointi 2 nyuma ya Timu ya 4 Arsenal, Pointi 4 nyuma ya Timu ya 3 Man City na Pointi 5 nyuma ya Timu ya Pili Spurs huku Chelsea wakiwa kileleni Pointi 14 mbele ya Man United.

Man United walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 41 baada ya Kichwa cha Chris Smalling kuwahiwa na Mkhitaryan kabla Beki wa Leicester Huth kuukuta Mpira na kumtoka Beki mwingine wa Leicester Morgan na kumchambua Kipa Schmeichel.

Sekunde 87 baada ya Bao hilo Man United walikuwa 2-0 mbele kwa Bao la Zlatan Ibrahimovic alieunganisha Krosi ya Valencia.
Hadi Mapumziko Leicester 0 Man United 2.

Kipindi cha Pili kuanza Timu zote zilifanya mabadiliko kwa Leicester kuwaingiza King na Gray kuwabadili Musa na Okazakina huku Man United wakimtoa Marcos Rojo na kumwingiza Daley Blind.
Man United walifunga Bao la 3 Dakika ya 49 kufuatia ushirikiano mwema wa Ibrahimovic na Mkhitaryan kumfungulia Juan Mata kupiga Bao.



http://a1.espncdn.com/combiner/i?img=%2Fphoto%2F2017%2F0205%2Fr178232_1296x518_5%2D2.jpg&w=1006&h=402&scale=crop&cquality=80&location=originBao la Egypt lilifungwa na Mohamed Elneny dakika ya (22')

Huku Nicolas N'Koulou akiisawazishia bao dakika ya (59') kipindi cha pili na dakika za lala salama Vincent Aboubakar aliipa bao dakika ya (88') na mtanange kumalizika kwa 2-1.



waliotembelea blog