Uongozi pamoja na Wafanyakazi wa kituo cha radio ya EFM 93.7 kwa
pamoja wakikata keki kusherehekea kutimiza mwaka mmoja wa kituo hicho
ambacho kwa sasa kinakuja kwa kasi jijini Dar na kwingineko,hafla hiyo
ilikwenda sambamba na kuadhimisha miaka 16 ya msanii Mkongwe wa muziki
wa kizazi kipya Juma Nature,katika tamasha lililoitwa KOMAA
CONCERT,ambalo lilifanyika ndani ya kiota cha maraha cha Dar
Live,Mbagala jijini Dar mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na maelfu ya
mashabiki na wapenzi wa muziki .
Lengo la kuwaburudisha
Mashabiki wa Juma Nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM ilikuwa pia ni
sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka kumi na
sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo Juma Nature aingie kwenye game
ya Muziki nchini Tanzania.
Baadhi ya Wasanii walioshiriki
kulinogesha tamasha hilo ni pamoja na Profesa Jay, Shetta, Snura,
Makomando, Msagasumu na wengine wengi. Katika tamasha hilo lililowavutia
wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake,kiingilio kilipangwa kuwa ni
shilingi 7,000 tu.
Meneja Mwasiliano na mambo ya Sheria wa
EFM 93.7 Deniss ssebo alisema kuwa wanaamini Msanii Juma nature ni
msanii mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii kibao kuingia
katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa heshima kubwa
kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi kipya,alisema na
kuongeza kuwa lakini kwa Efm huyo ni msanii wa Kwanza tu na itaendelea
kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwa kuwa wanaaamini Muziki unaongea.
Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akiongoza jopo la wafanyakazi wenzake kukata keki
Pichani kulia ni Meneja Mwasiliano na mambo ya Sheria wa EFM 93.7
Deniss Ssebo akizungumza jambo mbele ya mwashabiki na wapenzi wa muziki
na pia wasikilizaji wakubwa wa kituo hicho kuhusiana na utaratibu mzima
wa sherehe hiyo,kulia ni Mkurugenzi wa Efm Dj Majay akigawa keki kwa
mashabiki waliofika kushuhudia tukio hilo ndani ya Dar Live.
Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akitumbuiza
jukwaani mbele ya mashabiki wake,pia akiwashukuru kumpa sapoti ya
kutosha tangu ameanza muziki na sasa anatimiza miaka 16 katika tasnia
hiyo adhimu.
Wakongwe pamoja Juma Nature na Prof.Jay wakishoo love kwa mashabiki wao.
Msanii Snura na Madansa wake wakilishambulia jukwaa la KOMAA CONCERT
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii
Shetta akitumbuiza mbele ya mashabiki kibao waliofika kwenye tamasha la
KOMAA CONCERT.
Makamuzi yalikuwa yakiendelea jukwaani.
Amsha amsha za hapa na pale zikiendelea jukwaani.
Mashabiki walikuwa kibao.
Deejay Spar akionesha uwezo wake kwa mashabiki.
Shabiki wa ukweli kwa Juma Nature
Burudani ilipangwa sawa bin sawia huku Ma -Mc wakinogesha shughuli
Mashabiki na mandhari ya Dar Live kwa usiku huo ndani ya jicho la samaki
Dar Live palinoga usiku huo wa KOMAA CONCERT