Sunday, February 5, 2017


Ibra akishangilia bao lake MANCHESTER UNITED imewatandika Mabingwa wa England Leicester City 3-0 wakiwa kwao King Power Stadium kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Ushindi huu umewabakiza Man United Nafasi ya 6 lakini sasa wapo Pointi 1 nyuma ya Timu ya 5 Liverpool, Pointi 2 nyuma ya Timu ya 4 Arsenal, Pointi 4 nyuma ya Timu ya 3 Man City na Pointi 5 nyuma ya Timu ya Pili Spurs huku Chelsea wakiwa kileleni Pointi 14 mbele ya Man United.

Man United walipata Bao lao la kwanza Dakika ya 41 baada ya Kichwa cha Chris Smalling kuwahiwa na Mkhitaryan kabla Beki wa Leicester Huth kuukuta Mpira na kumtoka Beki mwingine wa Leicester Morgan na kumchambua Kipa Schmeichel.

Sekunde 87 baada ya Bao hilo Man United walikuwa 2-0 mbele kwa Bao la Zlatan Ibrahimovic alieunganisha Krosi ya Valencia.
Hadi Mapumziko Leicester 0 Man United 2.

Kipindi cha Pili kuanza Timu zote zilifanya mabadiliko kwa Leicester kuwaingiza King na Gray kuwabadili Musa na Okazakina huku Man United wakimtoa Marcos Rojo na kumwingiza Daley Blind.
Man United walifunga Bao la 3 Dakika ya 49 kufuatia ushirikiano mwema wa Ibrahimovic na Mkhitaryan kumfungulia Juan Mata kupiga Bao.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog