Wednesday, August 20, 2014


Marcos Rojo Tayari amewasili Nchini  England leo jumatano na akiwa tayri kupimwa afya kujiunga na  Manchester United msimu mpya 2014/15.Beki wa Sporting Lisbon Marcos Rojo ametoa fununu kubwa kwamba yeye na Mchezaji mwenzake wa Argentina Angel Di Maria wako njiani kuhamia Manchester United.Glory: The  winger helped Real Madrid win their 10th Champions League in Lisbon in May
Ripoti nzito toka huko England zimetoboa kuwa tayari Man United imewasilisha Ofa ya Pauni Milioni 50 kumnunua Di Maria kutoka Real Madrid na Kocha wa Klabu hiyo Carlo Ancelotti amekubali kumwachia Mchezaji huyo.
Big stage: Di Maria in action for Argentina at the World Cup, where they finished as runners-up
Klabu zote mbili, Sporting Lisbon na Man United, hazijatoa tamko rasmi lakini inasadikiwa ni kusubiri tu ukamilikaji wa taratibu zote ikiwemo upimwaji afya wa Wachezaji hao.

Jana Rojo, akiongea na Redio ya Nchini kwao Argentina, Kituo cha Radio Continental, Marcos Rojo, mwenye Miaka 24, alisema ameshakamilisha Uhamisho wa ‘Ndoto yake’ kwenda Man United.

Inaaminika Man United ilikubali kulipa Ada ya Uhamisho ya Euro Milioni 20 kwa ajili ya Rojo na pia kumtoa Winga wao Nani kwenda kwa Mkopo wa Msimu mmoja huko Sporting Lisbon. Klabu ambayo ndio alitokea na kujiunga na Man United Mwaka 2007.

Rojo alikaririwa kusema: “Ni kama ndoto kuwa Mchezaji wa Manchester United! Kuhama Sporting haikuwa rahisi!”

Hivi sasa zimeibuka ripoti kuwa Rojo aliisapoti Picha yake na Di Maria iliyowekwa kwenye Mtandao wa Instagram wakikumbatiana mbele ya Nembo ya Man United ikiwa ni ishara ya wazi kuwa wawili hao wako njiani kutua Old Trafford.

waliotembelea blog