Tuesday, May 27, 2014

Mbeya City Usiku huu imefungwa Bao 2-1 na AFC Leopards ya Kenya katika Mechi yao ya Pili ya KUNDI B la Mashindano ya CECAFA NILE BASIN CUP iliyochezwa huko Khartoum, Sudan.
Hadi Mapumziko, Mbeya City walikuwa nyuma kwa Bao 2-0 zilizofungwa na Mudde Musa katika Dakika ya 30 na Were Paul, Dakika ya 35.

Bao la Mbeya City lilifungwa na Deus Kaseke katika Dakika za Majeruhi.
Kwenye Mechi ya Kwanza, Mbeya City waliifunga Academie Tchite ya Burundi Bao 3-2 na Mechi yao ya mwisho ya KUNDI B ni hapo Jumatano dhidi ya Enticelles ya Rwanda.

VIKOSI VILIVYOANZA:

MBEYA CITY:
BARUAN David
MWAGANE Yeya (Nahodha)
KIBOPILE Hamad
JULIUS Deogratius
YOHANNA Morris
MATOGOLO Anthony
KASEKE Deus
MAZANDA Steven
NONGA Paul
KABANDA  John
THEMY Felix

Akiba:
LAMBON Ahery
YUSUPH Abdallah
YUSUPH Wilson
ABDALLAH Seif
KENNY Ally
SEMBULI Christian
KOCHA: MWAMBUSI Juma [Tanzania]

AFC LEOPARDS:
MATASI Patrick
WERE Paul (Nahodha)
WAFULA Edwin
MASIKA Eric Chemati
SHIKOKOTI Joseph
MUDDE Musa
IKENNE Austin
ABDALLAH Juma
SALEH Jackson
MANGOLI Benard
WAFULA Noah
Akiba:
MUSALIA Martin
IMBALAMBALA Martin
JUMAAN Khalid
KADENGE Oscar
OKWEMBA Charles
KHAMATI Michael
ETEMESI Augustine
KOCHA: Hendrik Pieter De Jong [Holland]


Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’,  Kareeem Omary ‘KO’  (kushoto) akiwa na familia ya marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ Mama mzazi wa Mangwea (Katikati) na  kaka wa Mangwea, Keneth Mangwea  (kulia).
Px2  
Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’,  Kareeem Omary ‘KO’ .
Px3
Bana ya Love Concert
px4  
Taswira ya Nyumbani kwa Mama Mangwea kwa sasa.
Albert MangwairMangwea enzi za uhai  wake
..Mastaa kibao kujumuika katika ‘LOVE CONCERT’
..Afande Selle, Belle 9, Samir na wengineo –Moro
P-Funky, Mswaki, Chemba Squad kutikisa 
Na Andrew Chale
MASTAA mbalimbali nchini wakiwemo wanamuziki wanatarajiwa kushiriki kwenye tukio maalum la kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha  marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ ,  litakalofanyika ndani ya ukumbi wa  Nyumbani Park (Samaki  samaki Spot) , Kihonda Morogoro mjini Juni 28.
Akizungumza na mtando huu , Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo,  Kareeem Omary ‘KO’  alisema maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila mwaka, limepwa jina la ‘Love Concert – Kumbukumbu ya kifo cha Albert Mangwe’.
Kareem, aliwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono kwenye tukio hilo kwani litakuwa la kipekee na la aina yake  ambalo pia litatoa fursa kwa wakazi hao pia mikoa jirani na watu kutoka nje ya Tannzania ambao watauzulia. 
“Nawaomba wadau kujitokeza kuonesha  upendo  wa pamoja. Kumbukumbu  kwa mpendwa wetu kama ilivyo utamaduni wetu.” alisema Kareem.
Na kuongeza kuwa, siku hiyo   Watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa  pamoja na mama mzazi wa Mangwea  kama kumbukumbu.
Kareem aliwataja wasanii watakaotoa burundani, ni pamoja  na kutoka kwa kundi la Wanachemba ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu Ngwair,  JSqueezer, P Funky Majani na Mswaki. Kwa upande wa wasanii kutoka Morogoro ni pamoja na Afande Sele, Team Racers, Mc Koba Chris wa Marya, Belle 9,  Samir, Zombie, President  Mirrow,  Jordan wa Dejavu na wengine wengi.
Katika siku hiyo ya Juni 28, ambayo ndiyo siku aliyopatwa na umati marehemu, Kareem alisema kabla ya matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa na ibada mbili maalum ikiwemo ya  Kanisani na ile ya nyumbani.
Aidha, Kareem alisema katika tukio hilo, ambalo linatarajia kuanza majira ya jioni ya saa 10 hadi saa 12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa burudani ikiwemo ya kuimba na nyinginezo  na baadae usiku wa kuanzia saa 2 hadi majogoo wasanii hao mbalimbali watatawala jukwaa na burudani ya nguvu ya kumbukumbu.
Marehemu ‘Ngwair’  alifariki  dunia akiwa  nchini Afrika kusini, alijizolea umaarufu kwa nyimbo kama Mikasi na Nisikilize Mi na nyingine nyingi alizowahi shirikishwa na wasanii mbalimbali nchini wakiwemo Professa Jay, Nuru, TID, Chidi Benz  na wengine wengi.


Open wide: David Luiz undergoing a medical check-up at the squad's Granja Comary training complex
Character: David Luiz poses on the doctor's bed as the Brazil squad settled down in Teresopolis
 Fundi: David Luiz akiwa amelala katika kitanda cha daktari.
Waiting patiently: David Luiz pulls a face as his ears are inspected during a medical check-up
Check-up: Thiago Silva gets inspected by the doctor as preparations step up ahead of the World Cup
Specimen: Dante is put through his paces on the treadmill, attached to a monitoring system
 Dante naye hakuwa mbali
Watchful eye: Bayern Munich gets his eyes checked out at the training complex
 Nyota huyo wa  Bayern Munich akichunguzwa jicho


DSC_4490Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Mart Nooij inatarajia kujipima ubavu katika mechi ya kimataifa ya kirafiki jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) kuanzia majira ya saa 11:00 jioni.
Taifa Stars iliyopiga kambi yake mjini Tukuyu jijini Mbeya inatarajia kuwasili asuhubi hii majira ya saa 4:00 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Air Tanzania.
Wapinzani wa Taifa stars tayari wapo jijini Dar es salaam kwa ajili ya mechi hiyo muhimu kwa makocha kuangalia uimara wa timu zao kabla ya kwenda kucheza mechi za mashindano.
Stars na Malawi wanakutana kwa mara ya pili ndani ya mwezi mmoja kwani mei 4 mwaka huu walipambana tena katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kutoka suluhu pacha ya bila kufungana.
Mechi hii itatumika na kocha mkuu wa Taifa stars, Nooij, kuangalia kama kuna maboresho katika kikosi chake kinachojiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Zimbabwe mjini Harare.
Mechi ya kwanza jijini Dar es salaam ambayo Stars ilishinda kwa bao 1-0 la John Bocco `Adebayor`, safu ya kiungo ilionekana kupwaya sana, hivyo leo hii itakuwa nafasi ya kocha kuona kama viungo wake wameimarika.
Pia safu ya ushambuliaji ilionekana kukosa nafasi muhimu za kufunga na kwa muda wote walipokuwa Tukuyu, Nooij alikuwa anahangaika kunoa makali ya washambuliaji wake.
Malawi (Flames) inayonolewa na mchezaji wake wa zamani Young Chidmozi nayo itakuwa inacheza mechi ya mwisho ya majaribio kabla ya kwenda N’djamena kuikabili Chad.
Shirkisho la soka Tanzania, TFF kupitia kwa Afisa habari wake, Boniface Wambura Mgoyo limewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ambayo kwa sasa inajengwa upya.
Wambura alitaja kiingilio katika mechi hiyo kuwa kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.

waliotembelea blog