Monday, June 1, 2015



Mlinda wa mlango wa Manchester United, David De Gea ameshindwa kutegua kitendawili kilichotanda juu ya mstakabali wake katika klabu hiyo na kuzipa nguvu tetesi za yeye kuhamia Real Madrid anakohusishwa nako kwa muda mrefu sasa.

Real Mdrid inayotazamiwa kumtangaza Rafa Benitez kama mrithi wa Carlo Anceloti katika klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu, imekuwa ikihaha kunasa dole gumba la mlinda lango huyo na kumrudisha katika jiji alilozaliwa na kuwa mrithi wa Ika Cassilas anayeonekana kuhitaji mbadala katika klabu hiyo.
Kocha mtarajiwa wa Real Madrid

David De Gea amebakisha mwaka mmoja katika kandarasi yake Old Trafford na ameshindwa kuweka wazi iwapo atabakia United au ataelekea Madrid wanaohitaji huduma yake kwa udi na uvumba katika kipindi hiki cha usajili.

“Tutaona nini kitatokea juu ya mstakabali wangu,” De Gea aliliambia gazeti la AS la nchini Hispania aliko mapumzikoni kwa sasa baada ya kwisha kwa msimu wa ligi na kuisaidia United kushika nafasi ya nne na kurudi katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Licha ya sintofahamu hiyo, kocha wa mashetani wekundu Manchester United bado ana matumaini kuwa De Gea atabaki Old Trafford na kuisaidia United kushinda mataji katika msimu ujao.
De Gea(24) aliyejiunga na United akitokea Atletico Madrid kwa ada ya uhamisho wa pauni million 17.8, ameshaichezea Man United michezo 132 mpaka sasa na ameonekana kuzivaa vema ‘gloves’ za Mdachi Edwin Van De Sar aliyestaafu baada ya fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2008.
Kama De Gea ataondoka United, itamlazimu Luis Van Gaal kuingia sokoni na kutafuta mlinda mlango atakayechukua nafasi ya Mhispania huyo licha ya kuwepo kwa Mhispania mwingine Victor Valdes aliyesajiliwa katikati ya msimu uliopita kutoka Fc Barcelona.Tayari walinda lango kama Hugo Loris (Spurs), Asmir Begovic(Stoke City) na Jasper Cillesen(Ajax) wametajwa kama tazamio la Luis Van Gaal kama warithi wa mikoba ya De Gea kama kweli atahamia kwa mabingwa hao mara 10 wa Ulaya.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog